Monday 23 June 2014

NOMAA::MCHEPUKO WAMTOKEA PUANI HUYU JAMAA,,AOGESHWA HADHARANI NA KUPIGWA

AMA kweli duniani kuna vituko! Mkazi wa Mtaa wa Lagos, Wazo Mivumoni, Msitu wa Pande jijini Dar es Salaam, Nuru Makala ‘Baba Eliza’ (42) Jumatano iliyopita alikumbwa na majanga baada ya mwanaume aliyejulikana kwa jina la Yusuf Ally ‘Mgosi wa Ndima’ kudai amemfumania Baba Eliza akiwa na mkewe ambaye jina halikupatikana.
Mgoni, Nuru Makala ‘Baba Eliza’ (42) aliyefumaniwa akiwa na mke wa mtu (jina halikupatikana).

Tafrani hiyo ilijiri usiku wa Jumatano iliyopita, Juni 18, mwaka huu kwenye nyumba yake iliyopo Mtaa wa Lagos, Msitu wa Pande.
CHANZO
Usiku wa tukio, Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ilikuwa katika harakati za kusaka matukio katika Jiji la Dar, ndipo ilipokumbana na kelele za watu waliokuwa wakijibizana.
Ilibidi OFM itie timu kwenye nyumba hiyo na kukutana na chanzo kimoja kilichodai kuwa baba mwenye nyumba hiyo anadai kumfumania jirani yake na mkewe kitandani.
Mke wa Bw. Yusuf Ally ‘Mgosi wa Ndima’ akiondolewa eneo la tukio.
OFM YATINGA NDANI, YAKUTA MAKUBWA
OFM ilizama ndani ya nyumba hiyo na kukuta purukushani kali ikiendelea, Yusuf akiwa amepandwa na jazba ambapo katika kumkurupusha mgoni huyo alijigonga mahali na kuumia usoni.
MWENYE MKE AZUNGUMZA NA OFM
Baada ya mambo kutulia, OFM ilimuuliza Yusuf nini kilitokea mpaka kuwepo kwa tukio hilo, akafunguka:
“Nilikuwa katika harakati za kumchunguza mke wangu kinyemela kwa siku nyingi kama anachepuka, nikabaini kuna mawasiliano yenye shaka kati yake na huyo jirani yangu.
Mgoni akijisafisha uchafu mara baada ya fumanizi .
“Nilipomuuliza mke wangu alikiri, akasema amekuwa akimwambia jirani yangu kwamba haiwezekani lakini jamaa anakomaa tu anamwambia wakutane, tena wakutane humu ndani.
“Ndipo nilipoamua kumuandaa mke wangu kwa mtego amwambie jamaa kuwa leo (siku ya tukio) sitakuwepo na sitarudi ili kumpa nafasi jamaa kuja kujinafasi. Baada ya kukamilisha mtego niliwasiliana na kamanda wa sungusungu wa eneo hilo, Kapteni Makumba na kumuelezea kinagaubaga.”
...akivaa nguo.
MTEGO WAANDALIWA
“Kapteni Makumba aliwaandaa vijana wake ambapo kuanzia mishale ya saa mbili usiku walijibanza kwenye kichaka kilichopo mbele ya nyumba huku akifanya mawasiliano na mimi.”
JAMAA ATIA TIMU NA KIFURUSHI CHA MACHUNGWA
Yusuf aliendelea kudai kuwa, ilipotimu saa tano usiku kukiwa kumetulia, Baba Eliza alionekana akikaribia nyumba ya jirani yake huyo kwa hatua za kunyata na kuangalia kulia na kushoto kisha akazama ndani huku mkononi akiwa ameshika kifurushi kilichobainika baadaye kwamba kilikuwa na machungwa kadhaa.
...Mgoni akiomba msamaha.
Alisema muda mfupi baada ya kuingia, sungusungu mmoja alikwenda kujibanza kwenye dirisha la chumba na kupiga chabo kilichokuwa kikiendelea ambapo alimshuhudia Baba Eliza akichojoa nguo chapchapu tayari kwa mtanange, sungusungu huyo akawatonya wenzake.
SUNGUSUNGU WACHOMOKA KICHAKANI
Yusuf akazidi kusema kwamba wote walitoka kichakani na kwenda kuvamia chumbani ambapo walimkuta mkewe aliyekuwa bado hajaanza kuvua nguo kwa sababu alijua majanga yatatokea muda si mrefu akiwa anajiandaa kufanya hivyo kiaina.
...Timu ya Sungusungu iliyoandaliwa kufichua uovu uliokuwa ukiendelea ikimbana mtuhumiwa kwa maswali.
JAMAA AMPIGIA MAGOTI MWENYE MKE
Baada ya hali kuwa shwari, Kamanda wa Sungusungu, Kapteni Makumba alianza kumsomea mashitaka jirani huyo aliyekuwa mtupu muda huo mbaye hakuwa na la kusema zaidi ya kuomba radhi na kumtupia lawama ibilisi kwamba ndiye aliyemshawishi na haikuwa amri yake.
Ilibidi jamaa aniombe radhi, alisema jirani yangu niko chini ya miguu yako naomba unisamehe sitarudia tena hiki kitendo kwa kweli siyo amri yangu ni ibilisi tu ndiye aliyeniponza, nisamehe jirani yako nakupigia magoti unihurumie miye mkosefu,” alisema Yusuf akimkariri Baba Eliza.
...Raia aliyeshuhudia mkasa huo akionesha sehemu ya kitanda  iliyochafuliwa na mgoni kwa kinyesi.
APIGWA FAINI
Wakati OFM ikiwepo eneo hilo, sungusungu walimtaka Baba Eliza kumlipa fidia Mgosi wa Ndima kwa kitendo cha kumdhalilishia ndoa yake.
Mpaka OFM inaondoka eneo la tukio saa sita na ushee usiku, Baba Eliza alikuwa katika harakati za kumlipa fidia ya shilingi milioni moja mwenye mke.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA