Monday 24 March 2014

ONA ALICHOFANYA HUYU MCHEZAJI WA SIMBA BAADA YA KUFUNGWA JANA NA COASTAL UNION!!

 

Hili ndio Tukio alilofanya "Messi" wa Simba Jana Baada ya Kufungwa na Coastal Union

RAMADHANI SINGANO MESSI AVUNJA MLANGO WA KIOO WA UWANJA WA TAIFA KWA HASIRA ZA KUFUNGWA
KIUNGO mshambuliaji wa Simba SC, Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’ anadaiwa kuvunja kioo cha mlango wa chumba cha kubadilishia nguo cha timu yake leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya mechi dhidi ya Coastal Union ya Tanga, Wekundu wa Msimbazi wakifungwa 1-0.
Pamoja na ushahidi uliotolewa na wafanyakazi wa Uwanja wa Taifa kwa askari Polisi kwamba, Messi ndiye aliyevunja kioo, hicho lakini wachezaji wenzake na viongozi wa Simba SC walimtetea.
Polisi walishindwa kuchukua hatua yoyote kuhofia kusababisha vurugu na mchezaji huyo aliondoka uwanjani hapo kuelekea kwenye basi la timu yake akisindikizwa na baunsa.
Tukio hilo limechukuliwa kama hasira za kipigo cha bao 1-0 nyumbani mbele ya Coastal Union katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA