Sunday, 25 June 2017

WATU ZAIDI YA 100 WAPOTEA MAISHA KUFUATIA MLIPUKO WA GARI YA KUBEBA MAFUTA


Takribani watu 123 wamekufa kwa kuteketea kwa moto baada ya Lori lililokuwa limebeba mafuta kupata ajali na kulipuka nchini Pakistan.

Taarifa iliyotolewa na Serikali nchini humo imeeleza kuwa ajali hiyo imetokea katika mji wa Ahmedpur Sharqia katika jimbo la Punjap ambapo watu wengine kadhaa wameteketea vibaya, pale walipokuwa wakijaribu kuteka mafuta kutoka katika lori hilo la mafuta.

Waliojeruhiwa wanatibiwa hospitali huku kikosi cha zima moto kipo katika eneo la ajali kikikabiliana na moto huo.

Lori hilo la mafuta limedaiwa kuwa lilikuwa likiendeshwa kwa kasi hali iliyosababisha kuanguka na kisha kushika moto, huku mashuhuda wakieleza kuwa, baadhi ya watu waliofika katika eneo la ajali walikuwa wakivuta sigara, jambo ambalo linakisiwa kuwa chanzo cha moto huo.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA