MVUA YAWAPIGANISHA MADEREVA MOSHI
Stori na KD MULA
Dereva wa dala dala
ambayo nambari zake hazikufahamika alijikuta katika timbwili zito baada ya
kuvamiwa na dereva wa piki piki almaarufu boda boda leo wakati akiwahi kupaki
gari katika stendi ya dala dala eneo la majengo kwa mtei mjini moshi.
Madereva hao ambao majina yao haya kupatikana mapema
walishindwa kuzuia hasira zao na kutupiana makonde asubuhi asubuhi huku
wakiwapa mzigo mashuhuda burudani ya bure kwa umahiri waliounoesha.
![]() |
NGOMA INOGILE |
Akisimulia kisa hiki shuhuda alietutumia habari hii alisema
kisa cha ugomvi alisema
“huyu dereva wadala dala alikuwa akiwahi kupaki gari kwenye
kilo na kama ilivyo wakati wa masika ALIMMWAGIA MAJI dereva wa boda boda
aliekuwa amejiegesha pembeni na alipotakiwa kusimama aliendelea na safari sasa alipopaki
tu ndio jamaa akamvaa na kuanza kutupiana makonde”.
![]() |
MASHUHUDA WAKIENDELEA KUFAIDI SHOW |
![]() |
WADAU WAJA KUAMUA UGOMVI |
Baada ya kuamuliwa na mpaka mwandishi wetu anaondoka eneo la
tukio madereva hawa kila mmoja alikuwa akielekea kituo cha polisi cha majengo
SIJUI WALIPOKUTANA HUKO NINI KILITOKEA…..
PICHA NA MOHAMED MGANGA
0 comments:
Post a Comment