HABARI MPYA

Sunday 24 March 2024

TCAA YATOA MKONO WA PASAKA KITUO CHA KULELEA WATOTO CHA ZILI

 

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imekabidhi mahitaji kwa kituo cha kulea watoto cha ZILI kilichopo Kipawa Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kurejesha kwa jamii inayowazunguka.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mahitaji hayo yaliyogharimu kiasi cha Shilingi (TSHS) Milioni Moja, Afisa Habari na Mawasiliano wa TCAA Bi. Maureen Swai amesema Mamlaka imeguswa kutoa mkono wa Pasaka kwa kituo hiki ambacho kinalea watoto kumi kwa sasa.

Mkurugenzi wa kituo cha ZILI Bw.  Emanuel Zadock ameishukuru TCAA kwa kuguswa kuwashika mkono wakati huu na kuwaomba wadau wengine kuendelea kuvishika mkono vituo vinavyowatunza watoto wenye mahitaji kwani ni baraka kubwa sana. 

Afisa Uhusiano na Mawasiliano - TCAA Maureen Peter Swai(kushoto) akikabidhi msaada kwa Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto cha Zili House Bw.  Emanuel Zadock (kulia) ikiwa ni kurudisha kwenye jamii kwakusambaza upendo na tabasamu kwa watoto yatima wa kituo hicho kilichopo eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam. Msaada uliotolewa na TCAA ni mchele, Unga, mafuta ya kula, Taulo za Kike, sabuni, ngano nk.

Afisa Uhusiano na Mawasiliano - TCAA Bi. Maureen  Swai akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi msaada katika kituo cha kulelea watoto cha Zili ikiwa ni kurudisha kwenye jamii kwakusambaza upendo na tabasamu kwa watoto yatima wa kituo hicho hasa kwa kipindi hiki cha Sikukuu ya Pasaka.
Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto cha Zili House Bw. Emanuel Zadock akizungumzia historia pamoja na kutoa shukrani kwa viongozi pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa kuweza kutoa msaada kwenye kituo hicho kilichopo eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam.
Dorethea  Daniel akitoa neno la shukrani wa viongozi pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa kuweza kuwapatia msaada kituo hicho kilichopo eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) pamoja na watoto  wakisikiliza historia ya Kituo cha kulelea watoto cha Zili House wakati wa hafla ya kutoa msaada  katika kituo hicho
 Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)  wakiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Kituo cha Zili House pamoja na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho mara baada ya kukabidhi msaada ikiwa ni kurudisha kwenye jamii kwakusambaza upendo na tabasamu kwa watoto yatima wa kituo katika kituo hichokilichopo eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam.

Friday 19 January 2024

Wednesday 17 January 2024

HIZI NDIO TOFAUTI SITA(6) KATI YA UBONGO WA MWANAMKE NA MWANAUME



1. Ubongo wa mwanamke unaweza kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja; mfano kuzungumza kwenye simu na kufuatilia kipindi kwenye TV Mwanaume hawezi.


2. Lugha: wanawake wanaweza kujifunza lugha nyingi kwa urahisi. Chukua mtoto wa kike
na wa kiume wenye umri wa miaka mitatu. Mara nyingi wa kike atakuwa anajua maneno mengi kuliko wa kiume.




3. Kusema uongo: mwanaume akimdanganya mwanamke uso kwa uso ni rahisi kushtukiwa. Wanawake hugundua ukweli kupitia uso wako kwa 70%, kupitia body language yako 20% na 10% kupitia maneno yako. Ubongo wa mwanaume hauna uwezo huo ndiyo maana ni rahisi mwanamke kumdanganya mwanaume uso kwa uso.



4. Uwezo wa kutatua matatizo: mwanaume akiwa na matatizo, ubongo wake huyachukua na kuyatenga katika makundi mbalimbalina kisha huanza kutafuta suluhisho moja baada ya
jingine. Mwanamke akiwa na matatizo ubongo wake hauwezi kuyatenga na badala yake hutaka mtu amsikilize. Baada ya kumwambia mtu matatizo yake yote akili yake hupata kiwango fulani cha utulivu na huwa mara nyingi hajali kama yatatuliwa au la.




5. Mahitaji: Wanaume wanahitaji heshima kwenye jamii, mafanikio, sifa, nk.; wanawake wanapenda mahusiano, familia, marafiki, etc.



6. Kuongea: mwanamke mara nyingi hutumia lugha ya kificho. Mwanaume hutumia lugha ya moja kwa moja.

Thursday 11 January 2024

MAMBO MUHIMU KWA VIJANA WENZANGU.!

MUHIMU KWA VIJANA WENZANGU.!
Na Kdmula

Wengi itakuwa bado miaka miwili, mitatu au minne kabla ya kutimiza miaka 30. Natambua kuwa kuna waliokwisha fikisha na kuna uwezekano kuna walio nyuma kidogo.
Kama katika umri tulionao sasa kuna mtu anakuambia wewe bado ni mdogo/mtoto, basi huyo mtu hakupendi na anakulemaza kiakili. Kua! Acha utoto! Mambo yafuatayo kwa vigezo vya kibinadamu mwenye akili timamu, mtu mwerevu lazima uwe ushayatimiza.

1) Kuweka misingi ya kifamilia:
Katika umri huo unatakiwa uwe umeoa, umechumbia au uko katika uhusiano wenye kueleweka unaelekea kwenye kujenga familia. Kama katika umri huu bado unabadilisha wanawake na kudandia vicheche, basi sahau kuwa na familia imara. Mambo yafuatayo yatakuwa yanakunyemelea;
– Kuoa/kuolewa msichana/mvulana mdogo sana ambaye atakuona unamzeesha
– Kuoa /kuolewa chapchap bila kuwaza
-Kuokoteza magonjwa ya hatari
– Kunogewa na usela na kusahau kuoa/kuolewa
2)Kujitegemea kiuchumi:
Hapa simaanishi kufanya kazi na kupata mshahara pekee, la hasha! Hapa nalenga wale watoto wa mama ambao pamoja na kuwa wana kazi na mishahara, bado wanalalama mishahara haitoshi na kukimbilia kuomba hela nyumbani wanapoishiwa mara kwa mara. Wale ambao bado wanakaa nyumbani hii inawahusu pia. Pia wale wanaotumia 100% ya mishahara kununua vitu vinavyoisha (consumption) wakingoja wapate hela nyingi au wazazi, ndugu na jamaa wawasaidie kwenye uwekezaji. Africa tunachelewa sana kwenye hii sector.
3) Kuwa na kitega uchumi:
Kama unadhani mshahara wako wa milioni kadhaa ni mwingi sana, ngoja augue mtu wa karibu au wewe mwenyewe halafu daktari akuambie mgonjwa wako/wewe ana/unatakiwa ape/upelekwe nje ya nchi kwa matibabu zaidi wakati huna bima ya afya inayolipia hilo ndo utajijua kama mshahara wako heshima yake inaishia samaki samaki au inavuka border. Kitega uchumi si lazima uwe na mkampuni mkubwa, la hasha! Ila uwe na kitu cha kueleweka na chenye malengo ya kukua kuwa kitu cha maana. Kwa wale wagumu kuelewa, UNATAKIWA UWE NA PATO LA PEMBENI NJE YA MSHAHARA.
4) Makazi:
Uwe hata na kiwanja hapo Bunju Arif! Huezi kunywa bia kila weekend halafu wenzio wakiongelea issues za nyumba/viwanja/mashamba yao unakimbilia kubadilisha mada (Eti Huyu LVG wamuondoe kabisa anaharibu timu). Kumbe unazuga kupotezea story za viwanja/nyumba.
5)Uwe na professional qualification
: ACCA,CPA,CFA,CSIA,CPB, LAW SCHOOL ETC wale wa procurement wana ya kwao n.k. Ikifika huu umri kama CPA imekataa, tafuta hata mitihani za marketing upige, CPA sio issue zako. Lazima uwe na defined career (Kama hukubahatika kwenda kidato kingi, uwe na namna ya halali na ya kudumu ya kukupatia kipato). Umri huu kama huna utaalam katika fani yako, jiandae kuwa frustrated ofisini. Madogo wanasoma jamaa angu! Halafu wako tayari kupewa salary ndogo wapige kazi kuliko wewe.. So take care!
6) Uwe ushaamua ka hicho kitambi unakiondoa au unakilea:
Hapa sichekeshi! Kitambi kina madhara mengi. Suruali haikai vizuri, UTAPIGIWA, Kisukari, pressure n.k. Ukikinyamazia muda huu jua kitakuwa kishakomaa na majukumu yatakuwa mlima. Ukikiachia kijiamulie, kitakuganda kama “roba ya mbao” till death does you apart! Kama unakipenda endelea nacho, kama hukipendi uwe ushaweka program ya kukiondoa.
7)Uwezo wa kusaidia wanaokutegemea:
Kama we ni wa kishua, hapa hapakuhusu. Wewe ambaye si wa kishua, wazazi walikuwa na mategemeo flani walipokuwa wanakusomesha. Kama umefika miaka 30 hujaanza kuyatimiza mategemeo yao bila sababu ya msingi, jua watakuwa washakata tamaa na wewe.
8) Uwe na busara.
Kuwa mtu wa kufikiri kabla ya kutenda. Tengeneza haiba nzuri na ya kuheshimika kwa wanaokuzunguka. Kama huna busara hadi umri huu basi we sahau suala la busara ukiwa hai.. Labda utakutana nayo akhera.!
9) Savings:
Hapa nimeweka kizungu kuonyesha msisitizo. Kila mtu ana kipato chake. Ila formula ni kwamba angalau uwe ushahifadhi fedha sawa na mishahara yako ya mwaka na nusu gross of Tax kwa kipindi hicho. Kwa wale wagumu kuelewa namaanisha Ukiacha kazi au kusimamishwa kazi, uwe na uwezo wa kukaa mwaka na nusu bila kuingiza kitu chochote lakini uendelee kuishi maisha yale yale.
10) Umjue Mungu:
Nimeliweka hili mwisho si kwamba ni la mwisho kwa umuhimu, La hasha! Ni ili ulikumbuke zaidi. Mjue Mungu, mpende na umuogope. Nenda ibadani, soma neno lake na umuombe. Uwe na desturi ya kusali nyumbani kwako angalau kila unapoamka na wakati wa kulala. Kama humuogopi Mungu katika umri huu, basi wewe kwenda Mbinguni ni ngumu kuliko ngamia kupenya tundu la sindani (hata kama ni masikini).

Friday 29 December 2023

WASHINDI WA TCAA FUN RUN WAAGWA UWANJA WA NDEGE WA JNIA WAKIELEKEA DUBAI



Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini imeratibu zoezi la kuwaaga washindi watano wa mbio za kujifurahisha (FUN RUN) zilizofanyika Oktoba 29 jijini Dar es salaam zikiwa  sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 tangu kuundwa kwa TCAA.

Washindi hao walipata zawadi za tikteki kutoka kwa wadau wa Usafiri wa Anga ambao ni mashirika ya ndege ya Ethiopian Airlines, Kenya Airways na Fly Dubai ambapo wataelekea Dubai kwa mapumziko ya siku tano.
 
Akizungumza wakati wa kuwaaga, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho ya miaka 20 ya TCAA ambaye pia ni Meneja Mipango wa Mamlaka hiyo Bi. Mellania Kasese aliwapongeza washindi hao na kuyashukuru Mashirika yaliyotoa tiketi hizo kwa kutimiza ahadi hiyo na kuishukuru TCAA kwa kugharamia fedha za kujikimu kwa washindi hao wawapo katika mapumziko hayo.

"Ni siku ya sote kufurahia utimilifu wa zoezi hili kwa washindi wetu hawa watano ambao walipatikana miongoni mwa zaidi ya washiriki 300. Nawatakia safari njema na hii iendelee kuwa chachu ya kujali afya zenu lakini ikawe hamasa kwa wengine ili wajikite katika kuimarisha afya zao kwa mazoezi" alisema Mellania.

Meneja wa Shirika la Ndege la Ethiopia Bi. Seble Woldemariam amewapongeza washindi na kuwataka kutumia fursa hii kufanya utalii na kujifunza mengi mema na mazuri watakayojionea huko waendako. 



Meneja Mipango TCAA  Melania Kasese akizungumza na wanahabari wakati wa tukio la kuwaaga washindi wa TCAA FUN RUN waliojishindia tiketi za kuelekea Dubai ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)

Bw. Samuel Makalla mtumishi wa TCAA akielezea maandalizi aliyofanya kuelekea safari ya Dubai mara baada kuibuka mshindi  wa TCAA FUN RUN  kwenye Maadhimisho ya Miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)

Mtumishi wa TCAA Bw. Aidan Adrian ambaye ni miongoni mwa washindi akitoa shukrani kwa wote waliofanikisha zoezi hilo wakati TCAA FUN RUN iliyofanyika katika maadhimisho ya Miaka 20 ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) iliyopelekea kutangazwa mshindi wa mashindano hayo.
Mtumishi wa LATRA  Bw. Lugano Mwasomola ambaye ni miongoni mwa washindi akitoa shukrani kwa wote waliofanikisha zoezi hilo pamoja nasafari hiyo ya kwenda Dubai wakati wa hafla ya kuondoka hapa nchini kuelekea Dubai.


Meneja wa Shirika la Ndege la Ethiopia Bi. Seble Woldemariam (katikati) akizungumza wakati wa kuwaaga washindi wa tiketi ya kuelekea Dubai ambapo Shirika hilo ni miongoni mwa wadau waliotoa tiketi moja wapo kwa mshindi.

Meneja Mipango kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Melania Kasese akiwa kwenye picha ya pamoja na  washindi wa tiketi ya kuelekea Dubai  pamoja na viongozi wa Shirika la Ndege la Ethiopia  pamoja na Emirate wakati wa kuondoka nchini kwa ajili ya kwenda kutembea Dubai.

Wednesday 6 December 2023

TCAA YAIBUKA MSHINDI WA PILI NA KUPEWA TUZO YA UTENDAJI BORA WIZARA YA UCHUKUZI 2023


Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)  Bw. Hamza Johari tuzo ya mshindi wa pili ya kiutendaji miongoni mwa taasisi chini ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka 2023. 


Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)  Bw. Hamza Johari akifurahia tuzo ya mshindi wa pili ya kiutendaji miongoni mwa taasisi chini ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka 2023 mara baada ya kukabidhiwa.




Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)  Bw. Hamza Johari akiwa timu ya maonesho ya TCAA wakifurahia tuzo hiyo.


Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) yaibuka mshindi wa pili na kupokea tuzo ya kiutendaji miongoni mwa taasisi chini ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka 2023. 

Tuzo hiyo imekabidhiwa na Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa alipokuwa akizindua Mkutano wa 16 wa Tathimini ya Utekelezaji katika Uchukuzi na Usafirishaji jijini Arusha na kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari.

Tuesday 5 December 2023

THE MWALIMU NYERERE FOUNDATION RECEIVES $3M LONG TERM GRANT FROM GREYHORSE CLEARINGHOUSE LTD



Background and Summary
The Mwalimu Nyerere Foundation (MNF) of Tanzania has signed a $3M Endowment Fund Establishment Agreement with Greyhorse Clearinghouse limited, a fully owned subsidiary of Greyhorse Financial Corporation of USA. 

The purpose of this agreement is to operationalize an initially signed Memorandum of Understanding (MoU) providing a framework of cooperation and collaboration between Greyhorse Financial Corporation and the Mwalimu Nyerere Foundation in the implementation of a long term programme of promoting and consolidating institutional and individual self-reliance in Tanzania (Africa) in particular and in the world in general. The initial focus of this Fund Agreement will cover the establishment of a Non-Profit Institution Endowment Fund. 

This fund agreement, therefore initiate both institutional and individual endowment funds as part of endowment fund strategy for the promotion and consolidation of institutional and individual self-reliance as follows:

1. At the level of promotion and consolidation of institutional self-reliance, an endowment fund of US
$3,000,000 will be established.

2. At the level of individual promotion and self-reliance, the focus will be the allocation of endowment
funds in the following community groups:
Children education fund
Teachers fund
Mwalimu Nyerere Pan African Young Leaders fellowship virtual programme

Funding for the programme
The major initial funding for the programme will be from Greyhorse Clearinghouse limited which will
contribute an aggregate of US $3,000,000, over the ten (10) years term with annual contribution of
$300,000 distributed as follows: (A) up to $150,000, earmarked for general administrative functions of the Mwalimu Nyerere Foundation and (B) $150,000, into the MNF’s Mwalimu Nyerere Endowment Fund.

Individual children, adolescents, young men and women from the age of 0 to 20 years will be covered by an endowment scheme which will guarantee their capability to meet their costs of education, possibility to start and grow their business Individual teachers will be covered by an endowment scheme which will incentivize and motivate them and ensure terminal benefits to enable them to enhance their self-reliance capacity in provision of housing or any few economic undertaking.

African young men and women will be virtually trained in leadership for the promotion of peace, African  unity, and people centered self-reliance development including training for capacity building and stringent standards of integrity and ethical behavior for the betterment of society across Africa,

Projects and Initiatives
The programme will be implemented through detailed projects and/or initiatives which will cover areas of
initial focus on:
1. Mwalimu Nyerere Endowment Fund
2. Tanzania Children Education Fund
3. Tanzania Teachers Fund
4. Mwalimu Nyerere Pan African Young Leaders fellowship virtual programme

Additional informations on the Programme and stakeholders
This Endowment is entirely a private-sector initiative rooted in corporate trusteeship. It primarily addresses the institutionalization of result-oriented, commercialized financial interventions in aid of clear objectives of the MNF and all of its active stakeholders going forward. Topmost priority is accorded to financial inclusion via self reliance initiatives of the stakeholders and beneficiaries of the MNF, in all of their charitable and allied endeavours via the Foundation.

The scope of relevance of this Endowment is to consequentially bring together all facets of productive
operations of the Foundation for mutual advantage and that of the beneficiaries. The interest and co-
involvement of all stakeholders and representatives from the Foundation and its good works informs and helps to formulate the Endowment.

Administration and management of the Endowment is by Greyhorse Asset Management division acting
through a designated endowment trust council which includes selected expert personnel from the
Foundation.

Actual contribution and trusteeship are the direct responsibility of Greyhorse acting through its
collaborative proprietary worldwide financial networks under the leadership of its founder and executive chairman, Mr. Rahim Thawer, and its boards and associated firms and institutional funds in New York and London.

About Greyhorse Clearinghouse Ltd (UK).
Greyhorse Clearinghouse Limited is a Cross-Border Multi-Currency Blockchain~based Decentralized
Clearinghouse that provides custodial settlement services via its external fully collateralized funds.

Through its 100% Insured and Proprietary Digital Financial Infrastructure which allows Retail and Institutional Clients immediate Multi-Currency Liquidity. Registered Clients can also Lend, Borrow, Swap and Invest in Domestic and International Securities Markets through our Registered Affiliates as well as Securitize all of their Assets into Dollarization to Hedge against Currency Devaluation and/or Inflation.

Established in 2020 in London, UK. With Over US$1.967B in Assets Under Management Representing
institutional and retail clients. Greyhorse Clearinghouse Ltd is one of the Largest Decentralized
Clearinghouses and remains a leading service provider to various Financial Institutions in both Developed & Emerging Markets.

About The Mwalimu Nyerere Foundation (MNF)
The Mwalimu Nyerere Foundation (MNF) was established in June 1996 as a permanent tribute to Mwalimu Julius K. Nyerere’s contribution to improving sustainably the quality of human relations. The Foundation is a Non-Profit, not affiliated with any political party or government. It is an intellectually and politically independent body. The Foundation works to promote peace, unity and people-centred self-reliant development throughout the World and particularly in Africa.

The Foundation’s work is based on Mwalimu Nyerere’s belief in the fundamental principle that all humanity, regardless of their differences, are the purpose and justification for the existence of society; and all human activity in any given society. This philosophy demands that communities everywhere should enjoy and develop themselves within the context of freedom and democracy based upon good governance and social justice.

The Foundation believes that people are central to any process of development. Therefore, their culture,
needs, aspirations, desires and fears must set the development agenda. That development agenda is
legitimated through the people’s active participation in all decisions concerning their lives and livelihoods.

The absolute necessity for equity of access to resources, opportunities for prosperity, personal fulfilment, basic rights and community advancement must inform the process at all times.

The Foundation is dedicated offering service to the people by distinguished performance in working with people; encouraging, supporting and facilitating their activities in the process of their capacity building and search for prosperity and progress.


ZIFAHAMU HATUA TANO ZA KUKUJENGEA UJASIRI KATIKA TAALUMA YAKO




Je wewe hujiamini na elimu au taaluma yako? Ukiweza kujua kitu gani kinahitajika kwenye eneo fulani unaweza kusimama na kwenda juu zaidi ya woga ulionao.
Mambo yanabadilika pale ambapo tunaacha kuangalia tunahitaji nini au taaluma gani na badala yake tujue kinahitajika kitu gani na sisi tufanyaje? Maisha hubadilika na mambo huanza kwenda kwa mtazamo mwingine.
Hii ni kweli pale unapojifunza kwa uchungu mkubwa mara tu unapoingia kwenye ajira au taaluma mpya. Mara nyingi tunataka kupendwa au tunakubalika na watu, ni sawa lakini kitu cha muhimu ni kusimamia taaluma yako vizuri zaidi ili mambo yakuendee vyema.
Haijalishi hujui kwa kiasi gani linapokuja suala la taaluma kwenye eneo la kazi au biashara inategemea sana na mawazo yako umeyajenga wapi. Kama ni jasiri mambo yatakwenda vizuri na kama ni mwoga utaboronga tu. Taaluma kwa kifupi ni kiwango cha huduma unayotoa si idadi ya vyeti ulivyonavyo. Ukiweza kudhibitisha hilo watu watakuamini na watakuthamini kwa wewe kujiamini mwenyewe kwanza na usijidanganye kwa vile ambavyo hujui fanya juhudi ya kuvijua vitu hivyo mapema iwezekanavyo.
Kama mawazo yako yanatokana na ubunifu wa kile unachokiamini inawezekana ukawa sahihi katika huduma au kazi unayofanya.
Mbinu hizi chache zitakusaidia kuongeza ujasiri wako katika zile mbinu nyingine ambazo uko nazo au utaendelea kujifunza mbele ya safari yako kitaaluma.
1 – Sikiliza kile kinachohitajika – Je kwenye jambo lililo mbele yako kinahitajika nini? kinachokosekana ni nini?  Namna gani ya kuingia kwenye jambo hilo? Sikiliza na usiogope kuuliza maswali kabla ya kurukia jambo.
2 – Wakati wote jaribu kujibu au kufanya jambo kwa uwezo wako wa hali ya juu sana. Jambo linapotokea kwenye kazi au biashara watu wengi hukurupuka na kufanya maamuzi ya haraka au kukwaruzana na watu wengi na hata kutoa lugha chafu au zisizopendeza na kukasirisha wengine. Jitahidi kuwa mtulivu, na ujibu mada kitaaluma hata kama umechefuka kiasi gani, wewe utaonekana jasiri na mwenye mwelekeo mkubwa kitaaluma kuliko wengine.
3 –  Kama huna uhakika uliza swali, usijiweke chini au kujidharau na wala usipende kusema samahani kwa kitu ambacho si kosa. Uliza swali kama huna uhakika na hicho kinachoongelewa au kama hujui kumetokea nini. Usijiweke kwenye mazingira ya kudharaulika au watu kukupanda kichwani, maisha ya kitaaluma yatakuwa magumu kwako.
4 –  Tatua kwanza tatizo halafu kukasirika baadaye. Kuwa mtaaluma si jambo jepesi, jambo linapotokea uwe mtulivu na shughulika nalo halafu vitu vingine utahusika navyo baadaye baada ya utatuzi wa jambo. Ukikasirika sana hakikisha uko sehemu ambayo haina watu wengi, kwa usalama wa watu wengine na usalama wako pia. Usiruhusu msongo wa mawazo ukakuua, nenda nje ya tukio au chooni ili kurudisha akili yako kwenye mstari.
5 – Usitengeneze urafiki kwa kusengenya watu – Usijaribu kutengeneza kundi lako kutokana na uwezo wako wa kuzungumzia watu wengine. Hii itakufanya uwe na marafiki wasio sahihi. Utakuwa na watu wengi wanaokufuata kila mtu anatafuta maslahi yake kwako na si urafiki wa kweli.
Ukiwa msengenyaji ni vigumu sana kupata nafasi ya kukupeleka juu na hata ukienda juu ni ngumu kuwa na watu wanaopenda kufanya kazi na wewe. Kwa namna nyingine usitumie nafasi uliyonayo kudhuru watu wengine kitaaluma, unaweza kufurahia kabla hujagundulika ila kuna siku watu watakuchoka na wakishakuchoka wanakuwa tayari kwa jambo lolote lile.
Ujasiri wa kupambana na matatizo na si watu wengine, itakupa nafasi ya kutofautisha hisia na tatizo la kutafutiwa ufumbuzi. Ujasiri wakati mwingine unaweza kutikiswa, ingawa imani yako ya ndani haitokani na kile unakifanya bali unajiamini vipi kufanya kitu sahihi haijalishi mazingira yamekusonga kwa kiasi gani. Hiyo itakutengenezea viwango vyako vya kipekee katika taaluma yako, hutahitaji watu wakutetee bali msimamo wako na ujasiri utawavuta watu na wapende kufanya kazi pamoja na wewe.

Monday 4 December 2023

Thursday 23 November 2023

WATUMISHI WA TCAA WAPONGEZWA KWA UTENDAJI KAZI KWA WELEDI




Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S. Johari (katikati) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la TCAA wakati wa kufungua kikao hicho. Kulia ni Bi. Massa K. Mumburi Katibu Msaidizi wa Baraza, Kushoto ni Katibu wa Baraza Bw. Dedacus Mweya






Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Sara Rwezaula akitoa pongezi wakati wa kikao cha Baraza


Katibu wa Baraza Bw. Mweya Dedacus akiwasilisha mrejesho wakati wa Baraza


Afisa Uchunguzi, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Bw. Silvanus Njenga akiwasilisha mada kuhusu Maadili ya Utumishi wa Umma


Menejimenti ya TCAA ikifuatia wasilisho la maadili.





Wajumbe wa Baraza wakiendelea kufuatilia mada hiyo


Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), wamepongezwa kwa kuendelea kufanya Baraza la Wafanyakazi lenye tija lililofanya mamuzi makubwa yenye tija kwa kutuoa huduma bora na kukuza sekta ya usafiri wa anga nchini.


Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi la TCAA uliofanyika Novemba 23,2023 makao makuu ya Mamlaka Banana jijini Dar es salaam.


Bw. Johari  amewasifu wajumbe wa baraza kwa kufanya kuweka mbele maslahi ya taasisi na kuwasilisha hoja zinazoichochea menejimenti kutekeleza majukumu yake vyema. Pia ameongeza kuwa vikao hivyo vya Baraza ni njia bora ya kuimarisha demokrasia mahala pa kazi,na kuwataka wajumbe wa Baraza hilo kurudisha mrejesho kwa watumishi wenzao.


”Kama tunavyofahamu Mamlaka imetekeleza na inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati ukiwemo wa Ununuzi wa Rada nne za kuongozea ndege, kuboresha Mfumo wa Masafa ya Mawasiliano wa Sauti baina ya rubani na waongozaji ndege katika vituo vyote vya kuongozea ndege nchini na Mradi wa kuimarisha na kuboresha utoaji taarifa za anga kuwa dijitali na yote hii ni mazao ya mawazo na hoja muhimu mnazoleta hapa na kwa pamoja tunapata ufumbuzi” alisema Bw. Johari.

Awali akiwasilisha salamu kwa niaba ya Chama cha Wafanyakazi Mkoa wa Dar es Salaam (TUGHE) Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Sara Rwezaula ameupongeza uongozi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania kwa kuteleza majukumu yake kwa namna shirikishi kwani inafanya kila mtumishi kujisikia sehemu ya Mamlaka na hivyo kuongeza ari ya utendaji kazi.

Akitoa maelezo ya jumla, Katibu wa Baraza hilo Bw. Mweya Dedacus amesema hichi ni kikao cha sita cha Baraza ambacho dhima kuu ni kuwasilisha mrejesho wa yale yaliyokuwa yamejadiliwa na kuazimiwa wakati wa kikao kilichopita cha Baraza kilichofanyika mwezi Aprili.

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA