Thursday, 24 April 2014

HUYU SI YESU JAMANI..SOMA ZAIDI HAPA...

Mtume na Nabii Hebron Wilson Kisamo amesema picha ya Yesu Kristo inayotumiwa na baadhi ya madhehebu ya Kikrito duniani siyo ya mwokozi huyo wa roho za watu. 

Mtume na Nabii Hebron Wilson Kisamo mwenye kanisa lake maeneo ya Moshono, Arusha.
 Nabii huyo ambaye ana kanisa lake maeneo ya Moshono, Arusha aliyasema hayo hivi karibuni kupitia kituo kimoja cha runinga nchini. 
Alisema watu wengi katika ulimwengu huu hawaijui sura halisi ya Yesu Mnazareti bali wamemuona mwigizaji wa sinema za Yesu aitwaye Brian Decon makanisani, majumbani, kwenye biashara, kwenye misalaba na wamemfanya kuwa ndiye mwokozi wao.
“Watu hususan Wakristo wanaiabudu hiyo picha ya huyo mwigizaji anayeitwa Brian aliyeigiza kuwa Yesu. Ni vizuri alivyoigiza, hii imesaidia kufundisha watu kuhusu Yesu kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Injili ya Luka,” alisema Nabii  Hebron.



Picha ya mwigizaji maarufu wa sinema za Yesu aitwaye Brian Decon.
 Akaongeza: “Mimi katika maisha yangu pia ufahamu ulitekwa ukaona ile picha ya Brian ndiyo Yesu kutokana na jinsi nilivyofundishwa toka utoto wangu katika madhehebu ya Kikristo. “Hata sasa inawezekana na wewe unayo picha ya Brian na unaiita picha ya Yesu , hili ni kosa,” alifafanua kuwa cha ajabu ni kuwa ukiingia katika baadhi ya makanisa utaona picha za Brian zimetundikwa ukutani na ndizo watu wanaziabudu.
 “Hapa watu wamepotea na ni mbaya kuiabudu picha ya mwanadamu, natumaini hata yeye Brian hapendi aitwe Yesu, maana Yesu tunayemjua alikufa na kufufuka na sasa yupo mbinguni na hata kuzaliwa kwake ni kwa njia ya Roho Mtakatifu,” alisema nabii huyo. Alifafanua kuwa, Yesu hakuwa mzee kama huyu muigizaji Brian aliyetumika kuifundisha jamii kwa njia ya sinema ili watu waelewe kirahisi na wapate mfano ilivyokuwa siku hizo. Alijigamba kuwa aliwahi kutokewa na Yesu akaongeza:
 “Mara ya kwanza kumuona Yesu sura sikuiona hii ambayo ipo hapa ulimwenguni na inauzwa madukani. Yesu anang’aa, picha yake ipo kwenye macho yangu na haipo mahali popote katika ulimwengu huu, haifanani kabisa na mtu yeyote na ndiyo maana anaitwa mwana wa pekee wa Mungu.” Alisema  watu wengi badala ya kumuangalia Yesu katika roho sasa fahamu zao zimetekwa na shetani, wanaziona picha za muigizaji kuwa ndiye Yesu na madhara ya kukaa na hizo picha ukutani na kuzibusu ni kwenda kwenye mlango wa kuzimu na kuzisujudia utakuwa tayari umeabudu sanamu,” aliionya dunia.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA