Kocha mpya Stars huyu hapa
, aanza kazi akiwa Ulaya
Martinus Ignatius "Mart" Nooij.
KOCHA Mpya wa kikosi cha timu ya taifa (Taifa Stars), ameanza kazi yake hiyo akiwa bado nyumbani kwao Uholanzi barani Ulaya.
Martinnus Ignatius Nooij ametuma programu kwa ajili ya kuwaendeleza vijana wa kikosi cha Taifa Stars kinachojengwa ambacho kimeweka kambi mjini Tukuyu.
Mart amewahi kuinoa timu ya taifa chini ya miaka 20 ya Burkina Faso na kubwa ya Msumbiji na ndiyo amekuwa chaguo la kwanza la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Habari za uhakika kutoka ndani ya TFF zinasema Nooij, maarufu kama Mart, ametuma programu ambayo wanatumia vijana hao.
“Kocha ametuma programu maalum ya wiki mbili na vijana chini ya benchi la ufundi ambalo liko nao mjini Tukuyu wamekuwa wakiifuata.
“Kocha mwenyewe ameishatumiwa picha kuhusiana na vijana hao na anajua mambo mengi sana ambayo yanaendelea, unaweza kusema yuko pamoja nasi,” kilieleza chanzo.
Kocha huyo anatarajia kutua nchini hivi karibuni kuchukua nafasi iliyoachwa na Kim Poulsen, raia wa Denmark, baada ya TFF kuamua kuvunja naye mkataba.
NA GPL
Kocha huyo anatarajia kutua nchini hivi karibuni kuchukua nafasi iliyoachwa na Kim Poulsen, raia wa Denmark, baada ya TFF kuamua kuvunja naye mkataba.
0 comments:
Post a Comment