WAZIRI LUKUVI AZIDI KUANDAMWA
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,William Lukuvi.
Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu nchini, imemtaka Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi, (pichani) kujiuzulu wadhifa wake kutokana na kauli yake ya kwamba serikali tatu ikipitishwa jeshi litatwaa madaraka.
Kadhalika, Lukuvi anadaiwa kusema kuwa wanaotaka nchi yao hawawezi kujitegemea bali wanataka serikali ili wapate nafasi ya kujitangaza kuwa nchi ya Kiislamu.
Pia anadaiwa kutamka kwamba Jumuiya ya Uamsho ni taasisi ya Waislamu wenye msimamo mkali.
Kauli ya hizo zilitolewa na Msemaji wa jumuiya hiyo, Rajabu Katimba, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Msikiti wa Mtambani wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam jana.
''Kauli hizo zinaonyesha Lukuvi ni mmoja wa mawakala wa mfumo kandamizi wa muda mrefu," alisema.
Alisema kuwa Waislamu hawakutarajia waziri mwenye mamlaka makubwa na aliyeaminiwa na Rais na kumwakilisha Waziri Mkuu kutamka kauli za uchochezi tena kanisani.
"Kama alikuwa akisisitiza amani, mbona hakuzungumzia ulipuaji wa mabomu unaoendelea Arusha, tena mpaka kanisani, na je wale ni Uamsho,? Alihoji.
Alisema mpaka sasa uchunguzi wa milipuko ya mabomu Arusha, haijawekwa wazi wala kuwataja wahusika.
CHANZO: NIPASHE (FS)
0 comments:
Post a Comment