DIEGO COSTA AZOMEWA NA MASHABIKI WA BRAZIL AKIICHEZEA HISPANIA DHIDI YA UHOLANZI
Alizomewa : Mshambuliaji, Diego Costa alizomewa na Wabrazil wakati Hispania ilipopambana na Uholanzi.
DIEGO Costa amezomewa na mashabiki wa Brazil katika mchezo wake wa kwanza katika ardhi ya nchini mwake tangu alipochagua kuwachezea wapinzani wa `Samba Boys` , Hispania, katika mbio za ubingwa wa fainali za kombe la dunia mwaka huu.
Mshambuliaji huyo ambaye yuko mbioni kujiunga na Chelsea alianza katika kikosi cha kwanza cha Hispania dhidi ya Uholanzi kwenye mchezo wa ufunguzi wa kundi B, lakini alipokelewa na kelele za kuzomewa kwa kitendo chake cha kuikimbia nchi yake.
Aliichezea Brazil katika mechi mbili, zote za kirafiki kabla ya yeye mwenyewe kuandika barua FIFA akiomba kuichezea Hispania ambapo ombi lake lilikubaliwa mwezi octoba mwaka jana.
Wakati wakijiandaa na mechi ambayo ilikuwa kama ya marudiano ya fainali ya mwaka 2010 dhidi ya Uholanzi, Costa alisema aliondoka Brazil kwa mapenzi yake mwenyewe na kujiunga na Hispania.
"Nimethibitisha Hispania ndio taifa langu na watu wa Hispania wapo nyuma yangu". Alisema. "Ukosoaji wa maamuzi yangu hauniathiri".
"Brazil ni washindani wa ubingwa, lakini wapo katika presha kubwa kutoka kwa mashabiki wao.Watu wanahitaji kuwaona fainali na hiyo inawapa ugumu zaidi".
Baada ya kuiona Brazil ikipata ushindi katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Croatia, Costa katika mchezo wa usiku huu amesababisha penati iliyofungwa na Xabi Alonso na kuwapa Hispania bao la kuongoza.
Nyota huyo mwenye miaka 35 yuko mbioni kujiunga na Chelsea majira ya kiangazi mwaka huu kwa dau la paundi milioni 32, lakini sasa ana presha na taifa la Hispania linalohitaji kutetea ubingwa wa kombe la dunia.
0 comments:
Post a Comment