CHEKI HAPA MPIGHA DEBE ALIVYO VUNJA REKODI YA MWAKA KWA KUWA'SUPRISE' WATOTO YATIMA
07:29 |
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mpigadebe maarufu katika kituo cha mabasi cha mbalizi wilayani mbeya amenunua mbuzi wawili na bidhaa nyingine za aina mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja na kuzipeleka kwenye vituo vya watoto yatima kama zawadi huku akiwaasa watoto hao kutoshawishika kwenda kupiga debe kwenye vituo vya mabasi.
Mpigadebe maarufu katika kituo cha mabasi cha mbalizi, Anganile Mwamuluma Andrea ambaye amefanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 20 ameushangaza umma wa wakazi wa mbeya baada ya kuamua kununua mbuzi wawili, mchele, maharagwe, sabuni, mafuta ya kupikia na mahindi na kupeleka bidhaa hizo katika vituo viwili vya watoto yatima ambako amezitoa kama zawadi kwa watoto hao, huku akiwaasa kutoshawishika kujihusisha na kazi ya kupiga Debe kwenye vituo vya mabasi.
Walimu wa watoto hao wameeleza kushtushwa na kitendo cha mpigadebe huyo, lakini wakasema kuwa ni mfano Bora wa kuigwa kwa vijana wanaofanikiwa kukumbuka mazingira walikotoka, huku wakiwahimiza wazazi kuongeza upendo kwa watoto wao ili kupunguza wimbi la watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini.
Baadhi ya watoto ambao wamepokea msaada huo, wamemshukuru mpigadebe huyo na kuwataka watu wengine kupata funzo la kuthamini na kuwapenda watoto ikiwa ni pamoja na kuwaandalia mazingira mazuri ya kujitegemea.
-ITV