ENG. KASEKENYA AKAGUA MAANDALIZI WIKI YA USALAMA BARABARANI
Mwenyekiti mwenza wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Eng. Godfrey Kasekenya akipata maelezo kuhusu masuala mbalimbali ya usalama barabarani alipokagua banda la Jeshi la Polisi ikiwa ni maandalizi ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo kitaifa yanaadhimishwa katika uwanja wa Sheikh Amir Abeid mjini Arusha. Nyuma ya Eng. Kasekenya ni Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Rogatus Mativila akifuatilia.
Mtaalam wa Masuala ya Kijamii wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Bi, Zafarani Madayi akifafanua jambo kwa Mwenyekiti mwenza wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Eng. Godfrey Kasekenya alipokagua maandalizi ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo kitaifa yanaadhimishwa katika uwanja wa Sheikh Amir Abeid mjini Arusha.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Usalama na Mazingira Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Eng. Kashinde Musa akifafanua jambo kwa Mwenyekiti mwenza wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Eng. Godfrey Kasekenya (Kulia), alipokagua maandalizi ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo kitaifa yanaadhimishwa katika uwanja wa Sheikh Amir Abeid mjini Arusha. (Kushoto), ni mtaalam wa TEHEMA wa Wizara hiyo Bw, Simon Chagula akifuatilia.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI
0 comments:
Post a Comment