Tuesday 25 March 2014

KABLA HUJAFA HAUJAUMBIKA SOMA HABARI HII YA HUZUNI LIVE!!




HAKIKA Mungu ni wa ajabu sana. Licha ya kwamba Domic Mage alizaliwa akiwa mlemavu, hali iliyomfanya ashindwe kujimudu kimaisha na hivyo kuishia kuwa omba omba, bado aligongwa na gari, lililomburuza urefu wa mita 40 na kumzidishia maumivu makali zaidi ya mwili.

Domic Mage akiwa anatafakali jambo.

Kwa zaidi ya miaka 10, Domic, mkazi wa kijiji cha Mvuti wilayani Temeke amekuwa barabarani akiomba, licha ya umri wake mkubwa wa miaka 58, kwani asipofanya hivyo, familia yake, ya mke na wajukuu wawili, haiwezi kujikimu kimaisha.


...Hili ni jeraha bada ya kupata ajali.
“Kazi hii ya kuomba barabarani ni ngumu sana, nimeifanya kwa kipindi hicho chote lakini cha kushangaza nimebaki na ulemavu ambayo sikuzaliwa nao, kwani wakati navuka barabara maeneo ya Ubungo Oktoba 25 mwaka juzi niligongwa na gari, likaniburuza umbali wa mita 40, nilijua ndiyo mwisho wa maisha yangu.” 

Akisimulia jinsi alivyopata ajali ile, alisema alikuwa anavuka sehemu ya wapita kwa miguu maarufu kama Zebra, likatokea gari likija kwa kasi na kumvaa, likimburuza umbali huo na kusababisha kuvunjika kwa mguu wake uliokuwa mzima na hivyo kupata ulemavu kwa mara ya pili.
“Nilichukuliwa hadi kituo cha polisi Ubungo Stendi kisha Hospitali ya Mwananyamala, nililazwa kwa muda wa miezi mitatu halafu nikapelekwa Muhimbili kwa miezi miwili, nikawa sina chakula, naletewa na majirani ninaoishi nao huko Mvuti, ninawashukuru sana, hata ombaomba wenzangu walionyesha moyo wa kunisaidia na kunifariji. 

“Niliporuhusiwa, polisi waliniambia niende mahakamani niendeshe kesi, lakini nilishindwa maana sikuwa na nauli ya kunitoa Mvuti hadi mahakama ya Kinondoni, niliwambia kama hamna jinsi ya kunisaidia, bora waniache Mungu atanilipa.


Mr. Championi akimkabidhi zawadi ya gazeti la Uwazi Domic Mage.
“Mbali na ajali hiyo pia nimekoswakoswa na magari mara nyingi, nahisi kifo changu kitatokana na ajali, nimekuwa nikinyeshewa mvua, napigwa jua ,vumbi za barabarani na kung’atwa na mbu na adha zingine, lakini navumilia kwa sababu ya shida. 

“Nilifika hapa jijini mwaka 2000 nikitokea kijiji cha Kipondodo mkoani Singida nikiwa na mke wangu na wajukuu zangu wawili ambao kijana wangu wa kiume aliniacha nao kijijn, hadi naondoka nao baba yao ambaye alikuwa mpiga debe sijui aliko. 

“Wajukuu zangu hao mama yao naye alitoweka na hajulikani aliko, nikashindwa kuwaacha wajukuu zangu, mimi nilibahatika kuwazaa watoto wawili mapacha wa kike na wa kiume, wa kike pamoja na kuolewa lakini maisha yao ni duni,
kwa kweli nilikosa usaidizi ndiyo maana niliamua kuja mjini ili serikali inisaidie, lakini ikawa tofauti, nilipata shida sana nikaamua bora niwe omba omba. 

“Nimekua nikitoka Mvuti asubuhi sana kutokana na tatizo la usafiri na kufika kituo cha daladala Mbagala yaendaayo Tandika, huko ndiko ninakofanyia shughuli zangu za kuomba, usafiri umekua mgumu sana hasa kipindi hiki cha mvua. 

“Ninishuka kituoni nabebwa na toroli hadi kituo cha magari yaendayo Tandika, natumia shilingi 2000 nauli ya kuja na kurudi kila siku, nachoka sana, lakini sina jinsi kwa vile hata mke wangu hana kazi, ni mzee na amekua akijishughulisha na kilimo cha mkono ambacho hakina tija. 

“Kwa ujumla mimi ndiyo tegemeo pale nyumbani ila kwa sasa nimechoka sana, nashindwa kuacha kwa sababu wale wajukuu zangu bado ni wadogo.
“Nawaombeni watanzania mnisaidie baiskeli ya miguu mitatu niondokane na magonjwa yanayonipata kwa kujiburuza chini, pia ningepata mtaji wa kuanzisha biashara ya mayai au kuwafuga kuku wa mayai ningeachana na kazi hii. 

“Kwa sasa nakabiliwa na kodi ya nyumba, nadaiwa shilingi laki moja na shilingi elfu arobaini (140,000) kwa nusu mwaka, niliyolipia imeisha mwezi uliopita, nimeshindwa pa kupata fedha kwani kwa sasa hata kazi ya kuombaomba si nzuri kutokana na mvua, wakati mwingine  nashindwa kuja hivyo kutufanya tushinde njaa au kushindia uji.”
Yeyote aliyeguswa na kilio cha mzee huyu anaweza kwenda kituo cha daladala Mbagala Rangi Tatu mabasi yaendayo Tandika, au kwa kumtumia kupitia simu yake ya mkononi yenye namba 0655 339616.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA