BASI LA AM COACH LAPATA AJALI ENEO LA IPULI NA KUSABASHA KIFO CHA MWANAFUNZI MMOJA KUFARIKI HAPO HAPO.
Umati mkubwa wa watu ambao ulifiika kushuhudia ajali hiyo mbaya |
Maafisa wa Chama cha Msalaba Mwekundu mkoa wa Tabora walifika eneo la tukio na kusaidia majeruhi wa ajali hiyo. |
Huu ndio uskani wa basi hilo ni mbovu kupindukia na si salama kwa kutumika kwenye magari ya usafirishaji wa binadamu |
Kufuatia
kutokea kwa ajali za mara kwa mara zinazosababishwa na mabasi ya kampuni
ya A.M,wananchi mkoani Tabora wameiomba Serikali kuyapiga marufuku
mabasi ya kampuni hiyo kwakuwa yamebainika kuwa ni mabovu na si salama
kwa wasafiri na wapita njia.
Wananchi
hao ambao walifika katika moja ya tukio la ajali iliyotokea eneo la
Ipuli mnadani kushuhudia ambapo wanafunzi wawili waliokuwa wakienda
shuleni kwa ajili ya masomo kwa muda wa ziada,mwanafunzi mmoja alifariki
papo hapo na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya kugongwa na basi la
A.M Coach lenye nambari za usajili T 861 ATZ lililokuwa likifanya safari
zake kutoka Mwanza kwenda Tabora.
Aidha
wananchi hao ambao hawakutaka kutajwa majina yao wamedai kuwa mabasi ya
kampuni hiyo yamekuwa yakiingia mjini kwa kasi kubwa huku yakionekana
kuyumba barabarani na kuzidi kutia shaka hata watumiaji wa barabara kuu
za mkoa wa Tabora.
Wameitahadharisha
Serikali kuwa endapo watayaachia mabasi hayo huenda yatasababisha ajali
mbaya zaidi na hata vifo visivyo vya lazima.
via>>kapipij blog
0 comments:
Post a Comment