MATOKEO YA UCHANGUZI MALAWI YATANGAZWA.
Hatimaye Tume ya uchaguzi nchini Malawi imeanza kutoa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo jumanne iliyopita.
Matokeo
hayo ambayo ni asilimia 30 tu ya kura ambazo zimehesabiwa hadi sasa
yanaonyesha kuwa mgombea wa chama kikuu cha upinzani Democratic
Progressive Party-DPP Profesa Peter Mutharika anaongoza kwa kura 683,621
akifuatiwa na Dr Joyce Banda wa Peoples Party kwa kura 372,101
Mgombea
Urais wa chama kikongwe cha kisiasa nchini humo, Malawi Congress Party
MCP Mchungaji Dr Lazarus Chakwera anashika nafasi ya tatu kwa kujipatia
kura 289,145 huku Atupele Muluzi wa United Democratic Front- UDF
akikusanya kura za wamalawi 269,250
Mwandishi
wa BBC Baruan Muhuza ambaye anafuatilia uchaguzi huo nchini humo,
amesema mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mackson Mbendera aliwaambia
waandishi wa habari mjini Blantyre usiku wa kuamkia leo kuwa tume yake
kwa pamoja na wawakilishi wa vyama vya siasa wamethibitisha matokeo
hayo.
Udanganyifu
Katika
mkutano huo Jaji Mbendera amesema tume yake imegundua kuwa kulikuwa na
udanganyifu katika baadhi ya maeneo ambapo wamekuta idadi ya kura
zilizopigwa ni zaidi ya watu walioandikishwa kupiga kura, na kwamba
wamezuia matokeo hayo hadi watakapo pata ufumbuzi na ukweli wa hali
ilivyokuwa.
Wakati
huo huo Mahakama nchini humo imezuia uamuzi wa bodi ya wakurugenzi wa
shirika la utangazaji la Malawi MBC kumlazimisha Mkurugenzi Mkuu Dr
Benson Tembo kwenda likizo ya lazima na haraka.
Uamuzi
huo umefuatia baadhi ya wanasheria kutoka kamisheni ya wanasheria wa
Lilongwe kuweka zuwio mahakamani kupinga uamuzi wa bodi ya shirika hilo.
Itakumbukwa
kuwa ijumaa asubuhi Dr Tembo alipewa barua ya kumtaka aende likizo ya
lazima kutokana na madai kuwa ameshindwa kufuata maelekezo ya mwajiri
wake ambaye ni serikali.
Miongoni
mwa madai hayo ni pamoja na vyombo vya shirika hilo ikiwemo television
na radio za taifa kuendelea kutoa matokeo ya uchaguzi ambayo
hayajathibitishwa na Tume ya uchaguzi.
Pia MBC
ilishindwa kurusha moja kwa moja matangazo ya mkutano wa Rais Joyce
Banda na waandishi wa habari mjini Lilongwe siku ya alhamis, ambapo Dr
Banda alikuwa akitoa maelekezo kwa tume ya uchaguzi kuanza kuhesabu kura
kwa kutumia mikono na kuzuia kutoa matokeo kutokana na udanganyifu
uliojitokeza
0 comments:
Post a Comment