Monday 22 September 2014

WACHEZA KAMARI WACHAPWA BAKORA MSIKITINI

Watu nane walichapwa bakora kwa kvunja sheria ya Kiisalmu kwa kucheza kamari.
Watu nane walichapwa bakora mbele ya watu 1,000 ndani ya msikiti nchini Indonesia baada ya kuvunja sheria ya Kiislamu kwa kucheza kamari.

Mwendesha mashtaka wa nchi, kwenye jimbo la Aceh, kaskazini-magharibi mwa Sumatra, alisoma adhabu hiyo mbele ya mtu aliyejifichwa uso akiwa amevaa nguo ndefu ya hudhurungi.
Akitumia fimbo nyembamba ya mti wa mpingo, aliwachapa kwenye makalio watu hao fimbo tano kila mmoja.
Watu hao walichapwa bakora tano kila mmoja kwa fimbo ya mti wa mpingo katika eneo la msikiti wa jimbo la Aceh, Indonesia.
Watu hao walichapwa bakora tano kila mmoja kwa fimbo ya mti wa mpingo katika eneo la msikiti wa jimbo la Aceh, Indonesia.
Msikiti ulijawa na watu wakati wa adhabu hiyo iliyofuatiwa na ibada ya Ijumaa asubuhi.
Adhabu hiyo ya fimbo ilifuatia baada ya kukamatwa watu tisa kwa kucheza kamari mwezi Julai. Polisi walikamata kisasi cha pauni 80 (208,000) kutoka kwa watu hao.
Adhabu hiyo ilifanywa na mtu aliyekuwa amevaa nguo ndefu ya hudhurungi baada ya mashtaka kusomwa na mwendesha mashtaka wa nchi.
Adhabu hiyo ilifanywa na mtu aliyekuwa amevaa nguo ndefu ya hudhurungi baada ya mashtaka kusomwa na mwendesha mashtaka wa nchi.
Mmoja wao hakuweza kuchapwa kwa sababu ya afya yake ila atakabiliana na adhabu hiyo atakapopona, alisema mwendesha mashtaka wa nchi Nurhalma ambaye anatumia jina moja tu.

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA