Friday 11 March 2016

EBOUE AJITIA KITANZI SUNDERLAND

Emmanuel-Eboue
Emmanuel-Eboue
Emmanuel Eboue akipozi na jezi ya  Sunderland.
BEKI wa zamani wa Klabu ya Arsenal, Emmanuel Eboue, amejiunga na timu ya Sunderland inayoshiriki Ligi Kuu ya England (EPL).
Eboue, mwenye umri wa miaka 32, alikuwa mchezaji huru baada ya kuondoka Galatasaray ya Uturuki mwanzoni mwa msimu huu.
eboue
Akiwa na Galatasaray kuanzia 2011, Eboue alifanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi hiyo mara tatu pamoja na makombe mengine matano.
eboue
Eboue aliichezea Arsenal kwa misimu minane baada ya kutua hapo mwaka 2004 kutoka klabu ya Ubelgiji ya Beveren na kisha kuhamia Galatasaray mwaka 2011.
Sunderland imempa mchezaji huyo mkataba wa muda mfupi ambao utamalizika mwishoni mwa msimu.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA