LIGI KUU ENGLAND :LIVERPOOL WAICHAPA SOUTHAMPTON 2-1
LIVERPOOL imeanza vizuri maisha mapya ya ligi kuu soka nchini England bila ya Luis Suarez kwa kuifunga Southampton mabao 2-1 ndani ya dimba la Anfield jioni hii.Majogoo wa jiji ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 23 kupitia kwa kinda wake, Raheem Sterling kabla ya Nathaniel Clyne kuisawazishia Sounthampton katika dakika ya 56 kipindi cha pili.
Daniel Sturridge ndiye aliyeibuka shujaa katika mchezo wa leo baada ya kufunga bao la pili na la ushindi katika dakika ya 79.
Kitu kambani: Nathaniel Clyne akiisawazishia Southampton bao
Rickie Lambert alitokea benchi na kuchukua nafasi ya Philippe Coutinho, hivyo kucheza mechi yake ya kwanza ya ligi kuu akiwa na Majogoo.
Pia Brendan Rodgers alimuanzisha Lucas Leiva katika safu ya kiungo.
Nyota wa zamani wa Liverpool, Adam Lallana aliikosa mechi ya ufunguzi kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.
Msimu uliopita Liverpool walishika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu nyuma ya mabingwa Manchester City.
Kinda mkali: Raheem Sterling akiandika bao la kuongoza.
Baada ya kuona washindi hao wa pili wakianza kwa ushindi, sasa mechi ya Manchester City dhidi ya Newcastle United inayopigwa leo imevuta hisia za mashabiki wakiwa na hamu ya kuona nini kikosi cha Manuel Pellegrini kitafanya ugenini.
Kikosi cha Liverpool: Mignolet, Manquillo, Skrtel, Lovren, Johnson, Henderson, Gerrard, Lucas (Allen 63), Sterling, Coutinho (Lambert 76), Sturridge.
Wachezaji wa akiba: Brad Jones, Toure, Sakho, Can, Ibe.
Wafungaji wa magoli: Sterling 23, Sturridge 79.
Kadi ya njano: Manquillo.
Kikosi cha Southampton: Forster, Clyne, Fonte, Yoshida, Bertrand, Wanyama, Schneiderlin, Tadic (Long 74), Ward-Prowse, Steven Davis (Isgrove 82), Pelle.
Wachezaji wa akiba: Kelvin Davis, Taider, Cork, Hooiveld, Stephens.
Mfungaji wa goli: Clyne 56.
Kadi ya njano: Schneiderlin, Steven Davis.
Mwamuzi: Mark Clattenburg (Tyne & Wear)
0 comments:
Post a Comment