MAWAKALA WAKIMATAIFA WA MATANGAZO HAVAS GROUP WAINGIA TANZANIA
Havas Group ni moja kati ya mawakala wakubwa
wa matangazo ya biashara yenye mtandao mpana duniani kote. Ikiwa na makao makuu
nchini Ufaransa, Havas inapatikana katika nchi 149 zikiwemo nchi 19 barani
Afrika ambapo wana ubia na kampuni nyingine. Havas Group,imegawanyika mara
mbili katika Afrika - Havas Media Africa & Arena Media Afrika.
Kihistoria, Havas imejikita kwa nguvu zaidi
kwenye nchi zinazoongea lugha ya kifaransa zikiwemo,Cameroon, DRC, Ivory Coast
& Senegal kuwa ndio nguzo yao katika ukanda huo. Nyingine ni pamoja na
Gabon, Niger, Burkina, Benin, Togo.
Hivi karibuni,Havas imekuwa kwa kasi katika
ukanda wa Afrika Mashariki, ikianzia na Kenya kwa miaka 5 iliyopita. Uganda na
Rwanda zilifunguliwa mwaka jana wakati Zambia ipo kwenye mipango ya kufunguliwa mwishoni mwa mwaka huu. Ofisi za Tanzania zimekuwa zikifanya kazi
tangu mwaka 2015 na tangu wakati huo hakuna kurudi nyuma. Hadi sasa tayari ina
wateja wa kimataifa kama vile Emirates, Airtel & DTCM, biashara ya Tanzania
inakua kulingana na mahitaji ya soko la media linaloongezeka siku hadi siku.
Shughuli za Havas Africa huratibiwa na
kusimamiwa na kitengo cha Havas Afrika chenye makao makuu mjini Paris,ikikuza
utaalamu kimataifa, zana na maarifa kwa masoko yote.Mtindo wao wa kufanya kazi
huhakikisha kwamba kuna uthabiti na utendaji bora katika matawi yao yote, ili kuinua na kuleta
mawakala wote kwenye kiwango cha ubora kilicho sawa.
Kinachoitofautisha Havas ni mbinu za utumiaji wa takwimu na namna yao
ya kipekee ya kuweka matangazo ya bidhaa kwenye mtandao. Ndani ya mazingira ya
Afrika, Havas tayari imepiga hatua mbele
na kuona umuhimu wa vitu hivi
viwili katika kufanya mapendekezo na
maamuzi.
Meneja uendeshaji wa Havas Tanzania anasema
mwaka jana umekuwa ni mwaka wa kusisimua sana katika suala la maendeleo ya
ofisi yake na timu kwa ujumla inaona fursa kubwa mwaka 2017. Mbinu kubwa
wanayoitumia kwa mteja wao,ni kuwa na uelewa wa soko la Tanzania, mteja wake
anataka nini na namna pekee wanayotumia kutangaza bidhaa kupitia mtandao, na
namna wanavyoweza kujenga fikra
kimkakati kwa kuongozwa na
takwimu.
Hii ndiyo sababu inayowafanya wateja wengi
kuchagua Havas.
Kwa mawasiliano na Havas Tanzania: fey.mallonga@tanzania.havasafrica.com
Fuatilia ukurasa wetu wa FB: https://www.facebook.com/Havas-Africa-Tanzania-751467008361935/
credit -Michuzi Blog
credit -Michuzi Blog
0 comments:
Post a Comment