Monday 31 March 2014

WATU 21 WAFARIKI, 10 WAJERUHIWA KATIKA AJALI YA HIACE RUFIJI..

Watu 21 wamekufa na 10 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi dogo la abiria aina ya Hiace na lori.
Ajali hiyo ilitokea juzi katika kijiji cha Mkupuka kata ya Kibiti wilayani Rufiji mkoani Pwani.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 2:00 usiku baada ya basi hilo dogo la abiria lenye namba za usajili T 194 CUX likitokea Ikwiriri kujaribu kupita gari lingine aina ya lori aina ya Tata lenye namba za usajili T 132 AFJ.
Basi hilo la abiria lilikutana uso kwa uso na lori lingine aina ya Canter lenye namba za usajili T 774 CJW.
Alisema  majeruhi walipelekwa hospitali ya Misheni ya Mchukwi huku maiti zikiwa zimehifadhiwa kwenye Hospitali ya Ikwiriri kwa ajili ya kutambuliwa. Hadi jana, majina ya marehemu yalikuwa hayajafahamika.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA