WAZIRI MKUU WA KOREA KUSINI AJIUZURU: NI BAADA YA KUZOMEWA ALIPOTEMBELEA FAMILIA ZA WAATHIRIWA WALIOTOWEKA KATIKA FERRY BAADA YA KUZAMA KATIKA HALI YA KUTATANISHA.
Waziri mkuu nchini Korea Kusini amejiuzulu kutokana na vile serikali yake ilivyolichukulia swala lote la ferry iliozama siku kumi na moja zilizopita.Chung Hong Won amesema kuwa kusalia afisini ni mzigo mkubwa kwake.Bwana Chung alizomewa alipozitembelea familia za waathiriwa waliotoweka katika ferry hiyo ya Sewol,baada ya kuzama katika hali ya kutatanisha.
Takriban watu 200 wanadaiwa kufa maji katika tukio hilo huku zaidi ya mamia wengine wakiwa hawajulikani waliko,wengi wao wakiwa wanafunzi na walimu waliokuwa wakielekea katika ziara ya shule.
Wapiga mbizi bado wanaendelea kuwasaka waathiriwa chini ya ferry hiyo iliozama.
Ripoti za awali zimedai kuwa watu wote wametolewa katika boti hiyo.
CHANZO BBC
0 comments:
Post a Comment