MSICHANA AONGOZA MATOKEO KIDATO CHA NNE, ZIJUE SHULE KUMI BORA
Baraza
la mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne
wa mwaka 2015 yanayoonesha kiwango cha ufaulu kushuka kwa asilimia 0.80.
Akitangaza
matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles Msonde amesema
kuwa jumla watahiniwa 272,947 sawa na 67.53% ya watahiniwa wote
waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2015 wamefaulu tofauti na mwaka
2014 ambapo ufaulu ulikuwa 68.33%.
Msonde
amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, waliofaulu ni 240,996 sawa
na asilimia 67.91 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 11,125 (64.84)
na wavulana wakiwa 124,871 (71.09).
Amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, ufaulu umeshuka kwa asilimia 1.85 ikilinganishwa na mwaka 2014.
Aidha
kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, Dkt Msonde amesema watahiniwa
31,951 sawa na asilimia 64.80 wamefaulu ikilinganishwa na watahiniwa
29,162 (61.12) waliofaulu mwaka 2014.
Kwa
upade wa ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa
wa shule, Msonde amesema waliopata daraja la kwanza ni 9,816 sawa na
asilimia 2.77, daraja la pili ni 31,986 sawa na asilimia 9.01, daraja la
tatu ni 48,127 sawa na asilimia 13.56.
Aidha
waliopata daraja la nne ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 na waliopata
daraja la sifuri (waliofeli) ni 113,489 sawa na asilimia 32.09.
Watahiniwa
waliopata ufaulu mzuri wa kati ya daraja la kwanza hadi la tatu ni
94,941 sawa na asilimia 24.73 wavulana wakiwa 56,603 sawa na 29.99 na
wasichana 38,338 sawa na asilimia 19.63.
Amesema
kwa upande wa ufaulu wa masomo kwa watahiniwa wa shule, ufaulu wa juu
kabisa ni wa somo la Kiswahili ambapo asilimia 77.63 wamefaulu huku
ufaulu wa chini kabisa ukiwa ni wa somo la Basic Mathematics ambapo
asilimia 16.76 wamefaulu.
Baraza
hilo limezuia matokeo ya watahiniwa 121 kutokana na sababu za kiafya na
watahiniwa hao wataruhusiwa kufanya mitihani ambayo hawakuifanya katika
mtihani wa kidato cha nne, mwaka 2016.
Aidha
baraza hilo limefuta matokeo ya watahiniwa 87 waliobainika kufanya
udanganyifu katika mtihani ambapo kati yao 25 ni wa kujitengemea na 52
ni watahiniwa wa shule wakati 10 ni wa mtihani wa maarifa (QT)
Amezitaja shule 10 zenye watahiniwa zaidi ya 40 zilizofanya vizuri zaidi
kuwa ni Kaizerege ya mkoani Kagera, Alliance Girls ya Mwanza, St.
Francis Girls ya Mbeya, Canossa ya Dar es salaam, Marian Boys ya Pwani,
Alliance Rock Army ya Mwanza, Feza Girls Dar es salaam, Feza Boys ya Dar
es salaam na Uru Seminary ya Kilimanjaro.
Shule 10 zilizofanya vibaya zaidi kwa watainiwa zaidi ya 40 ni pamoja na
Pande ya mkoani Lindi, Igawa ya Morogoro, Korona ya Arusha, Sofi ya
Morogoro, Kurui ya mkoani Pwani, Patema ya Tanga, Saviak ya Dar es
salaam, Gubali ya Dodoma, Kichangani ya Morogoro na Malinyi ya Morogoro.
Kwa
upande wa watahiniwa, Dkt Msonde amesema kati ya watahiniwa 10
waliofanya vizuri zaidi, wanne na wasichana na sita ni wavulana.
Mwanafunzi aliyeongoza ni msichana Butogwa Charles Shija wa Canossa, akifuatiwa na msichana mwingine Congcong Wang wa Feza Girls na wa tatu ni mvulana Innocent Lawrence wa Feza Boys.
Wengine
ni Dominick Marco Aidano wa Msolwa, Sang'udi E Sang'udi wa Ilboru,
Asteria Herbert Chilambo waCanossa, Belinda Jackson Magere wa Canossa,
Humfrey Martine Kimanya wa Msolwa, Bright B Mwang'onda wa Marian Boys na
wa 10 ni Erick R Mwang'ingo wa Marian Boys.
Matokeo
hayo yamepangwa katika mfumo wa madaraja (Division) badala ya ule wa
wasatani wa alama (GPA) kama ambavyo iliagizwa na Waziri wa Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Ufundi hivi karibuni.
KUANGALIA MATOKEO
0 comments:
Post a Comment