Showing posts with label SPORT MAJUU. Show all posts
Showing posts with label SPORT MAJUU. Show all posts

Tuesday, 22 August 2017

ROONEY AWEKA HISTORIA KWA KUFUNGA GOLI LA 200 EPL

Wayne Rooney ameandika historia kwa kuweka rekodi baada ya kufunga goli lake la 200 katika  Ligi Kuu ya Uingereza huku Raheem Sterling akifunga bao lililoiokoa Manchester City iliyobakia na wachezaji 10 na kuinyima Everton ushindi katika uwanja wa Etihad.

Manchester City walijikuta na kibarua kigumu baada ya Rooney kufunga goli na baada ya Kyle Walker kutolewa nje kwa kadi mbili za njano za haraka ndani ya dakika 44.

Kikosi hicho kinachonolewa na Pep Guardiola hakikuamini matokeo hayo na kilipambana mnono na kufanikiwa kuepuka kipigo cha pili nyumbani wakiwa chini ya Mhispania huyo.
   Mpira uliopigwa na Wayne Rooney ukiwa umempita tobo kipa wa Manchester City na kuandika goli 

   Raheem Sterling akiachia shuti na kuisawazishia Manchester City goli na kufanya matokeo kuwa 1-1

Friday, 12 May 2017

EUROPA::MAN UNITED YATINGA FAINALI SASA USO KWA USO NA AJAX

Manchester United imenusurika tishio la dakika za mwisho na kuwatoa wageni Celta Vigo na kufanikiwa kukata tiketi ya kutinga fainali ya Ligi ya Uropa dhidi ya Ajax.

Ikiongoza kwa goli 1-0 katika mchezo wa kwanza, United ilianza kwa kuumiliki mchezo wa jana na kufunga goli la kichwa kupitia kwa Marouane Fellaini kupitia pande la Marcus Rashford.

Lakini Celta, iliyokuwa ikihitaji kufunga magoli mawili, ilisawazisha goli hilo kupitia kwa mchezaji wao Facundo Roncaglia na kuufanya mchezo huo kwa wa roho juu.

Katika mchezo huo mchezaji wa Manchester United Eric Bailly na Roncaglia walitolewa nje kwa kupigana huku wenyeji wakigangamala na kutinga fainali.
                                              Marouane Fellaini akifunga goli kwa mpira wa kichwa
             Mpira uliopigwa na mchezaji Facundo Roncaglia ukiwa umetinga wavuni

                              Fellaini akimzuia Eric Bailly aliyempiga ngumi John Guidetti

EUROPA:: LICHA YA KUFUNGWA UGENINI,AJAX YATINGA FAINALI


Timu ya Ajax imejikuta ikipata wakati mgumu baada ya Lyon kutaka kulipa kisasi nchini Ufaransa katika kujaribu kutinga fainali ya Ligi ya Uropa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1996.

Katika mchezo wa jana Ajax ilipata goli la kwanza kupitia kwa Kasper Dolberg na kufanya matokeo ya jumla kuwa magoli 5-1.

Lakini Alexandre Lacazette aliifungia Lyon magoli mawili kabla ya kumalizika kipindi cha kwanza na kisha Rachid Ghezzal kufunga goli la tatu katika dakika ya 81.
                                     Alexandre Lacazette akichezewa rafu katika eneo la penati

               Alexandre Lacazette akiwa ameubeba mpira baada ya kufunga kiufundi penati

Sunday, 30 April 2017

LA LIGA::BARCELONA YAZIDI KUPIGANA VITA KALI KUWANIA UBINGWA

Timu ya Barcelona imeendelea kukaa kileleni mwa ligi ya La Liga wakati Luis Suarez akifunga mara mbili na kuihakikishia ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Espanyol.

Uzembe wa Jose Manuel Jurado kupiga pasi ya nyuma iliyomkuta Suarez, aliyeachia shuti lililompita kipa Diego Lopez, uliifanya Barcelona kupata goli la kwanza.

Ivan Rakitic aliongeza goli la pili kwa Barcelona kabla ya Suarez tena kutumia vyema makosa ya Espanyol kufunga goli la tatu.
    Luis Suarez akiuwahi mpira wa pasi mbovu ya nyuma ya  Jose Manuel Jurado na kufunga goli

Saturday, 29 April 2017

LA LIGA:: MARCELO AIBEBA REAL MADRID NYAKATI ZA JIONI, RONADO AZIDI KUWEKA REKODI

Real Madrid imefungwa goli la dakika za mwisho na kufanikiwa kuifunga Valencia kwa magoli 2-1 katika hatua muhimu ya kuwania taji la Ligi ya Hispania ya La Liga.

Katika mchezo huo Cristiano Ronaldo aliifungia Real, goli la kwanza na kumfanya kuwa mfungaji anayeongoza kufunga magoli mengi katika ligi tano za juu Ulaya.

Katika mchezo huo ambao Ronaldo alikosa penati, Valencia walisawazisha goli kupitia kwa Dani Parejo dakika ya 82, kisha baadaye Marcelo akafunga goli la ushindi kwa Real.
   Cristiano Ronaldo akiruka juu na kuupiga mpira kwa kichwa na kufunga goli la kwanza
   Dani Parejo akipiga mpira wa adhabu uliopaa juu ya ukuta wa Real na kufunga goli

Friday, 21 April 2017

EUROPA:: CELTA VIGO YAFUZU HATUA YA NUSU FAINALI ,GENK YA SAMATTA YAKWAMA


Celta Vigo imetinga nusu fainali ya Ligi ya Uropa na kuitoa timu ya Mbwana Samatta ya Genk kwa ushindi wa magoli ya jumla 4-1, baada ya jana kutoka sare ya 1-1.

Celta Vigo ilikuwa ishapata ushindi wa magoli 3-2 katika mchezo wa awali dhidi ya Genk na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.

Katika mchezo wa jana Pione Sisto alikuwa wa kwanza kuifungia goli Celta Vigo katika dakika ya 63 lakini Leandro Trossard alisawazisha dakika nne baadaye.
                     Pione Sisto akiachia shuti na kuifungia Celta Vigo goli katika mchezo huo
Leandro Trossard akishangilia baada ya kuifungia Genk goli la kusawazisha huku Mbwana Samatta akiangalia

Thursday, 20 April 2017

UEFA::JUVENTUS YAZIMA NDOTO ZA BARCELONA KUTINGA NUSU FAINALI


Timu ya Juventus imeweza kucheza mpira safi wa kujihami na kufanikiwa kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuilazimisha sare tasa Barcelona katika dimba la Nou Camp.

Ikiwa ishafungwa 3-0 katika mchezo wa awali, Barcelona ilishindwa kufanya miujiza iliyoifanya katika hatua ya 16 bora baada ya kuitoa Paris St-Germain licha ya kufunga 4-0 katika mchezo wa awali.

Lionel Messi, ambaye awali awali alinyimwa goli na kipa Gianluigi Buffon, alipiga mashuti kadhaa yaliyopotea kwa kutoka njea huku Luis Suarez na Neymar walipoteza nafasi za kufunga usiku wa jana.
                                     Lionel Messi akiangukia uso baada ya kukabiliana na Pjanic 
             Neymar akibembelezwa na mchezaji mwenzake wa zamani wa Barcelona Dani Alves

UEFA::MONACO YAINDOA BORUSSIA DORTMUND NA KUTINGA NUSU FAINALI


Monaco imetinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza 2004, baada ya kucheza mchezo safi wa marudiano dhidi ya Borussia Dortmund na kuibuka na ushindi wa magoli 3-1.

Monaco ikiwa na matokeo ya magoli 3-2 katika mchezo wa kwanza, ilipata goli lake la kwanza kupitia kwa kinda Kylian Mbappe na kisha baadaye Radamel Falcao akaongeza goli la pili.

Dortmund ilimuingiza mshambuliaji wake Ousmane Dembele na ilikuwa jitihada za mchezaji huyo mwenye miaka 19 zilizomfanya Marco Reus kufunga goli kabla ya Valere Germain kutupia la tatu.
                            Kinda Kylian Mbappe akifunga goli la kwanza katika mchezo huo 
                       Radamel Falcao akiifungia Monaco goli la pili kwa mpira wa kichwa

Wednesday, 15 March 2017

UEFA::LEICESTER CITY YAFUZU HATUA YA ROBO FAINALI


Leicester City imeandika ukurasa mwingine katika historia ya soka klabuni hapo  baada ya kubadili matokeo ya kufungwa katika mchezo wa kwanza kwa kufanikiwa kuifunga Sevilla magoli 2-0 na kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Leicester ilionekana kama itatolewa baada ya kufungwa magoli 2-1 Hispania katika mchezo wa kwanza na kutimuliwa kocha wao Claudio Ranieri, ambaye aliiongoza hadi kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa mara ya kwanza.

Ikiwa chini ya kocha wa muda Craig Shakespeare, Leicester imebadilika na ilikuwa katika kiwango kizuri jana ambapo nahodha wao Wes Morgan aliipatia goli la kwanza katika kipindi cha kwanza na kisha baadaye Marc Albrighton kufunga la pili.
                                         Beki Wes Brown akifunga goli la kwanza la Leicester City 

                                    Marc Albrighton akifunga goli la pili na kuizamisha Sevilla

Thursday, 2 February 2017

MANCHESTER CITY YAPATA USHINDI MNONO DHIDI YA WESTHAM UGENINI

Mchezaji Gabriel Jesus amefunga goli lake la kwanza akiwa na Manchester City wakati wakiichakaza West Ham 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza katika dimba la London.



Manchester City, ambao walimuacha mshambuliaji wa Sergio Aguero na kipa Claudio Bravo akiwa benchi walipata goli la kuongoza kupitia kwa Kevin de Bruyne baada ya kugongeana vyema na Jesus.



Dakika nne baadaye Leroy Sane aliwapita mabeki wawili na krosi yake iliyobabatizwa ikamkuta David Silva na kufunga goli. Raheeem Sterling alimtengenezea goli Jesus na Yaya Toure akafunga goli la nne kwa mkwaju wa penati katika kipindi cha pili.
                                     Kevin de Bruyne akifunga goli la kwanza la Manchester City

HULL CITY YAIZUIA MANCHESTER UNITED OLD TRAFFORD

Kipa Eldin Jakupovic ameokoa magoli kadhaa wakati Hull City ikiichanganya Manchester United kwa kufanikiwa kutoka sare tasa katika mchezo wa Ligi Kuu kwenye dimba la Old Trafford.

Wenyeji Manchester United walishinda kabisa kupata ujanja wa kutumbukiza mpira kumpita kipa wa Hull, ambaye alizuia kiufundi shuti la mbali la Zlatan Ibrahimovic na jitihada za shambulizi la Paul Pogba katika kipindi cha kwanza.

Kwa matokeo hayo Manchester United wanabakia katika nafasi ya sita, lakini yameisaidia Hull City kujikwamua kutoka chini kwenye msimamo.
                        Zlatan Ibrahimovic akijipinda kuachia shuti akijaribu kutafuta goli 
                                         Marcus Rashford akijaribu bila ya mafanikio kulenga goli

Thursday, 26 January 2017

SOUTHAMPTON YAFUZU FAINALI KOMBE LA EFL KWA KUIFUNGA LIVERPOOL


Southampton imeitoa Liverpool katika michuano ya kombe la EFL na kutinga nusu fainali ya michuano hiyo kwa kuifunga goli 1-0, na kuifanya kuibuka na ushindi wa jumla ya magoli 2-0.



Southampton walishuka katika mchezo huo wakiwa tayari wanaongoza kwa goli moja la mchezo wa awali lililofungwa na Nathan Redmond katika dimba la St Mary.




Katika mchezo huo Daniel Sturridge alikosa nafasi mbili za kufunga na kupaisha mpira juu huku Fraser Forster akifanikiwa kuokoa mpira uliopigwa Emre Can.



Goli la Southampton lilifungwa na Shane Long baada ya kufanyika shambulizi la kasi katika dakika za mwisho.

                                  Mshambuliaji Daniel Sturridge akipaisha juu mpira na kukosa goli 
        Kipa Fraser Forster akifanya kazi ya ziada kuokoa mpira uliopigwa na Emre Can 

Tuesday, 10 January 2017

CRISTIANO RONALDO ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA WA FIFA


Mshambuliaji nyota Cristiano Ronaldo ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka, na kupewa tuzo na Shirikisho la Soka Duniani- FIFA Jijini Zurich.

Nyota huyo wa Real Madrid na Ureno Ronaldo, 31, alimshinda mchezaji wa Barcelona, Lionel Messi na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid.

Ronaldo pia alishinda tuzo ya Ballon d'Or Desemba 2016, ambapo tuzo zote hizo ametwaa kutokana na mafanikio katika Ligi ya Mabingwa na Real, pamoja na Euro 2016 na Ureno.
                                          Mshambuliaji nyota Cristiano Ronaldo akibusu tuzo yake
Cristiano Ronaldo akiwa amemshika mtoto wake wa kiume katika picha ya pamoja na familia yake

Monday, 9 January 2017

CHELSEA YATINGA RAUNDI YA NNE YA KOMBE LA FA

Kapteni wa Chelsea, John Terry ametolewa nje kwa kadi nyekundu wakati timu hiyo ikiibuka na ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya timu ya ligi ya daraja la kwanza ya Peterborough katika mchezo wa kombe la FA.

Katika mchezo huo Chelsea ilifanya mabadiliko ya wachezaji tisa, na nusura wajikute wakiwa nyuma baada ya Asmir Begovic kuokoa mpira wa kichwa cha karibu uliopigwa na Lee Angol.

Hata hivyo kikosi hicho cha Antonio Conte, kilipata goli la kwanza kupitia kwa Pedro, kisha Michy Batshuayi kufunga la pili na Willian kufunga la tatu baada ya mapumziko kabla ya Pedro.
Pedro akiwa ameachia shuti lililojaa wavuni na kuandika goli la kwanza katika mchezo huo
Tom Nicholas akiangali mpira alioupiga ukielekea kutinga kwenye goli la Chelsea

KOMBE LA FA : LIVERPOOL YABANWA NA PLYMOUTH

Kikosi cha vijana wa Liverpool kimejikuta kikidhibitiwa na kutoa sare tasa na timu ya daraja la pili ya Plymouth Argyle katika mchezo wa raundi ya tatu wa kombe la FA katika dimba la Anfield hii leo.

Wenyeji Liverpool ambao wachezaji wake walikuwa na wastani wa miaka 21, walimiliki mpira kwa asilimia 80.3 katika kipindi cha kwanza huku Sheyi Ojo akishindwa kutumia nafasi nzuri kufunga.

Katika mchezo huo Divock Origi pia goli lake lilikataliwa kutokana na kumchezea rafu Gary Miller, kabla ya kocha Jurgen Klopp kuamua kuingiza kikosi cha kwanza cha kawaida cha kina Daniel Sturridge, Adam Lallana na Roberto Firmino.
                                                            Mpira uliopigwa na Sheyi Ojo ukidakwa na kipa 
                                  Jitihada za Divock Origi zikigonga ukuta wa timu ya Plymouth 

LIONEL MESSI AIOKOA BARCELONA NA KIPIGO DHIDI YA VILAREAL

Lionel Messi ameiokoa Barcelona isipate kichapo kupitia mkwaju wa adhabu wa dakika za mwisho na kuinyima Villarreal ushindi katika mchezo wa La Liga jana.

Nicola Sansone aliwapatia wenyeji goli la kuongoza kwa shuti la chini akipokea pasi ya mchezaji wa zamani wa Chelsea, Alexandre Pato.

Katika mchezo huo shuti la Messi liligonga mwamba na Barcelona walinyimwa penati pale Bruno aliposhika mpira wa shuti la Messi.

Kwa matokeo hayo ya goli 1-1 Barcelona inabakia katika nafasi ya tatu, ikiwa nyuma ya vinara Real Madrid kwa tofauti ya pointi tano.
                       Lionel Messi akipiga mpira wa adhabu katika dakika ya 90 na kuzaa goli
                                Kiungo Sergio Basquets akimfanyia madhambi Alexandre Pato

ZAHA AISAIDIA IVORY COAST KUPATA USHINDI DHIDI YA SWEDEN


Wilfried Zaha ametokea benchi na kuisaidia Ivory Coast, kupata ushindi kwa kuifunga Sweden magoli 2-1 katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na Kombe la Mataifa ya Afrika.

Baada ya kutoswa na makocha Roy Hodgson na Sam Allardyce, pamoja na Gareth Southgate, katika timu ya taifa ya Uingereza Zaha ameamua kuichezea nchi yake aliyozaliwa ya Ivory Coast.
Ivory Coast

Akicheza kwa mara ya kwanza na Ivory Coast mchezaji huyo wa kimataifa aliingia dimbani baada ya mapumziko Zaha, alitoa pande kwa Giovanni Sio aliyefunga goli la pili.
                                       Wilfried Zaha akielekea kupiga krosi iliyozaa goli la ushindi

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA