Thursday 19 May 2016

WANAFUNZI KUTOKA UGANDA WASHUKURU MSAADA WA TBL




Chama cha wanafunzi wa Uganda wanaosoma katika vyuo vikuu vya Tanzania (USAT) wameishukuru kampuni ya Bia ya Tanzania kwa kuwapatia msaada wa kuwawezesha kununua mahitaji mbalimbali ya kusaidia vituo vya  watoto yatima.


Akipokea msaada wa fedha zilizotolewa na TBL,mwakilishi wa wanafunzi hao Alex Kalanda alisema kuwa wamekuwa na utaratibu wa kutembelea vituo yatima na kushiriki shughuli za kijamii hivyo walipeleka ombi la kuwezeshwa kupatiwa fedha za kununulia mahitaji ya kwenda nayo ya kusaidia watoto kwenye vituo watakavyotembelea.

“Kwa niaba ya wenzangu nashukuru TBL kwa kutuunga mkono ili tuweze kutimiza dhamira yetu.
Kwa upande wake Meneja wa kampuni ya Bia Tanzania katika kiwanda cha Ilala akiongea muda mfupi baada ya kukabidhi msaada huo alisema kuwa kampuni hiyo siku zote inafanya kazi kwa karibu na wanafunzi kwa kuwa inaamini ndio  wafanyakazi wake wa baadaye.

Alisema TBL imekuwa ikishiriki katika kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu lijulikanalo kama AISEC ambapo wawakilishi wamekuwa wa kampuni wamekuwa wakiongea na wanafunzi na kuwapatia miongozo mbalimbali ya kupata ajira na kumudu kufanya kazi kwenye makampuni makubwa.

Alisema katika kongamano lililofanyika mapema mwezi uliopita jijini Dar es Salaam wanafunzi wengi walionyesha nia ya kufanya kazi katika kampuni ya TBL watakapomaliza masomo yao.

Meneja wa TBL kiwanda cha Ilala,Calvin Martin (kushoto) akikabidhi fedha kwa mwakilishi wa chama cha wanafunzi wa Uganda  wanaosoma nchini (USAT) Alex Kalanda (kulia) kwa ajili ya kusaidia vituo vya watoto yatima,mwingine pichani (katikati) ni mwanafunzi kutoka Uganda Ivan Bakimyuse.
 

 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA