DONALD TRUMP KUWEKA MAZINGIRA MAGUMU KWA WATOAJI MIMBA
Donald Trump amesema yeye ni muumini wa kutetea uhai, hivyo basi wanawake wajawazito wanaotaka kutoa mimba watalazimika kusafiri kwenda kwenye majimbo yenye sheria inayoruhusu utoaji mimba kwa kuwa hatohalalisha utoaji mimba kwenye majimbo yote.
Akiongea kwenye mahojiano na kituo cha CBS, amesema atamchagua Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ambaye naye ni muumini wa kutetea uhai, ili kuhakikisha mahakama hiyo ya juu nchini Marekani hairuhusu sheria za utoaji mimba.
Katika mahojiano hayo yaliyorushwa jumapili, Trump amethibitisha nia yake ya kujenga ukuta katika mpaka na Mexico, ingawa amekiri katika baadhi ya maeneo ataweka fensi, na kuahidi kuwarejesha kwao wahamiaji milioni 2 ama milioi 3 wenye rekodi za uhalifu.
Donald Trump akifanya mahojiano kwenye jumba lake la kifahari
0 comments:
Post a Comment