HIZI NDIZO SABABU 10 ZA WANAWAKE WENGI KUACHIKA MAPEMA SIKU HIZI
1) Kwanza kabisa ni wavivu kwenye swala zima la mahaba, eti wanadai
wamechoka na mihangaiko akirudi nyumbani yeye anakula tu kisha analala,
hapo ujue ndio haamki mpaka asubuhi akitaka kwenda kazini.
2) Hawajitumi, atakavyo kaa ndio hivyo hivyo mpaka mwisho wa mchezo, haangaiki wala hajihangaishi.
3) Akishapata tu kazi ndio balaa kabisa anakuwa busy na kujifanya amechoka kama anaumba watu.
4) Kama mume wake hajisikii yeye pia hajisikii, yani hawezi kumleta
mumewe kwenye mood ya mapenzi hajisumbui kufanya utundu kwani nae
anajiona yuko juu hana huo muda
5) Siku zote anasubilia yeye aanzwe , yeye kuanza hataki . Yani mpaka
uanze kumchezea na kumuimbisha kama vile demu mpya kumbe mkeo.
6) Akipata pesa yeye hizo ni za kwake na matumizi yake tu binafsi,
majukumu kwenye familia yeye hataki keshajitoa, pesa za mwanaume ndio
zitumike hadi kumnunulia pedi zake.
7) Wanamaneno mengi hadi muda mwengine huwakosea heshima waume zao,
mwanamke kuongea sana haipendezi. Mwengine ukimkuta anaongea na mume
wake utafikiri anaongea na konda
8) Wanajali marafiki zako kuliko hata waume zao wa ndani
9) Mitandao ya kijamii inawaponza sana dada zetu, ndoa zina vunjika
kila siku. Wala hakuna cha maana niumbea tu na kupost picha kila muda
instagram na facebook. wewe umeshaolewa huko instagram unampostia
nani,na ili iweje.
10) Kuzurula, mwanadada unakuta anazurula utafikiri anashughuli ya
maana, tena bora azurule na atoe taarifa anaenda wapi lakini walaa
mwanamke anatembea kama dalali, mara magomeni, mara kinondoni mara
mwananyamara mara sinza yani kama vile muuza urembo. mjirekebishe la
sivyo mtaachika mpaka mkione cha moto.
NA MWEUSI CLASIC
0 comments:
Post a Comment