HABARI MPYA

Monday, 26 August 2024

MAMBO MUHIMU KWA VIJANA WENZANGU.!

MUHIMU KWA VIJANA WENZANGU.!
Na Kdmula

Wengi itakuwa bado miaka miwili, mitatu au minne kabla ya kutimiza miaka 30. 

Natambua kuwa kuna waliokwisha fikisha na kuna uwezekano kuna walio nyuma kidogo.
Kama katika umri tulionao sasa kuna mtu anakuambia wewe bado ni mdogo/mtoto, basi huyo mtu hakupendi na anakulemaza kiakili. Kua! Acha utoto! Mambo yafuatayo kwa vigezo vya kibinadamu mwenye akili timamu, mtu mwerevu lazima uwe ushayatimiza.

1) Kuweka misingi ya kifamilia:
Katika umri huo unatakiwa uwe umeoa, umechumbia au uko katika uhusiano wenye kueleweka unaelekea kwenye kujenga familia. Kama katika umri huu bado unabadilisha wanawake na kudandia vicheche, basi sahau kuwa na familia imara. Mambo yafuatayo yatakuwa yanakunyemelea;
– Kuoa/kuolewa msichana/mvulana mdogo sana ambaye atakuona unamzeesha
– Kuoa /kuolewa chapchap bila kuwaza
-Kuokoteza magonjwa ya hatari
– Kunogewa na usela na kusahau kuoa/kuolewa
2)Kujitegemea kiuchumi:
Hapa simaanishi kufanya kazi na kupata mshahara pekee, la hasha! Hapa nalenga wale watoto wa mama ambao pamoja na kuwa wana kazi na mishahara, bado wanalalama mishahara haitoshi na kukimbilia kuomba hela nyumbani wanapoishiwa mara kwa mara. Wale ambao bado wanakaa nyumbani hii inawahusu pia. Pia wale wanaotumia 100% ya mishahara kununua vitu vinavyoisha (consumption) wakingoja wapate hela nyingi au wazazi, ndugu na jamaa wawasaidie kwenye uwekezaji. Africa tunachelewa sana kwenye hii sector.
3) Kuwa na kitega uchumi:
Kama unadhani mshahara wako wa milioni kadhaa ni mwingi sana, ngoja augue mtu wa karibu au wewe mwenyewe halafu daktari akuambie mgonjwa wako/wewe ana/unatakiwa ape/upelekwe nje ya nchi kwa matibabu zaidi wakati huna bima ya afya inayolipia hilo ndo utajijua kama mshahara wako heshima yake inaishia samaki samaki au inavuka border. Kitega uchumi si lazima uwe na mkampuni mkubwa, la hasha! Ila uwe na kitu cha kueleweka na chenye malengo ya kukua kuwa kitu cha maana. Kwa wale wagumu kuelewa, UNATAKIWA UWE NA PATO LA PEMBENI NJE YA MSHAHARA.
4) Makazi:
Uwe hata na kiwanja hapo Bunju Arif! Huezi kunywa bia kila weekend halafu wenzio wakiongelea issues za nyumba/viwanja/mashamba yao unakimbilia kubadilisha mada (Eti Huyu LVG wamuondoe kabisa anaharibu timu). Kumbe unazuga kupotezea story za viwanja/nyumba.
5)Uwe na professional qualification
: ACCA,CPA,CFA,CSIA,CPB, LAW SCHOOL ETC wale wa procurement wana ya kwao n.k. Ikifika huu umri kama CPA imekataa, tafuta hata mitihani za marketing upige, CPA sio issue zako. Lazima uwe na defined career (Kama hukubahatika kwenda kidato kingi, uwe na namna ya halali na ya kudumu ya kukupatia kipato). Umri huu kama huna utaalam katika fani yako, jiandae kuwa frustrated ofisini. Madogo wanasoma jamaa angu! Halafu wako tayari kupewa salary ndogo wapige kazi kuliko wewe.. So take care!
6) Uwe ushaamua ka hicho kitambi unakiondoa au unakilea:
Hapa sichekeshi! Kitambi kina madhara mengi. Suruali haikai vizuri, UTAPIGIWA, Kisukari, pressure n.k. Ukikinyamazia muda huu jua kitakuwa kishakomaa na majukumu yatakuwa mlima. Ukikiachia kijiamulie, kitakuganda kama “roba ya mbao” till death does you apart! Kama unakipenda endelea nacho, kama hukipendi uwe ushaweka program ya kukiondoa.
7)Uwezo wa kusaidia wanaokutegemea:
Kama we ni wa kishua, hapa hapakuhusu. Wewe ambaye si wa kishua, wazazi walikuwa na mategemeo flani walipokuwa wanakusomesha. Kama umefika miaka 30 hujaanza kuyatimiza mategemeo yao bila sababu ya msingi, jua watakuwa washakata tamaa na wewe.
8) Uwe na busara.
Kuwa mtu wa kufikiri kabla ya kutenda. Tengeneza haiba nzuri na ya kuheshimika kwa wanaokuzunguka. Kama huna busara hadi umri huu basi we sahau suala la busara ukiwa hai.. Labda utakutana nayo akhera.!
9) Savings:
Hapa nimeweka kizungu kuonyesha msisitizo. Kila mtu ana kipato chake. Ila formula ni kwamba angalau uwe ushahifadhi fedha sawa na mishahara yako ya mwaka na nusu gross of Tax kwa kipindi hicho. Kwa wale wagumu kuelewa namaanisha Ukiacha kazi au kusimamishwa kazi, uwe na uwezo wa kukaa mwaka na nusu bila kuingiza kitu chochote lakini uendelee kuishi maisha yale yale.
10) Umjue Mungu:
Nimeliweka hili mwisho si kwamba ni la mwisho kwa umuhimu, La hasha! Ni ili ulikumbuke zaidi. Mjue Mungu, mpende na umuogope. Nenda ibadani, soma neno lake na umuombe. Uwe na desturi ya kusali nyumbani kwako angalau kila unapoamka na wakati wa kulala. Kama humuogopi Mungu katika umri huu, basi wewe kwenda Mbinguni ni ngumu kuliko ngamia kupenya tundu la sindani (hata kama ni masikini).

KWA NINI WAGANGA WANAWEZA KUWASAIDIA WATU KUWA MATAJIRI WAKATI WAO NI MASIKINI?



Kuna watu ambao wanapata mafanikio makubwa kwa kutumia uchawi. Ila mafanikio yale hayaletwi na uchawi bali imani ya mtu husika.

Tutajadili kwa nini waganga wanaweza kuwapatia watu wengine dawa au mbinu za kuwa matajiri wakati wao ni masikini. Na pia tutaangalia jinsi ambavyo unaweza kutumia mbinu hizi wanazotumia waganga bila ya wewe kuwa mchawi na ukafikia mafanikio makubwa.


Kila mmoja wetu anaelewa kwamba kuna watu wanakwenda kwa waganga na wanasaidiwa kupata utajiri. Japokuwa utajiri huu haudumu, lakini angalau wanaupata kwa kiwango fulani.


 

 Wakati waganga hawa wanawasaidia watu kuweza kujenga magorofa, wao bado wanakaa kwenye vibanda vya nyasi.


Sasa kwa nini wao wasingetumia uchawi wao na kuwa matajiri zaidi ya hao wateja wao? Ina maana wao hawapendi utajiri huo?


Mbinu za waganga kuwasaidia watu kupata utajiri.

Watu wanaokwenda kwa waganga ili kupata utajiri au mafanikio yoyote hupewa masharti ambayo ni magumu kwa kiasi fulani. 


Na watu hawa huambiwa wakivunja masharti hayo tu utajiri wao unaisha mara moja. Ni masharti haya ambayo humjengea mtu nidhamu kubwa sana na kumfanya aweze kufanya kazi kwa juhudi kubwa kuliko wengine ambao wanafanya anachofanya. 


Kwa mfano mganga anamwambia mtu kila siku aamke asubuhi na mapema sana na apasue nazi barabarani ndio aende kwenye biashara zake. 


Kupasua nazi hakuna uhusiano wowote na mafanikio yake ila kuamka asubuhi na mapema kila siku ina msaada mkubwa kwenye mafanikio yake.


Hivyo mtu huyu atafuata masharti haya kila siku na hata kama kuna siku hajisikii itambidi afanye tu kwa sababu ameshaaminishwa akiacha atafilisika.


Sasa wewe ambaye huna sharti la aina hii siku ukiwa hujisikii vizuri unalala, siku nyingine unachelewa na hivyo kushindwa kufikia mafanikio makubwa. 


Masharti mengine kama kutokufanya starehe, kutokunywa pombe, kuvaa nguo moja na mengine mengi yanapelekea mtu kupunguza matumizi na kupata muda mwingi wa kufikiria kazi au biashara yake.


Masharti mengine yanayotolewa na waganga ni kumfanya mtu aweze kuondoka kwenye woga wake(comfort zone). Kila mmoja wetu kuna vitu fulani anaogopa kufanya, lakini vitu hivi ndio vinaweza kumletea mafanikio.


 Ili kukuondolea woga huu mganga anamfanya mtu afanye jambo kubwa sana ambalo litamuondolea woga kabisa.


 Kwa mfano mtu anaambiwa aue, kwa kuona kwamba ameweza kuua mtu, inamfanya mtu asizuiwe na kitu chochote.


Kikubwa ambacho mganga anamsaidia mtu ni kumjengea utaratibu ambao lazima kila siku ataufuata na pia kumjengea nidhamu binafsi na hivyo kuweza kufanya jambo hata kama hajisikii kufanya. Na hili ndio hitaji kubwa la kuweza kufikia mafanikio.


Kwa nini waganga hawawezi kutumia mbinu hii wenyewe.?

Kwa sababu wanajua inavyofanya kazi na pia hawana mtu wa kuwajengea imani hiyo kubwa kwao wenyewe.


Kwa nini watu baadaye hufilisika?

Wengi hufilisika baadae kwa sababu wanapopata mafanikio wanasahau kutumia yale masharti waliyopewa na pia imani yao inakuwa imewekwa kwenye vitu fulani(mfano hirizi) badala ya kuwa kwao wenyewe.


Ufanyeje ili uweze kutumia mbinu hii kufikia mafanikio.

Cha kwanza kabisa lazima ujijengee nidhamu binafsi. Jiwekee masharti yako ambayo utayafuata kila siku na hakikisha unayafuata.


Kwa mfano weka utaratibu kwamba kila siku utakuwa unaamka saa kumi asubuhi, kuipanga siku yako na kisha kujisomea kidogo. 


Baada ya hapo unawahi kwenye eneo lako la kazi au biashara na kuanza kazi zako mapema. Pia unaweza kujiwekea utaratibu kwamba kila mteja au mtu yeyote unayekutana naye kwenye siku husika atajisikia vizuri kukutana na wewe.


Fuata masharti haya kila siku na utaona mabadiliko makubwa kwenye maisha yako na shughuli zako.

Kwa hiyo mpaka sasa una mbinu mbili za uhakika za kufikia mafanikio;

1. Una uwezo mkubwa uko ndani yako, ila unatakiwa kuwa na imani kubwa sana kwamba unaweza kupata kile unachotaka.

2. Lazima uwe na nidhamu binafsi, uwe na masharti(rituals) na uwe na utaratibu wa kufanya kila siku (routine). Vitu hivi jiwekee mwenyewe na vifuate kila siku kwenye maisha yako.

Ukiweza kufanya mambo hayo mawili ni lazima utafikia mafanikio makubwa.

Nakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio. Kumbuka unaweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa sana bila ya kutumia uchawi au kwenda kwa mganga.Uchawi kamili upo kwenye kichwa chako. Anza kuutumia sasa.

credit- Makirita Amani-(Amka mtanzania)

Sunday, 25 August 2024

HIZI NDIO TOFAUTI SITA(6) KATI YA UBONGO WA MWANAMKE NA MWANAUME



1. Ubongo wa mwanamke unaweza kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja; mfano kuzungumza kwenye simu na kufuatilia kipindi kwenye TV Mwanaume hawezi.


2. Lugha: wanawake wanaweza kujifunza lugha nyingi kwa urahisi. Chukua mtoto wa kike
na wa kiume wenye umri wa miaka mitatu. Mara nyingi wa kike atakuwa anajua maneno mengi kuliko wa kiume.




3. Kusema uongo: mwanaume akimdanganya mwanamke uso kwa uso ni rahisi kushtukiwa. Wanawake hugundua ukweli kupitia uso wako kwa 70%, kupitia body language yako 20% na 10% kupitia maneno yako. Ubongo wa mwanaume hauna uwezo huo ndiyo maana ni rahisi mwanamke kumdanganya mwanaume uso kwa uso.



4. Uwezo wa kutatua matatizo: mwanaume akiwa na matatizo, ubongo wake huyachukua na kuyatenga katika makundi mbalimbalina kisha huanza kutafuta suluhisho moja baada ya
jingine. Mwanamke akiwa na matatizo ubongo wake hauwezi kuyatenga na badala yake hutaka mtu amsikilize. Baada ya kumwambia mtu matatizo yake yote akili yake hupata kiwango fulani cha utulivu na huwa mara nyingi hajali kama yatatuliwa au la.


5. Mahitaji: Wanaume wanahitaji heshima kwenye jamii, mafanikio, sifa, nk.; wanawake wanapenda mahusiano, familia, marafiki, etc.



6. Kuongea: mwanamke mara nyingi hutumia lugha ya kificho. Mwanaume hutumia lugha ya moja kwa moja.

Tuesday, 13 August 2024

KAMA KWELI UNAHITAJI MWENZI WA MAISHA: HII INAKUHUSU



 
Ni njia gani za kumpata mwenzi wa maisha yako? Inawezekana unakabili mtihani mzito, hujui ni yupi wa nafsi yako. Bila shaka unamtaka yule wako wa kufa na kuzikana.

Mada hii inakuja na suluhisho mahsusi kwako, kumjua mapema anayekufaa, anayeweza kudumu nawe maishani. Zingatia kwamba mwenzi sahihi wa maisha yako ni hatua muhimu kuelekea kwenye mafanikio.

KWANZA TAMBUA HILI

Uhusiano wa kimapenzi ni suala binafsi. Kwanza kabisa ni sanaa inayokutaka uangalie mahitaji yako mwenyewe. Je, unahitaji nini kwa mtu ambaye ungependa awe mwenzi wa maisha yako?

Yale unayotaka kutoka kwa mtu ambaye unapenda awe mwenzi wa maisha yako, unapaswa kuyapa kipaumbele. Hata siku moja, usithubutu matamanio ya mwili na moyo yakupe mwongozo wa kumwona umpendaye.

NANI MWENZI WA MAISHA?

Ni swali ambalo unapaswa kujiuliza. Kwa uwazi kabisa, unatakiwa kuzingatia kuwa mwenzi wa maisha ni yule ambaye utachangia naye mambo mengi kwa uaminifu na maelewano makubwa.

Mwenzi wa maisha si mtu unayeweza kuwa naye kwa mantiki ya kupeana tulizo la ngono unapohitaji au kampani ya kwenda kuangalia ‘muvi’, muziki, ufukweni na kwingineko unapoona huhitaji kuwa peke yako.

Mwenzi wa maisha ni yule atakayefanya ujione umekamilika, bila kujali ‘ubize’ wala ukapa ambao pengine unao ndani ya jamii inayokuzunguka. 

Kingine cha kuzingatia ni kwamba, mwenzi wa maisha yako ni yule ambaye anakukubali na kukupenda kama ulivyo, bila kuwepo kwa nyongeza ambazo zitatokana na kukubadilisha kutoka yule wa zamani.

Kupata mwenzi wa maisha mwenye sifa kamili, ni sawa na kupatia herufi ya mwisho kwenye mchezo wa kubahatisha. Kwa maana hiyo, baada ya kumpata, kila kitu kinakuwa kimekamilika maishani mwako.

NANI MWENZI WA MAISHA YAKO?

Pointi ya msingi kuzingatia ni kwamba unahitaji kuwa na yule anayekubalika ndani ya nafsi yako. Hivyo basi, fikiria kwa yale yanayoweza kukufanya uwe na furaha, pia yanayoweza kukupa huzuni.

Zingatia mapitio yako ya nyuma kuona ni kwa namna gani yamekutengeneza mpaka kufika ulivyo sasa. Jiulize pia kuhusu ndoto na malengo yako siku za usoni.

Ikiwa tu utaweza kutambua mahitaji na matarajio yako ya kimaisha, bila shaka utaweza kutambua ni mtu gani anayefaa katika kukusaidia kutimiza kila kilichomo ndani ya malengo yako.

JENGA IMANI

Kutafuta mwenzi wa maisha siyo suala la kuangalia mtu wa kwenda naye klabu kujirusha usiku. Vile vile ni muhimu kutambua kwamba inaweza kukuchukua muda kupata mtu wa kukidhi vigezo vyako.


Pamoja na ukweli huo, bado unatakiwa uwe na imani kwamba itafika wakati utasahau habari za kutafuta mwenzi na utakuwa mwenye furaha, ukijipongeza kwa kumpata anayekufaa.

Mapenzi ni mchezo lakini ni rahisi kuucheza ukitambua kanuni zake. Hii ina maana kuwa unapokuwa kwenye kipengele hiki, unakuwa na jukumu moja zito la kuhakikisha unampata yule mwenye uwezo wa kukonga moyo. Mwenye sura ya kutimiza malengo yako.

Hata hivyo, muhimu kwako ni kuwa mtulivu na kuacha macho yafanye kazi ya kuangaza kwa utaratibu, halafu akili ifanye kazi ya kutathmini kiwango cha huyo atakayeonwa.

Kitu kingine ambacho unatakiwa kuheshimu ni kuwa, wawili wanaopendana, kila mmoja kwa nafasi yake ni nusu ya kitu kizima kinachoitwa ndoa au wapenzi, hivyo wanapounganishwa ndiyo kinapatikana kitu kizima.

Ukiamini kuwa wewe ni nusu na utakamilika baada ya kukutana na mwenzi wako, unachotakiwa kufanya ni kujenga imani kwamba mwenzi wako yupo sehemu kwa ajili yako, hivyo endelea kumtafuta na siku moja utamuweka mikononi mwako. 

NJIA 4 ZA KUZUIA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO




Migogoro katika mahusiano ya mapenzi ni kitu cha kawaida kutokea. Wenza katika mahusiano hugombana na ugomvi mwingine hupelekea hadi kupigana na kusababishiana maumivu hata kuumizana.
Lakini migogoro mingi inaweza kuepukika kama tu wenza hao wakitambua vitu vinavyosababisha kugombana kwao na kuweka mikakati itakayowasaidia kuishi kwa amani zaidi na kuifuata.
Mara nyingi katika mahusiano ugomvi hausababishwi na ujumbe au mawazo tofauti yanayotolewa na mmoja wao bali namna ujumbe huo unavyotolewa na jinsi mpokeaji anavyotafsiri.
Hii inamaana kuwa kama wenza hao wakikubaliana na wakawasiliana hoja zao katika namna ambavyo kila mmoja wao anahisi kusikilizwa na kujaliwa namba za magomvi zitapungua sana.
Hebu tuone namna ambavyo migogoro katika mahusiano inaweza kupunguzwa na kusuluhishwa:

Mbinu # 1: Acha Kujihami



Mapambano kati ya wenza wawili yanaweza kufananishwa na mpambano wa mchezo wa ngumi. Bondia mmoja anapotupa makonde mfululizo na mwingine anajaribu kuzuia ni kawaida atakuwa narudi nyuma na kuruhusu mwenzake aendelee kumvamia.
Vivyo hivyo katika ugomvi katika mahusiano ya wapenzi. Mwenza mmoja napomvamia mwenzake kwa maneno makali na tuhuma kwa mfano, na mwingine akawa anajihami nayo kwa kupinga au kwa kurudisha tuhuma,kinachotokea ni kuwa mapambano yataendelea.
Kama unatengeneza mazingira ya kujihami na mpenzi wako basi unafanya aendelee kukushambulia na hivyo kuendeleza mgogoro kwa muda mrefu.
Zuia kujihami na toka katika uringo wa mapambano. Kumbuka bondia hawezi kupigana na upepo,kama hakuna mpinzani basi hakuna pambano.
Epuka majibizano ya maneno ambayo yatapelekea ugomvi. Kuwa wa kwanza kukaa kimya,ikiwezekana kuondoka kwa muda huo na muendelee mazungumzo baadae wakati kuna utulivu na kusikilizana.

Mbinu # 2: Toa Nafasi Ya Kusikiliza


Kuna haja kubwa kwa binadamu yeyote kupenda kusikilizwa na kueleweka.
Mpenzi wako anapokuwa amekasirika au amepandwa na jazba au ameumizwa kihisia anapenda kusikilizwa shida yake na apate kueleweka.
Unahitaji kutoa nafasi ya kusikiliza na kuelewa nini anafikiri au kuhisi moyoni. Jaribu kurudia kile alichosema kumhakikishia kuwa umemsikia vizuri. Pia inaonyesha kuwa unajali. Mpenzi yeyote anapenda kuona kuwa mawazo yake na yeye mwenyewe yanajaliwa.
Unaporudia kutamka alichosema kuna maana mbili, ya kwanza ni kuwa umemsikia vizuri lakini pili ni kuwa inaonyesha kuwa unajali.
Mfano: “Najua jambo hili ni muhimu kwako,lakini nafikiri tungeangalia mambo yanayohusu watoto na mahitaji yao kwanza na hilo lifanyike baadae”
Jaribu mbinu hii kwa mwenza wako mnapokuwa na migogoro na uone jinsi inavyofanya maajabu.
Kumbuka sauti inayotumika iwe yenye kuonyesha kujali na sio kuongea kama vile ni polisi.

Mbinu # 3: Chukua Wajibu




Tatizo linapotokea na likazusha mgogoro ni jambo la busara kwa mmoja wenu kukubali kuwajibika katika suala hilo na sio kurushiana lawama kila mmoja akimlaumu mwenzake kuwa amekosea.
Kama mmoja wao akikubali kuwa ni kosa lake,hakutakuwa na ugomvi tena. Wengine hukubali kosa hata kama si lao ilimradi tu kuwe na amani. Utasikia mtu akisema “Nakubali yaishe..”
Mfano:

I. Mapambano
Mke: “Tumelala bila kufunga milango leo,kwanini hukuangalia milango kabla hatujalala?”
Mme: ”Hilo ni tatizo lako,kwanini wewe ndio ulikuwa wa mwisho kuingia”

II. Kuwajibika
Mke: “Tumelala bila kufunga milango leo,kwanini hukuangalia milango kabla hatujalala?”
Mme: ”Ahh.. Samahani! Ni kweli kama baba wa nyumba ni jukumu langu kuhakikisha usalama wa nyumba. Nitakuwa makini zaidi,ni kosa langu”

Katika mfano wa kwanza ni lazima mabishano yataendelea,na usishangae yakaishia hata kupigana. Lakini katika mfano wa pili,mgogoro umeisha,sana sana watacheka na kukumbatiana.

Mbinu # 4: Kusimama Pamoja



Mapambano mengi baina ya wapenzi husababishwa na kuvunjika kwa mawasiliano. Kunasababishwa na kutoelewa madhumuni ya mwenza wake.
Kutoelewana ni adui ambaye anaweza kuwasambaratisha wapenzi,na wakaharibu mahusiano yao.
Ni muhimu sasa kwa wapenzi kwa pamoja kushambulia KUTOELEWANA.
Kutoelewana kunapotokea ni muhimu kupeana nafasi ya kufafanua maana ya maneno yake ya awali au matendo yake.
kwa namna hii utaweza kufahamu madhumuni yake.
Kufaninisha hili ni lazima kuwa msikivu(Mbinu #2) vinginevyo utakosa kusikia ufafanuzi wake.
Ni muhimu kutumia neno “SISI” na siyo “MIMI” katika kufafanua mazungumzo yenu.
Mfano:
Mme:”Ni kweli tumelala bila kufunga milango,ila wote tulikuwa tumechoka sana na kazi za siku nzima,tuwe waangalifu zaidi siku zijazo”

Fanyia Kazi..:

Hebu tumia mbinu hizi nne rahisi kabisa katika kutatua migogoro katika mahusiano yako, ni hakika kuwa utafanikiwa sana na kuleta amani na maelewano na mweza wako.
Kumbuka hakuna mshindi katika mabishano yanayotokea katika mahusiano yako,wote mnapoteza. Mkilitamba hili kwapamoja mtasimama pamoja na mtaangalia mbinu sahihi ambazo zimetajwa katika makala hii kuwasaidia kuondokana na migogoro katika mahusiaono yenu.
Je huwa unagombana na mpenzi wako mara kwa mara? Najua jibu lako ni ndiyo. Basi jaribu mbinu hizi nne zilitotajwa na uone matokeo yake.
Kama una maoni juu ya mada hii, tuandikie mawazo yako katika kisanduku cha maoni hapa chini . Pia tutumie mbinu nyingine ambazo unazitumia na zinafanya kazi ili tufaidike.
-KD


OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA