Wednesday 29 March 2017

RAIS MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO WA MAWAZIRI WA TANZANIA NA UGANDA ULIOONGELEA MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI KUTOKA HOIMA HADI TANGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kikao cha pamoja cha Mawaziri wa Serikali za Tanzania na Uganda pamoja na wadau kuzungumzia mradi wa ujenzi wa Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Mkutano huo, uliofanyika Ikulu, Dar es salaam Jumanne Machi 28, 2017, ulihudhuriwa na Mawaziri wa Nishati na Madini pamoja na Mawaziri wa Ardhi wa nchi hizo mbili, Wanasheria wa Serikali  na kampuni washirika wa mradi huo Lake Albert (CNOOC, TOTAL na TULLOW).

Pamoja na mambo mengine, Mawaziri, Maafisa na Wataalam wa pande zote husika walikaa na kukubaliana kwamba rasimu ya  makubaliano rasmi ya kuanza kwa mradi yawe yamekamilika na kuwa tayari katika kipindi cha wiki mbili ili kuwezesha Marais wa Tanzania na Uganda kuweka jiwe la msingi kuashiria kuanza ujenzi wa kihistoria wa mradi huo wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga, Tanzania. 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA