Tuesday 18 March 2014

HOSPITALI MWANANYAMALA "HATARI SANA!"



Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam imebainika kuwa na uzembe uliopitiliza, hali inayowafanya wagonjwa kuendelea kuilalamikia kila kukicha, mlolongo wote huu hapa.

OFM wakiwa na mgonjwa wao mapokezi hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam wakakuta patupu.
Uzembe huo umebainika baada ya makachero wa Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wanaopata huduma duni katika hospitali hiyo huku wakilalamikia uzembe wa matabibu na rushwa kwa baadhi ya wahudumu.

Mtoa habari wetu alieleza kinagaubaga akidai kuwa mambo hayo husababisha wagonjwa kupoteza maisha kwa sababu ya kutopata huduma kwa wakati unaostahili au kwa kukosa fedha ya kutoa rushwa.
OFM wakimpeleka mgonjwa wao mapokezi hospitali ya Mwananyamala.
Jamani OFM tusaidieni, hapa Hospitali ya Mwananyamala kuna matatizo sana. Unaweza kuja na mgonjwa wako lakini akakaa mapokezi hata nusu saa kabla ya kupata matibabu, halafu baadhi ya wahudumu wanapokea sana ‘kitu kidogo’.

“Hali hii inasababisha wagonjwa kufariki dunia na ndiyo maana mara nyingi utasikia mgonjwa alikufa kwa sababu ya kuchelewa kuhudumiwa kwa uzembe wa wauguzi,” alisema mwananchi huyo.

HABARI ZAIDI ZAMA NDANI YA BONGO

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA