CHEKA UPATE AFYA::JEMSI MZEE WA MISIFA
Jamaa alianza kujisifu sana kazini kwake;
Jemsi : Wiki ijayo nafanya mtihani, ni miezi sita
sasa nafanya masomo ya jioni, nimejua mengi
sana, we unamjua David Livingstone?
Devi : Hapana simjui
Jemsi : Huyo ndie mzungu wa kwanza kuliona
Ziwa Victoria, ungekuwa unasoma masomo ya
jioni ungemjua huyu.
Jemsi akawa kero kazini kwa maswali yake.
Jemsi : We unamjua Graham Bell?
Devi : Hapana simjui
Jemsi : Huyo ndie alikuwa mtu wa kwanza
kutengeneza simu, ungekuwa unaenda kuchukua
masomo ya jioni ungemjua.
Siku moja Devi akamwita Jemsi;
Devi : Jemsi unamjua Hasani Makolokocho?
Jemsi : Hapana
Devi : Huyo ndie mchepuko wa mkeo kwa miezi
sita sasa, ungekuwa huendi kuchukua masomo
ya jioni ungemjua.
0 comments:
Post a Comment