DAR YADAIWA KUSAMBAZA UGONJWA WA DENGUE MIKOANI
Ugonjwa wa homa ya dengue umeanza kusambaa kwa kasi mikoani ambapo sasa wagonjwa wapya 50 wamegundulika huku ikielezwa wengi ni waliotoka nao mkoani Dar es Salaam.Hayo yalisemwa jana mjini hapa na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Afya na Dharura, Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii Dk Elias Kessy.Alikuwa akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Steven Kebwe wakati wa kufunguliwa mafunzo kwa Waganga Wafawidhi wa Mikoa, Maofisa Afya, Wauguzi Wakuu wa Mikoa yote
ya Tanzania yenye lengo la kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa
kadhaa nchini ambapo asilimia kubwa ya watu hao walikuwa wamesafiri
kutoka jijini Dar es Salaam na kuingia na ugonjwa huo kwenye mikoa
waliyokwenda.Alisema tangu ugonjwa huo uanze Januari mwaka huu zaidi
ya watu 850 wameugua na wagonjwa wanne kati yao walipoteza maisha.
Alisema jitihada zinaendelea kudhibiti kueneakwa ugonjwa huo.Alisema
bado tatizo hilo ni kubwa na utafiti unaendeleana Wizara kwa
kushirikiana na Bohari Kuu ya Madawa (MSD), wamekuwa wakisambaza vifaa
na dawakwenye maeneo mengi nchini.Kwa upande wake, Naibu Waziri wa
Afya alisema ugonjwa huo ni mpya katika ukanda wa joto. Alisema ni
muhimu kujipanga kuhakikisha ugonjwa huo hauenei kama ilivyo
sasa.Alisema kazi ni kubwa iliyofanyika katika kutibu wagonjwa
waliogundulika lakini jambo la muhimu ni kuangalia suala zima la usafi
wa mazingira."Tumekubaliana kupita nchi nzima kuangalia suala la usafi
wa mazingira linapewakipaumbele, maeneo mengi yamekuwa na nyasi,
madimbwi na hata matairi ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa mazalia
makubwa ya mbu kutokana na maji kutuama humo kwa muda mrefu,"
alisema.Alitaka wataalamu hao wa afya kusimamia vizuri suala la usafi
wa mazingira na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea."Tiba
pekee ya homa ya dengue ni usafi wa mazingira, wataalamu kwenye
halmashauri walionehilo, tatizo hili liko mbele yetu tukiligeuza kuwa
malaria ya pili litakuwa tatizo kubwa sana," alisema.Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma Dk Ezekiel Mpuya alisema hospitali ya mkoa ilipata
kesi moja ya mtu aliyekuwa akiugua ugonjwa huo."Huyo aliyeugua alikuwa
amekwenda Dar es Salaam kikazi na aliporudi akaanza kuumwa na kulazwa
lakini alitibiwa na kupona na sasa hakuna mgonjwa tena hapa Dodoma,"
alisema. Washirikizaidi ya 70 wanahudhuria mafunzo hayo.Ugonjwa huo
unaotokana nakirusi kinachosambazwa na mbu aina ya Aedes , unatajwa
kuwa ni wa ukanda wa joto. Dalili za ugonjwa huo ni homa, kuumwa
kichwa, maumivu ya viungo na uchovu huku wakati mwingine, dalili zake
zikifanana na za malaria.Taarifa iliyotolewa hivi karibuni bungeni,
ilisema Sh milioni 132 zimeshatumika na wakati huo huo Sh milioni540
zimetengwa kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa dengue ulioibuka
jijini Dar es Salaam. Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Afya na
Ustawi waJamii, Dk Stephen Kebwe katika taarifa yake bungeni, ilisema
imeshafanya utafiti mkoani Kagera, Morogoro na Kigoma na kuthibitisha
kuwa haijaathirika na ugonjwa huo.Dk Kebwe alisema Serikali
itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kukabili ugonjwa huo kadri
itakavyohitajika. Alihimiza uvaaji wa nguo ndefu na zenye mikono
mirefu hususani katika maeneo ambayo ugonjwa huu umeripotiwa kuepuka
kuumwa na mbu husika
0 comments:
Post a Comment