ADHABU KUBWA YA MPENZI ANAYEKUSALITI
Wanaume wengi wanapobaini kuwa wapenzi wao
wanawasaliti, hutunisha
misuli kuonesha umwamba kwa kuwatwanga makonde
wapenzi wao au kuwafanyia mbaya wale waliowanasa. Lakini uchunguzi wa wana
mapenzi unaonesha kuwa
ubabe haukomeshi tabia ya usaliti. Kuna wengi ambao
waliwafumania wake zao, wakawapiga na kuwajeruhi,
lakini wakajikuta hawakukomesha tatizo, zaidi ya
kuwapa usugu wapenzi wao wa kuendeleza wizi tena kwa
dharau na kejeli.Katika hali ya kawaida usaliti ni
jambo linalouma kwa kiwango kikubwa. Katika mapenzi hakuna suala la kuazimana
mume/mke. Watu huazimana magari na pesa, lakini laazizi hakuna jasiri wa namna
hiyo! Hivyo ndivyo lakini, kupiga au
kuachana baada ya kufumaniana kunasaidia? Jibu
hakusaidii, kwani
ukimpiga adhabu inaishia hapo hapo, kesho yake
watakaokutana watakusaliti tena kupozana machungu.
Maamuzi ya kuacha naye hayasaidii kwani ukimwacha
mpenzi wako
hujamtibu, utakuwa umetoa mwanya wa yeye kuendelea
kukusaliti na
kukuumiza zaidi pale macho yako yatakapowaona
wameshikana mikono
mitaani kwa uhuru na raha zao. Ukiamua kuua na wewe
utauawa, huku wanadamu wenzako
wakikucheka kwa uzembe wa kufikiri. Jamani usaliti
upo kila siku, si tunawaona wake na wapenzi wa watu
wanaingizana gesti kila siku?
Hivyo, kama hujamfuma mpenzi wako leo kuna siku
utakutana na meseji kali akibembelezana na
‘kidume’ mwingine kwa maeneo fulani. Utafanyaje
baada ya kubaini hivyo, maana kama ni tukio basi
utakuwa umeona lile la stejini laivuuuuuu bila
chenga. Twende pamoja ili tuelimishane kama wadau
wa mapenzi njia sahihi ya kufanya ili kumwadhibu mpenzi
msaliti.
Kwanza, baada ya kuwaona uso kwa macho wakisaliti
penzi, unatakiwa kutoa ishara zitakazoonesha kuwa
umewaona, halafu ondoka eneo hilo. Ukifika home mtu
mzima endelea
kunywa maji ili kupoza presha. Akirudi mpenzi wako
jitahidi kumkaribisha
kwa bashasha, lakini usimuulize ulichoona mwache
aendelee kujiuliza
mwenyewe. Au kama umenasa meseji za kimahaba kutoka
kwa mwizi wako, zitume kwenye simu yako kwanza,
kisha baada ya kumaliza uchunguzi wako mtumie tena
sms hizo mkeo/
mumeo. Ukifanya hivyo usimuulize, endelea kumpenda
na ikiwezekana
ongeza matunzo. Nunua ‘mikuku’ akaange kila siku na
umpe penzi moto
moto. Nakwambia ukifanya hivyo mpenzi wako ataumia
sana na hataendelea kukusaliti kwa kuwa atakuwa anawaza
unafikiria kumfanya nini? Na kwa yule uliyemshika
naye, vivyo hivyo
usizozane naye, mwache! Utashangaa anahama eneo
maana atakuwa anafikiri unamwandalia kombora
kumbe wewe wala, umeamua kujituliza tu!
Wadau wa mapenzi hii ndiyo dawa ya mtu msaliti.
Mwadhibu kwa upole,
wanasaikolojia wameithibitisha
adhabu hii kuwa ina uchungu mara 1,000 zaidi ya
kupiga au kukemea.
Ukisema umwache siyo dawa kwani unaweza kutafuta
mwanamke/
mwanaume mwingine naye akawa na tabia zile zile,
ikiwa ndivyo utaacha
wangapi basi katika maisha haya? Adhabu ya mpenzi
anayekusaliti ni kumnasa kwenye usaliti wake kisha
kumpuuza huku wewe ukiendelea na mambo yako kama
kawaida, ukifanya hivyo utakuwa unamtibu ugonjwa wake wa kupenda penda hovyo na
hii
ndiyo dawa hasa ya kumponya msaliti, lakini pia
inasaidia kupunguza
maumivu ya penzi. Kumchunga na kumlilia machozi
hakusaidii.
0 comments:
Post a Comment