Wednesday, 9 April 2014

ANGALIA PICHA ZA AJALI ILIYOTOKEA TAZARA JIJINI DAR ES SALAAM


Hapa ni kwenye makutano ya barabara ya Mandela na ile barabara iendayo Mwembe Yanga. ikiwa ni majira ya saa nane mchana wa jana tarehe 8 april ndipo tukio hili limetokea katika maeneo haya.

Eneo hili linafahamika kwa jina maarufu sana kama Vetenali, ambapo eneo hili liko karibu sana na wizara ya kilimo. 
Huyu mwenye mwavuli, ni moja kati ya mashahidi ambao wameshuhudia tukio zima la ajali hiyo, kwa jina anaitwa Bonge (jina la kazi), akiwa anaenda kuwapatia taarifa kamili "traffic" juu ya tukio lilivyotokea.
Kwa mujibu wa Bwana Bonge amesema, "Gari lenye namba T434 ASK, mali ya mwanajeshi, lilikuwa kwenye "service road" likitokea maeneo ya wizara ya kilimo likielekea Sokota, lilipata hitilafu ya breki na kuingia ubavuni mwa lori la mizigo".
Hawa ni moja kati ya mashuhuda wa tukio hili, wakiendelea kushirikiana na "traffic" katika ukamilishaji wa taarifa juu ya tukio hili.
 Wakati kwa upande wa pili likiwepo gari lenye namba za usajili T279 BRH, linalofanya safari zake za Temeke - Ubungo, likiwa limepata ajali baada ya kuchanwa ubavuni na gari la kushusha mizigo.
























































0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA