MALENGO NI NINI?... SOMA UJUE WAPI ULIPO NA NINI UFANYE KUFIKA UTAKAPO
Malengo ni nini
Malengo ni mafuta katika tanuru la mafanikio. Kama ilivyo katika tanuru la matofali, kuni zinavyokuwa na uwezo wa kuwaka vizuri ndivyo katika tanuru la mafanikio, kadri malengo yanavyokuwa makubwa ndivyo bidii ya kutafuta mafanikio inavyoongezeka.. Malengo humsukuma mtu kufanya kazi kwa lengo la kufikia malengo waliyojiwekea.
Kila mtu mwenye mafanikio anaishi kwa malengo, kwani hata kama una pesa nyingi, bila kuwa na malengo hazitakusaidia chochote cha maana kwa mfano, kuna kipindi flani nikiwa chuo nilikuwa sina pesa kabisa hadi natamani nipate sh. 2000 ya kula, cha ajabu nilikwenda benki ili niangalie kama nilibakiza walau sh. 10,000 ili nisogeze siku ndipo nilikuta nimeingiziwa sh. 320,000 toka sehemu fulani, huwezi amini sikujiachia katika burudani wala sikuzifanyia chochote cha msingi na kwa wiki 3 nilikuwa nimebaki na sh. 40,000 tu na hapo ndipo nilianza kufikiri na kupiga hesabu na kugundua kuwa, Hiyo pesa niliipata bila kuiwekea malengo kwani sikutegemea kuipata. Panga malengo hata kama hujapata pesa, jitathmini kitu gani unahitaji kununua iwapo utapata kiasi fulani cha pesa.
Hii itakusaidia katika kupangilia maisha yako kwa kujua kipi kianze na kipi kifuate na kwa muda gani. Wanaoishi kwa malengo wanajua wanachokitaka na wanakomaa nacho bila kujali vikwazo na magumu yote kwani hata katika safari hapakosi kona pamoja na milima na mabonde, kama umelenga kufika utafika tu. Uwezo wako wa kupanga malengo ndio hatua ya kwanza katika mafanikio yako. Ukiamka asubuhi jiulize, nini kifanyike kwa siku hiyo. Mwanafunzi, unapokuwa unasoma jiulize, kwanini unasoma? Ukimaliza masomo itakuwaje, utataka nini maishani mwako.
Kama mfanyakazi yaani umeajiriwa jiulize, nitaajiriwa na kufanya kazi za watu hadi lini, ukijiwekea malengo huwezi kuwa kama boss wako? Kwa ujumla, malengo hufungua mlango wa fikra chanya. Haijalishi maisha yako yalivyokuwa bali maisha unayoyatamani kwani haya yanapimwa na wewe mwenyewe na fikra zako.
SIKU NJEMA!
SIKU NJEMA!
0 comments:
Post a Comment