SENEGAL, NIGERIA KUIVAMIA GAMBIA KIJESHI ILI KUMNG'OA RAIS YAYHA JAMMEH ALIYEGOMA KUACHIA MADARAKA
Jeshi la Senegal limesema kuwa majeshi ya Afrika Magharibi yataingilia suala la Gambia usiku wa kuamkia tarehe ya mwisho wa madaraka ya Rais Yayha Jammeh ambayo ni leo ili akabidhi madaraka kwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanywa mwezi uliopita ,Adama Barrow ambaye kwa sasa yuko nchini Senegal..
Vikosi kutoka Senegal vimesogea katika mipaka ya Gambia, Nigeria pia imetuma vikosi vya anga katika eneo hilo.
Senegali imeomba Jumuiya ya Usalama ya Umoja wa Mataifa kushinikiza Umoja wa nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) kuchukua hatua za msingi katika kuhakikisha Rais mteule wa Gambia anakabidhiwa madaraka.
Kwa nini Senegal inaongoza Mpango wa Kumng'oa?
Ecowas, Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, iliipa Senegal jukumu hilo kwa sababu taifa hilo linaizunguka Gambia.
Kanali Abdou Ndiaye, msemaji wa jeshi la Senegal, amesema Ecowas iliamua kumuwekea Jammeh mkakati huo ili kujaribu kupata suluhu ya kidiplomasia.
"Mambo yote yako tayari na wanajeshi wa Ecowas wako tayari kuingilia kati baada ya saa sita iwapo hatutapata suluhu ya kidiplomasia kwa mzozo huu wa Gambia," alisema.
Wanajeshi hao wa Ecowas wanasubiri Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lipitishe azimio la kutumiwa kwa "hatua zozote zile" kusaidia kuondolewa madarakani kwa Be Jammeh. Wanajeshi wote wa Gambia ni takriban 2,500.
Nigeria imesema imetuma ndege za kivita na ndege nyingine za kawaida, pamoja na wanajeshi 200 nchini Senegal. Wanajeshi hao walienda Senegal Jumatano asubuhi.
Meli za kivita za Nigeria pia zimewekwa tayari baharini.Manowari moja iliondoka Lagos Jumanne na itakuwa na jukumu la kuwaokoa raia wa Nigeria walio nchini Gambia.Ghana pia inachangia wanajeshi
Credit: BBC
0 comments:
Post a Comment