HII NDIO JAMII YA AJABU AMBAYO HUKATWA VIDOLE KATIKA KILA MAOMBOLEZO YA MSIBA WA NDUGU...
Hii imeshtua wengi walioisikia, kwa wale waliobahatika kuitembelea basi ni mashuhuda kwamba watu wengi wa kutoka jamii hiyo wamekatwa vidole na ndugu yoyote wa marehemu anakatwa vidole, umri sio kitu kinachoangaliwa sana hivyo hata watoto pia wanaguswa na hii moja kwa moja.
Utaratibu huo huwa unakuwa na ibada ya utangulizi ili kufukuza mapepo ya marehemu halafu linafuatia zoezi la kukata vidole, kwa utamaduni huo maumivu ya mwili huonyesha huzuni ya kufiwa pamoja na kuonyesha upendo kwa marehemu.
Hapa vidole vinakatwa kwa shoka, vipande vilivyokatwa vinachomwa moto halafu majivu yanahifadhiwa au kuzikwa pamoja na mwili wa marehemu.
Jitihada zimeanza kufanywa ili kuzuia utamaduni huo ambao madhara yake yameanza kuonekana kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment