Sunday, 1 June 2014

DAKIKA '100' TAIFA STARS WAIPEPERUSHA BENDERA YA TAIFA MJINI HARARE

10357474_634079413340945_8148690486284095511_n

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imejihakikishia nafasi ya kusonga mbele katika hatua inayofuata kusaka tiketi kucheza AFCON mwakani baada ya kutoa suluhu ya bao 2-2 na timu ya taifa ya Zimbabwe mjini Harare jioni hii.
Stars iliyohitaji sare yeyote ikiwa na faida ya ushindi wa goli moja iliyoupata Dar es salaam siku kadhaa zilizopita ilianza kwa kusua sua na kufungwa goli katika dakika kumi za mwanzo kupitia mchezaji Phiri D kabla ya team captain Nadir Haroub "Canavaro" kusawazisha dakika ya 21 na kufanya mchezo kuwa 1-1 hadi mapumziko.
Stars walirejea kwa kasi na kupata kuandika bao la pili kunako 46 kupitia kwa straika machachari Thomas Ulimwengu "Bufalo" kabla ya Zimbabwe kusawazisha dakika ya 55 kupitia Katsande W baadae.
Zimbabwe walicheza kwa kasi kuliendea lango la Stars lakini beki ilisimama imara na kuondoa hatari zote huku kipa Deogratius Munishi "Dida" akifanya kazi nzuri kulinda lango lake.
Pamoja na burudani ya soka mwamuzi alionesha kuibeba Zimbabwe lakini Tanzania walitulia na kufanya kile walicho tumwa na Taifa licha ya kucheza kwa dakika 100"MIA MOJA",,45+3 kipindi cha kwanza na 45+7 kipindi cha pili.
Stars imeitoa Zimbabwe kwa wastani wa mabao 3-2 na itakutana na Msumbiji,
Msumbiji walifuzu hatua hiyo kwa wastani wa mabao 5-0 baada ya juzi kutoka suluhu ya bila kufungana na Sudan Kusini Ugenini, wakati waliibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 mjini Maputo.
Msumbiji wana historia ya kuwaharibia Taifa stars katika michezo muhimu ya mashindano, hivyo ni jukumu la wachezaji na kocha Nooij kupanga mikakati kabambe ya kuwanyamazisha    `Mamba hao weusi`.
Mechi nyingine iliyomalizika jioni hii ni baina ya Lesotho na Liberia na kushuhudia Lesotho wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Huo ni mchezo wa pili wa kiushindani wa kocha Mart Noij tangu aanze kibarua chake mwezi uliopita na hajapoteza mchezo wowote hadi sasa.
KILA LA HERI TAIFA STARS
na KD MULA

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA