Sunday, 1 June 2014

TAIFA STARS USO KWA USO NA ZIMBABWE LEO


 Taifa Stars walioripotiwa kufanyiwa hujuma hapo juzi kwa kufungiwa Hoteli wanayoishi mjini Harare,wanahitaji sare ya aina yoyote au ushindi ili kusonga mbele leo.Hii inatokana na ushindi wa bao 1-0 walioupata uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Lesotho waliofungwa bao 1-0 ugenini, watawakaribisha wapinzani wao Liberia katika mechi ya marudiano. Nao Botswana waliotoka suluhu mjini Bujumbura,leo watawakaribisha Burundi nyumbani kwao.
Congo yenye kumbukumbu ya kuchapwa bao 1-0 na Namibia,itakuwa nyumbani kulipa kisasi. Katika mechi nyingine,Benin waliotoka suluhu mechi ya kwanza, watakuwa nyumbani kuvaana na Sao Tome. Chadi waliofungwa mabao 2-0 na Malawi,leo hii watakuwa kwenye kibarua kigumu nyumbani kuhitaji kufuta matokoe hayo. Guinea ya Ikweta iliyofungwa bao 1-0 ugenini,leo nayo itahitaji ushindi nyumbani katika mechi ya marudiano na Mauritania.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA