DC Kahama Ageuka MbogoALIAGIZA JESHI LA POLISI KUMSAKA MTENDAJI WA KATA ALIYETOROSHA MKULIMA WA BANGI
Mkuu wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, ameliagiza jeshi la polisi wilayani humo kumtafuta na kumkamata Afisa Mtendaji wa Kata ya Mega, Peter Kupingwa, kwa tuhuma za kuhusika katika kumtorosha mkulima wa Bangi.
Mpesya ametoa agizo hilo jana baada ya kufika katika shamba lililokuwa limelimwa bangi hiyo lililopo katika kijiji cha Masabi, huku akiwa ameongozana na askari polisi na kukuta bangi hiyo imeshavunwa na kubaki miche kadhaa iliyochukuliwa kama ushahidi.na wananchi blg
0 comments:
Post a Comment