WABUNGE WA UKAWA WALIODAIWA KUMDHALILISHA NA KUMJERUHI KATIBU TAWALA WA DAR WASHINDA KESI NA KUACHIWA HURU
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imewaachia huru wabunge wa Ukawa na makada wa muungano huo baada ya kuona kuwa hawana kesi ya kujibu.
February 27 2016 katika ukumbi wa Karimjee Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara, Diwani wa Kata ya Kimanga, Manase Njema, mfanyabiashara na kada wa chama hicho, Rafii Juma na Diwani wa Kata ya Saranga Kimara, Ephreim Kinyafu walidaiwa kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresa Mmbando.
Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amesema katika ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibisha, hata mlalamikaji Mmbando hakumbuki ni nani aliyemjeruhi.
Aidha ameongeza ushahidi wake ulielezea Jinsi washtakiwa walivyojishughulisha na nyaraka siku ya tukio na siyo kumjeruhi, hivyo hakimu aliwaachia huru washtakiwa wote kwa kuwa hawana kesi ya kujibu.
0 comments:
Post a Comment