WANA JIHAD WAUWA WATU 700 SYRIA
14:24 |
No Comments |
Wapiganaji wa Islamic State
Shirika linalochunguza maswala ya kibinaadamu nchin Syria lenye makao yake nchini Uingereza limesema kuwa wapiganaji wa Islamic state wamewaua watu 700 wa kabila moja mashariki mwa Syria katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.
Shirika hilo limesema kuwa wengi wa waathiriwa wanatoka katika kabila la al-Sheitaat katika mkoa wa Deir al-Zor ambapo raia waliuawa bila kupewa mda wa kujitetea.
Waandishi wanasema pande hizo mbili zilianza kupigana katika jimbo moja lenye utajiri wa mafuta baada ya kutofautiana .
Awali ,rais wa muungano wa upinzani nchini Syria Hadi Al Bahra alitoa wito kwa ulimwengu kuingilia kati nchini Syria ili kukabiliana na tishio la wanamgambo wa Islamic state.
Mchanganuzi wa BBC katika eneo la mashariki ya kati amesema kuwa serikali ya Syria mara chache hushambulia kambi za Islamic State hatua iliosababisha wapiganaji hao kujiimarisha ikilinganishwa na makundi mengine ya waasi.
-BBC
Related Posts:
Saudi Arabia yawatimua wanadiplomasia wa Iran Mfalme wa Saudi Salma bin Abdul-Aziz al-Saud. Saudi Arabia imevunja uhusiano wa kidiplomasia na Iran, baada ya waandamanaji kuuvamia ubalozi w… Read More
WABUNGE UINGEREZA WAMJADILI TRUMP Donald Trump ametaka waislamu kupigwa marufuku kuingia nchini Marekani Wabunge wa Uingereza wamekuwa na mjadala kuhusu kupigw… Read More
FAMILIA UCHINA ZARUHUSIWA WATOTO WAWILI Sera ya kuruhusu mtoto mmoja pekee katika familia ilianza kutekelezwa 1978 Familia nchini Uchina sasa zimeruhusiwa kupata wato… Read More
WATU WAWILI WAUAWA NA MSHAMBULIAJI TEL AVIV Polisi wanamsaka mwanamume aliyetekeleza uvamizi huo Watu wawili wamefariki na wengine watano kujeruhiwa baada ya mtu mwenye silaha kufyatulia w… Read More
UN: MAELFU YA RAIA WAMEUAWA IRAQ Takriban watu milioni 3.2 wamelazimika kuhama makwao nchini Iraq Umoja wa Mataifa unasema kuwa ghasia zinazowakumba raia nchi… Read More
0 comments:
Post a Comment