Showing posts with label elimu. Show all posts
Showing posts with label elimu. Show all posts

Monday, 7 September 2026

KWA NINI WAGANGA WANAWEZA KUWASAIDIA WATU KUWA MATAJIRI WAKATI WAO NI MASIKINI?



Kuna watu ambao wanapata mafanikio makubwa kwa kutumia uchawi. Ila mafanikio yale hayaletwi na uchawi bali imani ya mtu husika.

Tutajadili kwa nini waganga wanaweza kuwapatia watu wengine dawa au mbinu za kuwa matajiri wakati wao ni masikini. Na pia tutaangalia jinsi ambavyo unaweza kutumia mbinu hizi wanazotumia waganga bila ya wewe kuwa mchawi na ukafikia mafanikio makubwa.


Kila mmoja wetu anaelewa kwamba kuna watu wanakwenda kwa waganga na wanasaidiwa kupata utajiri. Japokuwa utajiri huu haudumu, lakini angalau wanaupata kwa kiwango fulani.


 

 Wakati waganga hawa wanawasaidia watu kuweza kujenga magorofa, wao bado wanakaa kwenye vibanda vya nyasi.


Sasa kwa nini wao wasingetumia uchawi wao na kuwa matajiri zaidi ya hao wateja wao? Ina maana wao hawapendi utajiri huo?


Mbinu za waganga kuwasaidia watu kupata utajiri.

Watu wanaokwenda kwa waganga ili kupata utajiri au mafanikio yoyote hupewa masharti ambayo ni magumu kwa kiasi fulani. 


Na watu hawa huambiwa wakivunja masharti hayo tu utajiri wao unaisha mara moja. Ni masharti haya ambayo humjengea mtu nidhamu kubwa sana na kumfanya aweze kufanya kazi kwa juhudi kubwa kuliko wengine ambao wanafanya anachofanya. 


Kwa mfano mganga anamwambia mtu kila siku aamke asubuhi na mapema sana na apasue nazi barabarani ndio aende kwenye biashara zake. 


Kupasua nazi hakuna uhusiano wowote na mafanikio yake ila kuamka asubuhi na mapema kila siku ina msaada mkubwa kwenye mafanikio yake.


Hivyo mtu huyu atafuata masharti haya kila siku na hata kama kuna siku hajisikii itambidi afanye tu kwa sababu ameshaaminishwa akiacha atafilisika.


Sasa wewe ambaye huna sharti la aina hii siku ukiwa hujisikii vizuri unalala, siku nyingine unachelewa na hivyo kushindwa kufikia mafanikio makubwa. 


Masharti mengine kama kutokufanya starehe, kutokunywa pombe, kuvaa nguo moja na mengine mengi yanapelekea mtu kupunguza matumizi na kupata muda mwingi wa kufikiria kazi au biashara yake.


Masharti mengine yanayotolewa na waganga ni kumfanya mtu aweze kuondoka kwenye woga wake(comfort zone). Kila mmoja wetu kuna vitu fulani anaogopa kufanya, lakini vitu hivi ndio vinaweza kumletea mafanikio.


 Ili kukuondolea woga huu mganga anamfanya mtu afanye jambo kubwa sana ambalo litamuondolea woga kabisa.


 Kwa mfano mtu anaambiwa aue, kwa kuona kwamba ameweza kuua mtu, inamfanya mtu asizuiwe na kitu chochote.


Kikubwa ambacho mganga anamsaidia mtu ni kumjengea utaratibu ambao lazima kila siku ataufuata na pia kumjengea nidhamu binafsi na hivyo kuweza kufanya jambo hata kama hajisikii kufanya. Na hili ndio hitaji kubwa la kuweza kufikia mafanikio.


Kwa nini waganga hawawezi kutumia mbinu hii wenyewe.?

Kwa sababu wanajua inavyofanya kazi na pia hawana mtu wa kuwajengea imani hiyo kubwa kwao wenyewe.


Kwa nini watu baadaye hufilisika?

Wengi hufilisika baadae kwa sababu wanapopata mafanikio wanasahau kutumia yale masharti waliyopewa na pia imani yao inakuwa imewekwa kwenye vitu fulani(mfano hirizi) badala ya kuwa kwao wenyewe.


Ufanyeje ili uweze kutumia mbinu hii kufikia mafanikio.

Cha kwanza kabisa lazima ujijengee nidhamu binafsi. Jiwekee masharti yako ambayo utayafuata kila siku na hakikisha unayafuata.


Kwa mfano weka utaratibu kwamba kila siku utakuwa unaamka saa kumi asubuhi, kuipanga siku yako na kisha kujisomea kidogo. 


Baada ya hapo unawahi kwenye eneo lako la kazi au biashara na kuanza kazi zako mapema. Pia unaweza kujiwekea utaratibu kwamba kila mteja au mtu yeyote unayekutana naye kwenye siku husika atajisikia vizuri kukutana na wewe.


Fuata masharti haya kila siku na utaona mabadiliko makubwa kwenye maisha yako na shughuli zako.

Kwa hiyo mpaka sasa una mbinu mbili za uhakika za kufikia mafanikio;

1. Una uwezo mkubwa uko ndani yako, ila unatakiwa kuwa na imani kubwa sana kwamba unaweza kupata kile unachotaka.

2. Lazima uwe na nidhamu binafsi, uwe na masharti(rituals) na uwe na utaratibu wa kufanya kila siku (routine). Vitu hivi jiwekee mwenyewe na vifuate kila siku kwenye maisha yako.

Ukiweza kufanya mambo hayo mawili ni lazima utafikia mafanikio makubwa.

Nakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio. Kumbuka unaweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa sana bila ya kutumia uchawi au kwenda kwa mganga.Uchawi kamili upo kwenye kichwa chako. Anza kuutumia sasa.

credit- Makirita Amani-(Amka mtanzania)

Thursday, 3 September 2026

UKIZITUMIA KAULI HIZI KUMFARIJI MTU ZITAZIDISHA HUZUNI KWA MUHUSIKA


Haya ni makosa ambayo tunayafanya bila kujua, kwasababu katika muda huo, tunakuwa hatuna njia ya kumfanya aliyeondokewa na mali au mtu ajisikie tuko pamoja naye katika machungu.

Na kwakuwa ni vigumu kwa muhusika kukueleza kwamba nataka kufanyiwa au kuambiwa kitu fulani ndio nitajisikia vizuri, inakubidi utumie ujuzi wako binafsi kutafuta njia ya kumfanya ajisikie vizuri.

Hapo sasa balaa ndio linaanza,kwani mara nyingi maneno tunayochagua kumwambia aliyepotelewa hayamfanyi ajisikie poa bali yanamfanya aanze kutafakari ulikuwa na maana gani.

Na hii inatokana na si wote wana uwezo wa kutafakari kauli zinazotolewa na watu wengine katika mtazamo chanya.

Hebu tuangalie maneno ambayo hupaswi kuyasema  kwa muhusika:

1."Shukuru (ameishi/umeishi nacho) miaka mingi"

Unapoongea kauli kama hii inampa picha mtu huyo, kwamba jambo hilo lilipaswa kutokea kwake,na hivyo hapaswi kuhuzunika.Yawezekana kuna ukweli ndani yake, lakini unapoongea mbele ya muhusika haitamfanya ajisikie vizuri.

2."Muda wake ulifika"

Hata kama umekosa la kuongea hii kauli sio kabisa,itamfanya akuone umefurahia tukio hilo.

3."Alikosea/Ulikosea sana ku.... "

Ikiwa tukio lilikuwa la ajali, hata kama liliempata alisababisha usiongee kauli kama hii kwa muhusika,itaonekana kana kwamba alifanya uzembe na alistahili kupatwa na hilo.

4."Kuna sababu ya kila kitu"

Hii  kauli kweli ina maana, unapofikiria kwa kina lakini si nzuri kuizungumza kwa mtu aliye kwenye majonzi.

5."Usihofu utampata mwengine tu"

Ikiwa mtu amepoteza mtoto, mume au mke, kauli ya kumwambia kwamba asihuzunike na kuwa atapata mwengine tu,itamfanya aone hukuwahi kuona umuhimu wa aliyeondokewa naye,na ulikuwa unaombea hilo litokee.

Mara nyingi maneno haya yanapotamkwa na muhusika yanakuwa na matumaini zaidi kuliko yanapotamkwa na mtu mwengine wa pembeni. 

Ni heri utumie maneno kama:

1."Pole sana kwa yaliyotokea" 

2."Natamani ningekuwa na maneno mazuri ya kukueleza ujisikie vizuri"

3."Niko pamoja nawe katika hili"

4."Niko pamoja nawe katika sala"

5."Tulimpenda wote"

6."Ukihitaji msaada, niko hapa kwa ajili yako"

TABIA YA KUWAFARIJI WENZETU WANAPOPATWA  NA MATATIZO, NI NZURI SANA NA ITAWAFANYA  WAJISIKIE VIZURI.

KWELI YAWEZEKANA UNA TAFSIRI YAKO MOYONI JUU YA TUKIO LILILOTOKEA,  LAKINI IWEKE MOYONI UKIONA HAITAMFARIJI MUHUSIKA.

WOTE TUNAWEZA KUWA TUMAINI KWA WENGINE PALE WANAPOPATWA NA  MATATIZO 
KWA KUTUMIA MANENO NA NJIA SAHIHI 


KUELEZEA HISIA ZETU PIA.

Wednesday, 2 September 2026

MAMBO MUHIMU KWA VIJANA WENZANGU.!

MUHIMU KWA VIJANA WENZANGU.!
Na Kdmula

Wengi itakuwa bado miaka miwili, mitatu au minne kabla ya kutimiza miaka 30. 

Natambua kuwa kuna waliokwisha fikisha na kuna uwezekano kuna walio nyuma kidogo.
Kama katika umri tulionao sasa kuna mtu anakuambia wewe bado ni mdogo/mtoto, basi huyo mtu hakupendi na anakulemaza kiakili. Kua! Acha utoto! Mambo yafuatayo kwa vigezo vya kibinadamu mwenye akili timamu, mtu mwerevu lazima uwe ushayatimiza.

1) Kuweka misingi ya kifamilia:
Katika umri huo unatakiwa uwe umeoa, umechumbia au uko katika uhusiano wenye kueleweka unaelekea kwenye kujenga familia. Kama katika umri huu bado unabadilisha wanawake na kudandia vicheche, basi sahau kuwa na familia imara. Mambo yafuatayo yatakuwa yanakunyemelea;
– Kuoa/kuolewa msichana/mvulana mdogo sana ambaye atakuona unamzeesha
– Kuoa /kuolewa chapchap bila kuwaza
-Kuokoteza magonjwa ya hatari
– Kunogewa na usela na kusahau kuoa/kuolewa
2)Kujitegemea kiuchumi:
Hapa simaanishi kufanya kazi na kupata mshahara pekee, la hasha! Hapa nalenga wale watoto wa mama ambao pamoja na kuwa wana kazi na mishahara, bado wanalalama mishahara haitoshi na kukimbilia kuomba hela nyumbani wanapoishiwa mara kwa mara. Wale ambao bado wanakaa nyumbani hii inawahusu pia. Pia wale wanaotumia 100% ya mishahara kununua vitu vinavyoisha (consumption) wakingoja wapate hela nyingi au wazazi, ndugu na jamaa wawasaidie kwenye uwekezaji. Africa tunachelewa sana kwenye hii sector.
3) Kuwa na kitega uchumi:
Kama unadhani mshahara wako wa milioni kadhaa ni mwingi sana, ngoja augue mtu wa karibu au wewe mwenyewe halafu daktari akuambie mgonjwa wako/wewe ana/unatakiwa ape/upelekwe nje ya nchi kwa matibabu zaidi wakati huna bima ya afya inayolipia hilo ndo utajijua kama mshahara wako heshima yake inaishia samaki samaki au inavuka border. Kitega uchumi si lazima uwe na mkampuni mkubwa, la hasha! Ila uwe na kitu cha kueleweka na chenye malengo ya kukua kuwa kitu cha maana. Kwa wale wagumu kuelewa, UNATAKIWA UWE NA PATO LA PEMBENI NJE YA MSHAHARA.
4) Makazi:
Uwe hata na kiwanja hapo Bunju Arif! Huezi kunywa bia kila weekend halafu wenzio wakiongelea issues za nyumba/viwanja/mashamba yao unakimbilia kubadilisha mada (Eti Huyu LVG wamuondoe kabisa anaharibu timu). Kumbe unazuga kupotezea story za viwanja/nyumba.
5)Uwe na professional qualification
: ACCA,CPA,CFA,CSIA,CPB, LAW SCHOOL ETC wale wa procurement wana ya kwao n.k. Ikifika huu umri kama CPA imekataa, tafuta hata mitihani za marketing upige, CPA sio issue zako. Lazima uwe na defined career (Kama hukubahatika kwenda kidato kingi, uwe na namna ya halali na ya kudumu ya kukupatia kipato). Umri huu kama huna utaalam katika fani yako, jiandae kuwa frustrated ofisini. Madogo wanasoma jamaa angu! Halafu wako tayari kupewa salary ndogo wapige kazi kuliko wewe.. So take care!
6) Uwe ushaamua ka hicho kitambi unakiondoa au unakilea:
Hapa sichekeshi! Kitambi kina madhara mengi. Suruali haikai vizuri, UTAPIGIWA, Kisukari, pressure n.k. Ukikinyamazia muda huu jua kitakuwa kishakomaa na majukumu yatakuwa mlima. Ukikiachia kijiamulie, kitakuganda kama “roba ya mbao” till death does you apart! Kama unakipenda endelea nacho, kama hukipendi uwe ushaweka program ya kukiondoa.
7)Uwezo wa kusaidia wanaokutegemea:
Kama we ni wa kishua, hapa hapakuhusu. Wewe ambaye si wa kishua, wazazi walikuwa na mategemeo flani walipokuwa wanakusomesha. Kama umefika miaka 30 hujaanza kuyatimiza mategemeo yao bila sababu ya msingi, jua watakuwa washakata tamaa na wewe.
8) Uwe na busara.
Kuwa mtu wa kufikiri kabla ya kutenda. Tengeneza haiba nzuri na ya kuheshimika kwa wanaokuzunguka. Kama huna busara hadi umri huu basi we sahau suala la busara ukiwa hai.. Labda utakutana nayo akhera.!
9) Savings:
Hapa nimeweka kizungu kuonyesha msisitizo. Kila mtu ana kipato chake. Ila formula ni kwamba angalau uwe ushahifadhi fedha sawa na mishahara yako ya mwaka na nusu gross of Tax kwa kipindi hicho. Kwa wale wagumu kuelewa namaanisha Ukiacha kazi au kusimamishwa kazi, uwe na uwezo wa kukaa mwaka na nusu bila kuingiza kitu chochote lakini uendelee kuishi maisha yale yale.
10) Umjue Mungu:
Nimeliweka hili mwisho si kwamba ni la mwisho kwa umuhimu, La hasha! Ni ili ulikumbuke zaidi. Mjue Mungu, mpende na umuogope. Nenda ibadani, soma neno lake na umuombe. Uwe na desturi ya kusali nyumbani kwako angalau kila unapoamka na wakati wa kulala. Kama humuogopi Mungu katika umri huu, basi wewe kwenda Mbinguni ni ngumu kuliko ngamia kupenya tundu la sindani (hata kama ni masikini).

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA