Showing posts with label MATUKIO. Show all posts
Showing posts with label MATUKIO. Show all posts

Saturday, 21 June 2014

MOTO MKUBWA WATOKEA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM).


Moto uhuu umezuka  karibu na hostel za mabinti katika skuli ya sanaa na lugha (humanities), chanzo cha moto huo hakijajulikana mpaka sasa..... tutakujuza kadri taarifa zitavyozidi kutolewa.

mashuhuda wakipiga picha katika eneo la tukio


UKATILI****MWANAFUNZI DARASA LA NNE AKATWA MAPANGA NA MFANYAKAZI WA NYUMBANI



Mama mzazi akiwa na Mwanafunzi wa darasa la nne wa shule ya msingi Motomoto kata ya Vumilia wilayani Urambo aliyekatwakatwa mapanga na mfanyakazi wa nyumbani kwa madai ya kunyimwa hela na baba mzazi wa mtoto hu
========  =======  =======
Na Allan Ntana, Urambo

MTOTO Perezi Christian (12) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Motomoto iliyoko katika kata ya Vumilia wilaya ya Urambo mkoani Tabora amekatwakatwa  mapanga mikononi na miguuni na   mfanyakazi wa nyumbani.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa akiwa wodini alikolazwa Perezi mama mzazi wa mtoto huyo Regina Fumbo (45) ambaye ni muuguzi katika kituo cha afya Zogolo kilichoko katika tarafa ya Nyasa wilayani Nzega alisema mtoto wake amekatwakatwa mapanga na mfanyakazi wa shambani anayeitwa Abdallah Alfan muha mwenye umri wa kati ya miaka 39-44.

Alisema awali hapakuwa na ugomvi wowote kabisa kila alichotaka alikuwa anapewa, alichukua uamuzi huo kwa hasira tu kwani tayari alikuwa ameahidiwa kulipwa hela alizokuwa ameomba kwa bosi wake ambaye ni baba mzazi wa mtoto huyo Bw. Christian Mlela.
‘Hili tukio limenisikitisha sana, nilipigiwa simu nikiwa kazini kwangu kule Nzega, nikajua mtoto wangu sitamkuta hai tena, nilikuja mbio mpaka wodi ya wanaume alipolazawa, kwa kweli hali yake haikuwa nzuri, namshukuru Mungu sasa hivi anaendelea vizuri, na huyo mtuhumiwa ameshakamatwa na polisi’, alisema.

Mtoto Perezi alipohojiwa na mwandishi wa gazeti hili akiwa wodini katika hospitali ya wilaya Urambo alisema kabla ya kukatwa mapanga babake hakuwepo, mtuhumiwa huyo alipokuja alidai baba hataki kumpa hela yake yeye anajali kazi zake tu, sasa ngojea, ndipo akaanza kumkata kata.

‘Ninaumia sana, sijui kama nitapona ili niendelee na shule kama nilivyokuwa, jamani naomba madaktari wanisaidie nipone haraka kabla shule hazijafunguliwa mwezi ujao’, alisema mtoto Perezi  kwa masikitiko makubwa mbele ya mwandishi.

Baba mzazi wa Perezi ambaye ni Katibu Meneja wa Chama cha Msingi Kasela katika kijiji cha Motomoto alipohojiwa na mwandishi wa gazeti hili alidai walikuwa wamekubaliana amlipe sh 200,000 watakapouza tumbaku msimu huu na tayari walikuwa wameshaikausha hivyo wakawa wanasubiri kupima uzito wake na kujua gredi ili wakauze.

‘Huyu bwana alianza kunidai hela hata kabla ya kuuza tumbaku kama tulivyokubaliana, nikamwomba avumilie kidogo ili nimtafutie kwani yeye alidai anataka kurudi kwao Kigoma, lakini awali nilimpa hela kidogo za kujikimu kiasi cha sh 20,000’, aliongeza.

Aidha aliongeza kuwa tayari wameshatoa taarifa kituo cha polisi Urambo na mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya hatua zingine za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.

Friday, 20 June 2014

MAAJABU***ANGALIA PICHA BIBI WA MIAKA 60 AJIFUNGUA MTOTO


Photo: Nigeria: Bibi wa miaka 60 ajifungua salama mtoto wa kike!

- Ni baada ya kuhangaika miaka 31 akisaka mtoto

Soma zaidi => http://bit.ly/1rbqjj0

Nigeria: Bibi wa miaka 60 ajifungua salama mtoto wa kike!
- Ni baada ya kuhangaika miaka 31 akisaka mtoto
here is hope for women who think age is a big barrier to their conception.
A 60-year-old Nigerian woman just gave birth to a baby girl at a hospital in Lagos.
After 31 years of childlessness, Mr Omolara Irurhe has finally set her eyes on her own child.

After several attempt to give birth failed, she ended up in the most unlikely hospital and country in 2010 when she started an IVF (Invitro Fertilization treatment) at St Ives Hospital in Lagos.

This past Monday, what began as a seed hope four years ago culminated in the delivery of a bouncing baby girl.

Mrs. Irurhe becomes the oldest IVF mother in Africa. The global recognition for oldest IVF delivery goes to Rajo Deri Lohan, an Indian who in 2008 was delivered of a baby at 69 years.

The IVF Unit at St. Ives Hospital successfully aided the conception and delivery of the baby and has now equaled the United Kingdom’s record of IVF age delivery.

The team of doctors at the hospital was led by the Chief Medical Director, Dr. Tunde Okewale, who expressed joy at the successful delivery. Okewale said the physical condition of the mother – and not just the age – is a major factor that determines the success of conception and delivery through IVF.

“We treat only after strict medical check of couples. For us, age is not important in our decision to take her on; what was important is the physical condition of the mother. Older women generally make better patients in our experience,” Okewale said.

Hear what the excited new mother said;

“I believe we should not limit God and what the doctors can do in this modern age. I believe this is the appointed time. I was very hopeful throughout the years I was childless and I remained focused on God. We went to many hospitals but we didn’t give up,” “We didn’t have much pressure, even though our marriage is cross cultural –I am Yoruba; my husband is Edo- but we remained hopeful,” .

Desmond Adekunle Irurhe was elated at the birth of his baby. When asked if she supported his wife going for the IVF he replied:

“ I supported her throughout because my wife was dogged and she believed in herself. When I saw her faith, I had no choice but to go with her. She kept telling me she would have her child”. “ The hospital didn’t give us any problem, they were very helpful and we thank them for the successful delivery.”

The couple paid less than one million naira for the IVF treatment

“I will advise couples who are trying to get a baby to try the IVF. My case has rekindled hope for the barren woman. I will say the couple should relax and take it as it comes, they will surely smile,”. “ I don’t know if I will have another baby, but if the doctors say I can, I will try it,” she said, smiling.

“I give glory to God, we kept our faith in God, we believe this is God’s appointed time. – the mother said

This is a very good news coming from Nigeria.

MTOTO AZALIWA NA MKIA , AABUDIWA KAMA MUNGU,INDIA


 


Balaji3
Mvulana mdogo aliyezaliwa na mkia unaofikia urefu wa inch saba anatarajia kufanyiwa upasuaji ili utolewe licha ya kuwa anaabudiwa kama Mungu na watu wa jamii yake.
Balaji
Arshid Ali Khan, mwenye miaka 13 anaweza kuathiriwa ukuaji wake kutokana na mkia huo ingawa unamfanya aonekana kama alama ya uponyaji katika Jimbo la Punjab, India.
Mtoto huyo anayetumia kiti cha watu wenye ulemavu amekuwa akiabudiwa na watu wa jamii yake kama Mungu aliyepewa jina la Balaji.
Balaji2
Khan anasema mkia huo amepewa na Mungu na anaabudiwa kwasababu ni Mungu huyo huyo ndiye anayemuomba ambapo maombi ya watu hugeuka kuwa kweli.
Anasema hajisikii vizuri wala vibaya kuwa na mkia huo yeye anaona sawa tu.
Arshid sasa anaishi na babu yake Iqbal Qureshi, na wajomba zake wawili baada ya baba yake kufariki akiwa na umri wa miaka sita na mama yake kuolewa tena.

Thursday, 19 June 2014

MAAJABU: MTOTO WA KINGONI APOTEA KIGOMA, AIBUKA AKIWA MMASAI HUKO CHALINZE

 Mtoto Samson Matei Joseph akiwa na baba yake mzazi, Bw. Matei Joseph.


Mtoto aliyezaliwa na wazazi wa kabila la Kingoni (Mngoni), Samson Matei Joseph wa Nguruka Kata ya Nguruma wilayani Uvinza mkoani Kigoma alipotea miaka miwili iliyopita lakini katika hali ya kushangaza, hivi karibuni ameibuka akiwa ni Mmasai baada ya kusakwa bila mafanikio.



Akizungumza na paparazi kwa njia ya simu akiwa mkoani Kigoma, baba mzazi wa mtoto huyo, Matei Joseph alisimulia mkasa mzima na kusema kuwa yeye na mkewe walimpoteza mtoto wao huyo Desemba 16, 2012 wakati huo akiwa na umri wa miaka 11, akisoma darasa la tatu.
Alisema kuwa baada ya kupotea walimsaka kila kona ya nchi bila  mafanikio na kuamua kumuachia Mungu.
“Siku moja niliona simu yangu ya mkononi ikiita kwa namba ngeni, nilipopokea kuna bibi kajitambulisha kwa jina la Mama Vero akasema kuna mtoto anataka kuongea na mimi.
“Alimpatia simu mtoto ambaye alijitambulisha kuwa yeye ni Samson, nilifurahi na kushangaa lakini pia sikuamini kwani alikuwa akiongea Kimasai!” alisema Matei.


Matei alisema mwanaye huyo alimwambia kuwa alikuwa Chalinze mkoani Pwani akihitaji msaada, akilalamika kuteswa kwa muda mrefu na Wamasai ambao ndiyo waliomtorosha.
“Nilifunga safari hadi Chalinze na kukuta kweli ni Samson, lakini alikuwa katika muonekano wa Kimasai kwani aling’olewa meno nane kama mila zao zinavyosema,” alisema Matei.
Aliendelea kusimulia kwamba alipomhoji mwanaye alidai alichukuliwa na Mmasai aliyemtaja kwa jina moja la Nasoro ambaye alikuwa akiuza dawa na pipi mkoani Kigoma kabla ya kumuiba na kutimkia naye Chalinze.
“Nilishangaa kusikia alichukuliwa na Mmasai niliyekuwa namjua ambaye alikuwa akifanya biashara pale Nguruka huku Kigoma.
“Alimrubuni mwanangu kuwa anakwenda kufanya kazi dukani kwa mama Yoyoo, kumbe ni kuchunga ng’ombe na mabwawa ya maji,” alisema Matei.
Baada ya kupata habari kamili, Matei alikwenda Kituo cha Polisi cha Nguruka na kutoa taarifa ambapo alifungua jalada la kesi namba NGK/IR/2022/2014- KUTOROSHA MTOTO.
“Baada ya kuchukua RB niliambiwa nifanye juu chini nikamfuate mwanangu Chalinze kisha nimtafute Nasoro kwa ajili ya kumfungulia kesi ya kujibu.
“Kweli nilifanya hivyo, tulipomkamata Nasoro hakuwa na la kujibu, nikamchukua mwanangu nikarudi naye Kigoma,” alisema Matei.
Kwa upande wake mtoto Samson alisema kuwa alikuwa amewekwa kwenye mapori ya Milima Mitatu Chalinze Kata ya Vizimbwi ambapo alikuwa akichunga ng’ombe na mabwawa ya maji.
Alisema alifanikiwa kutoroka baada ya kuua sungura na kuwauzia Wamasai wengine ambapo alipata fedha ndipo akakutana na Mama Vero ambaye alimnunulia vocha akawapigia wazazi wake kwa kuwa alikuwa akikumbuka namba zao kichwani.
na matukio tz

HOFU YATANDA*** KITU KINACHOHISIWA BOMU MLIMANI CITY CHAOKOTWA,,CHEKI HAPA



HUKU watu karibia 60 nchini kenya wakiuawa kwenye mashambulizi ya kigaidi, katika hali isiyo ya kawaida nchini Tanzania, walinzi wa Maduka ya Mlimani City jijini Dar wamejikuta wakipata mchecheto wa aina yake baada ya kitu kilichodhaniwa ni bomu kukutwa kwenye eneo la kuegeshea magari. 

Walinzi wa maduka ya Mlimani City jijini Dar wakikagua kitu kinachosadikika kuwa ni bomu.Tukio hilo lilitokea Juni 16, mwaka huu ambapo kwa mujibu wa shuhuda aliyeomba kusitiriwa jina, aliona gari dogo jeupe likiangusha kifaa hicho kilichodhaniwa ni bomu kisha likatoweka.


Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa baada ya gari kutoweka, dada mmoja alipita eneo hilo na kukuta kitu hicho kilichofungwa nyaya kikiwa ndani ya mfuko, akashtuka na kwenda kumtonya mlinzi wa eneo hilo ambaye alifika mara moja na kuwaita wenzake.
...Ukaguzi ukiendelea.
Taarifa za uwepo wa kifaa hicho ziliwafikia waandishi wetu waliokuwa wakipiga doria katika eneo hilo na haraka wakasogea karibu kuwashuhudia walinzi hao wa Kampuni ya Ulinzi ya Omega wakiwa wamekizunguka kifaa hicho kwa umakini mkubwa.
Walinzi hao walimuita kiongozi wao ambaye alifika na kukichunguza kifaa hicho ambapo alipokifungua aligundua ni betri bovu la pikipiki.Waliichukua betri hiyo na kuitupa huku wakitawanyika kurudi kwenye maeneo yao ya ulinzi.



Eneo la Mlimani City

UKATILI***KICHANGA CHATUPWA JALALANI...MAMA YAKE AKAMATWA NA POLISI..


Mwili wa kichanga.

Mama anayedaiwa kutupa kichanga akiwa na mwanae wa kwanza.
 
Difenda la polisi likiwa eneo la tukio kuchukua mtuhumiwa na mwili wa kichanga.
MWILI wa kichanga umeokotwa eneo la Njiro jijini Arusha juzi baada ya kudaiwa kutupwa na mama mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja.
Baada ya kichanga hicho kuokotwa, wananchi walitoa taarifa polisi waliofika na kufanikiwa kumkamata mama mwenye kichanga hicho.

KALI YA LEO****MBUNGE AKWEA BODABODA KUWAHI NDEGE BAADA YA KUKWAMA KATIKA FOLENI



Adha ya Foleni jijini Dar es Salaam imemkumba mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka nchini Tanzania, Shy-Rose Bhanji aliyekuwa akisafiri kwa ndege na kulazimika kukwea bodaboda ili imuwahishe Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere Dar es Salaam hii leo.

HII KALI***Mtoto wa miaka tisa anayemfanyia ukatili mama yake, amshikia kisu akitaka kumuua

bobbi2
Wewe unadhani ukatili wa kijinsia ni kwa wazazi au walezi tu kwenda kwa watoto? Hapana hata kwa baadhi ya wazazi pia inatokea kwa kufanyiwa ukatili na watoto wao ila hushindwa kujitokeza hadharani kusema mbele ya jamii kwa aibu au kufanya hivyo mara chache.Hii imemtokea mwanamke huyu aitwaye Bobbi kutoka Southampton , Uingereza ambapo anasimulia jinsi alivyofanyiwa ukatili na mtoto wake mwenye umri wa miaka tisa akitaka kumchoma kisu na wakati mwingine kumvizia akitaka kumuua.

bobbi
Mtoto huyo aitwaye JJ mara kadhaa amekuwa akifanya mashambulizi ya vurugu kwa mama yake kwa kumpiga, kumrushia vitu kichwani na wakati mwingine kumvuta nywele ambapo katika tukio jingine alijaribu kumchoma kisu akitaka kumuua.
bobbi3
Hali hiyo ilimlazimu Bobbi kuondoa vitu vyote vyenye ncha kali karibu na nyumbani ili kuepusha hatari ambapo hata kwa baba yake wa kambo imekuwa ngumu kwake kuishi pamoja na mtoto huyo kwani ni vita kali.

Wednesday, 18 June 2014

UKATILI DHIDI YA MTOTO AFUNGIWA NDANI NA KUCHOMWA MOTO NA MAMA YAKE MKUBWA


Mtoto Fatuma Hassan (9) anyedaiwa kufungiwa ndani kwa siku tatu kisha kuchomwa moto mikononi na mama yake mkubwa aliyetajwa kwa jina moja la Diana (38), mkazi wa maeneo ya Tandale.

UNYAMA ulioje? Mtoto Fatuma Hassan (9) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Hekima iliyopo Tandale, Dar anadaiwa kufungiwa ndani kwa siku tatu kisha kuchomwa moto na mama yake mkubwa aliyetajwa kwa jina moja la Diana (38), mkazi wa maeneo hayo, kisa kikielezwa kuwa ni shilingi mia tano.

Tukio hilo lilitokea Juni 10, mwaka huu katika maeneo hayo ya Tandale Sokoni ambapo mama huyo alikuwa akiishi na mtoto wa mdogo wake kwa kile kilichodaiwa kuwa alimchukua kwa ahadi ya kumsomesha lakini kuna madai kuwa badala ya kufanya hivyo, alimnyanyasa.
Mama mkubwa wa mtoto Fatuma Hassan anyetuhumiwa kumtesa mtoto huyo.
Taarifa zilidai kwamba mama huyo aliamua kumfanyia ukatili mtoto huyo akidai kuwa alichukua fedha hizo akiwa na mwanaye wa kumzaa kwa ajili ya kwenda kutumia kununulia sambusa na juisi shuleni.
Ilisemekana kwamba kitendo hicho kilimkera mama huyo na kuamua kuwasubiri warudi ili awaulize kama kweli walichukua fedha hizo ambapo walikiri kuzitumia shuleni.
Wakizungumza na wanahabari wetu, majirani wa eneo hilo walisema kuwa walimuona mtoto Fatuma akipigwa na mama’ke huyo mkubwa fimbo na kumchoma moto mikononi pasipo kumpeleka hospitali huku akimpa onyo kali na kumfungia ndani.
Walisema kuwa mwanamke huyo amekuwa akimfungia ndani na kwenda kwenye genge lake.
Mjumbe  wa  eneo hilo, Said Sundi na Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Pakacha, Ally Mdee wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Wananchi walifikia hatua ya kufananisha tukio hilo na lile la mtoto aliyefungiwa kwenye boksi mkoani Morogoro, Nasra Mvungi (marehemu), walimkamata na kupiga simu katika Kituo cha Polisi cha Magomeni ambapo askari walifika na kumchukua mwanamke huyo.
Pia walimpeleka mtoto Fatma kwenye Hospitali ya Magomeni anakopatiwa matibabu huku mwanamke huyo akishikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano na alifunguliwa kesi ya kujeruhi yenye jalada namba MAG/RB/5676/2014

HII KALI**VURUGU KALI ZATOKEA WILAYANI MULEBA BAADA YA WAZAZI KUKATAA MAITI ILIYONYOFOLEWA VIUNGO


Vurugu kubwa zimetokea katika kijiji cha Buyango wilayani Muleba mkoani Kagera baada ya wazazi kuikataa maiti ya mtoto wao kwa madai amenyofolewa viungo vyake vya mwili hali iliyosababisha polisi kutumia mabomu ya machozi kutawanya makundi yaliyofunga barabara na kubomoa chumba cha kuhifadhia maiti kutafuta viungo hivyo.
 
Vurugu hizo zimetokea baada ya mama mmoja mkazi wa Arusha aliyepeleka maiti ya mtumishi wake wa ndani na kuwakabidhi wazazi wake kwa masharti ya kutoifunua hali iliyosababisha mtafaruku mkubwa ambapo mama huyo amelazimika kwenda hospitali kukabidhi mwili huo ambapo baadhi ya ndugu na jamaa walivamia chumba cha kuhifadhi maiti na kubomoa mlango kisha waka angalia mwili ambao wameukuta ukiwa na majeraha na kwamba haufanani na binti yao aliyefahamika kwa jina la Ajela Tilifon mwenye umri wa miaka 16 aliyechukuliwa kijijini hapo tangu mwaka 2012 kwa lengo la kwenda kufanya kazi za ndani mjini Arusha na kwamba baada ya ndugu kukataa kupokea mwili askari polisi wamewakamata ndugu na mwaandishi wa habari kwa madai kuwa wanahamasisha vurugu.
Kufatia hali hiyo mkuu wa wilaya ya Muleba Bw. Lebris Kipuyo alilazimika kufika eneo la vurugu na kuamuru askari polisi kutawanya wananchi ili magari yaweze kupita na baadaye alifika hospitali na kuteuwa baadhi ya ndugu,jamaa na wazazi wa mtoto ambao walikagua mwili wa marehem kisha mkuu wa wilaya akawahutubia wananchi na kuwataka walioshuhudia mwili waseme ukweli walichokiona nao bila kusita wamesema maiti inamajeraha tumbo limetobolewa na sehemu za mwili zimekwaruzika kisha akavishwa nguo na soksi ili kuficha ukweli.
Naye mwaandishi wa habari wa kujitegemea gazeti la Mwananchi aliyejeruhiwa na askari polisi kwa kupigwa virungu Bw. Shaban Ndyamkama amesema kuwa yeye ndiye aliyetoa taarifa za vurugu hizo kwa mkuu wa wilaya ya Muleba baada ya askari kufika eneo la tukio walimkamata na kumshambulia kwa vipigo kisha wakamshikilia kwa muda hadi wananchi waliposhinikiza kuachiwa kwake na baada ya waandishi wa ITV,Radio one kanda ya ziwa kumuomba kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Bw. George Mayunga ambaye amekiri kwa njia ya simu kuwa vurugu hizo zimesababisha uvunjifu wa amani na kumtaka mkuu wa polisi wilaya ya Muleba kumuachia huru mwaandishi wa habari ambaye amepelekwa hospitali na wananchi kwa matibabu zaidi.
 
chanzo:ITV

Bosi adaiwa kumbaka house girl wake mwenye umri wa miaka 14 siku 4 baada ya kuanza kazi


binti

Mfanyakazi wa ndani, miaka 14 mkazi wa kijiji  cha Mdenge, Kata ya Likombe katika Wilaya ya Mtwara, amebakwa na mwajiri wake usiku wa kuamkia jana na kumsababishia maumivu makali na kisha kutokomea kusikojulikana.Akiongea  jana Jumatatu Juni 16, 2014, Mama mzazi wa mtoto huyo, mwenye umri wa miaka 36, amesema mtoto wake amekumbana na masahibu hayo siku nne tangu aanze kufanya kazi kwa mwajiri wake aliyemtaja kwa jina moja la, Sharifu (42), mfanyakazi katika kiwanda cha kuzalisha saruji cha Alosko mkoani humo.Amebainisha kuwa, mtoto wake alipata kazi ya kufanya kazi za ndani kwa mwajiri huyo Juni 12, 2014 ambapo ilipofikia usiku wa kuamkia leo mtoto huyo aliamua kutoroka nyumbani kwa mwajiri wake anayeishi na mke wake bila kuaga kutokana na hofu ya kuzuiwa kwenda kwao au kufanyiwa unyama zaidi na kukimbilia nyumbani kwao.

“Alivyopata kazi anasema hii sio mara ya kwanza kufanyiwa hivyo hii ni mara ya pili, usiku wa kuamkia Jumamosi ya Juni 14, 2014 alimuingilia mtoto wangu na alipomwambia atatoa taarifa akamwambia asiseme kwa mtu yeyote kwani atamfanya kama mtoto wake, sasa leo tena amemuingilia.
“Nimemkuta yule mama aliyekuwa anafanya kazi kwake amesema alihisi kuwa kuna huo mchezo lakini aliogopa kuniambia tangu Jumamosi” alisema  mama  wa  mtoto.
Kwa upande wa mtoto huyo, amesema ,“Nilikuwa nimelala usiku wa manane ndipo niliposhtuka, nilipotaka kupiga kelele alinikataza kuwa nisiseme kwa mtu kwani atanifanya kama mtoto wake, na usiku wa kuamkia leo alikuwa ameenda kuangalia mpira nilivyoshtuka alikuwa ameniingilia kimwili ndio nikaondoka asubuhi kwenda kwetu kwa maana alisema nisipige kelele”
Taarifa yatolewa Polisi
Mama mzazi wa mtoto huyo amesema wameripoti tukio hilo katika Kituo cha Polisi Mtwara, kwa tuhuma hizo na amefunguliwa jalada namba Mt/RB/2198/2014 ambapo mtoto huyo amefanyiwa vipimo katika kituo cha Polisi kilichopo wilayani humo na kugundulika kuwa alibakwa na kupata majeraha makubwa.

Mtandao ulimtafuta Kamanda wa Polisi wa mkoani humo, Zelothe Stephen, ambaye hakupatikana kupitia simu yake ya mkoni baada ya kuita bila kupokelewa, huku upande wa ndugu wa mtuhumiwa wakigoma kuongelea suala hilo wakidai hawajui alipo ndugu yao licha ya kushangazwa na tukio hilo.
-MATUKIO TZ

Monday, 16 June 2014

PICHA::WASANII WALIPOKULA CHAKULA CHA JIONI IKULU NDOGO DODOMA NA RAIS KIKWETE


 Msanii Jb akiteta na Rais Kikwete
 Rais Kikwete akionge na Ommy Dimpoz alipompa kazi yake

 Ommy Dimpoz akichukua chakula
 Meneja wa bia ya Kilimanjaro George Kavishe

 
 Rais Kikwete Akifurahi na Msanii Mrisho Mpoto


 Wasanii Izo B na Quick Racka wakichukua chakula
 Ruge Mutahaba na Sebastian Maganga
 Queen Darleen akichukua chakula
 Ridhiwan Kikwete Mbunge wa chalinze akichuka chakula
 Shilole na Mbebe wakee


OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA