Monday 14 April 2014

AJALI MBAYA: MKUU WA KITUO CHA POLISI KAHAMA MATATANI KWA KUGONGA WATU WATATU NA GARI


Watu watatu wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya kahama mkoani shinyanga kufuatia ajali ya kugongwa na gari iliyokuwa ikiendeshwa na mkuu wakituo cha polisi cha wilaya ya Kahama Elias Haway huku mmoja akiwa ameumia sana sehemu ya mguu.

Ajali hiyo imetokea Jana majira ya 1.30 usiku katika barabara itokayo isaka kuingia kahama mjiniu ambapo Haway akiendesha gari yake Toyota Rav 4 lenye namba T 798 BSK alimgonga mwendesha pikipiki.
Watu waliogongwa wametambuliwa kwa majina ya Joseph Malugu (35) mkazi wa
Mbulu Bw. Fitina Majuto (20) na Cosmas Peter (21) wote wakazi wa mjini humo mitaa ya Nyasubi mjini Kahama. 
Majeruhi wa awali Joseph Malugu akiwa hospitali ya wilaya ya Kahama baada ya kuumia vibaya mguu wake na sehemu zingine za mwili.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema Haway alianza kumgonga mwendesha bodaboda Bw. Malugu katika eneo la Zahanati ya Igalilimi ambapo watu wenye hasira walimzingira wakimtaka asimame naye akakimbia huku akiwagonga tena waenda kwa mguu wawili.
Msukuma Toroli Fitina Majuto akiwa Hospitalini Hapo
Wamesema Haway akionekana kuwa amelewa hakutaka kuwatii watu waliyokuwa wakimweleza ndipo alipoondoa gari lake kwa mwendo kasi na kwenda kumgonga Bw. Majuto katika eneo la Mkude ambae aliumia sana kwenye sehemu ya tumbo na kusababisha utumbo kutoka nje.

Mtembea kwa miguu Cosmas Peter akiwa hoi hospitalini

Shuhuda mmoja Mkulo Iddy amesema eneo hilo pia Haway hakutaka kusimama na aliendelea na mwendo kasi ndipo alipokwenda kumgonga mtu mwingine wa tatu Bw. Peter katika barabara ya eneo la Paradise mitaa ya Nyasubi.

MKUU WA KITUO CHA POLISI KAHAMA ELIUS HAWAII
Haway alipohojiwa amekiri kutokea kwa ajali hiyo huku alisema kuna upotoshaji mkubwa wa taarifa hiyo kwani yeye ndiye aliyegongwa na mwendesha pikipiki huyo wa kwanza.
Amesema alipotaka kusimama kumwona mtu huyo aliyegonga, aliona watu wameanza kumzonga naye akamua kukimbia kwa usalama wake ndipo alipoweza kuwagonga tena wale wengine wawili.

Mganga Mfawidhi wa Hospitari ya wilaya ya Kahama Dk Joseph Foma amethibitisha kugongwa na gari watu hao na wamelazwa katika wodi namba moja katika hospital hiyo, huku hali zao zikiwa mbaya na kwamba wapo katika utaratibu wa kumuhamishia Malugu katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza.
Credit: Kijukuu Blog

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA