Tuesday, 11 November 2014

HIVI NDIVYO ILIVYOKUA MAHAKAMANI KESI YA MADAWA YA KULEVYA INAYOMKABII CHID BENZ!

Chid Benz (kushoto mwenye shati la bluu) akiingia katika lango la mahakama.

...Akiingia katika chumba cha kusikiliza kesi inayomkabili.
...Akitimua mbio kutoka lango la mahakama kuogopa kamera za mapaparazi.
...Akionyesha mkono kupinga kupigwa picha.KESI ya msanii muziki wa kizazi kipya, Rashid Makwiro ’Chid Benz’, imeahirishwa tena leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hadi Desemba Mosi mwaka huu. 
Msanii huyo anakabiliwa na kesi ya kukamatwa na madawa ya kuletvya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jiji Dar es Salaam wakati akisafiri kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya kutumbuiza.
Upande wa mashitaka ukiongozwa na mawakili wawili Ofmed Mtenga na Leonard Challo mbele ya Hakimu Waliarwanda Lema, umesema upelelezi bado haujakamilika nakutaja tarehe ya kusikilizwa kesi hiyo Desemba mosi.
-gGPL

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA