Thursday, 16 October 2014

HATARI...POLISI WAKAMATA ZANA ZA MILIPUKO HUKO TANGA, ZILIKUWA ZIKITOKEA NIGERIA


Jeshi la Polisi mkoani Tanga limewakamata kisha kuwatia mbaroni raia wawili wa kigeni kutoka Nigeria wakiwa na zana za milipuko inayotumiwa katika vitendo vya kigaidi.

Kamanda wa Polisi mkoani Tanga kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Fraisser Kashai amesema watuhimiwa hao waliotambulika kwa majina ya Kenneth Ekeneh Luodo na Amick Bonniface Aje ambao wamekamatwa katika kijiji cha kigwasi kilichopo kata ya mashewa wilayani Korogwe ambapo walikutwa kwa mwenyeji wao aliyetambulika kwa jina la Frank ambaye alitoroka baada ya operesheni hiyo.
 
Amesema zana hizo ambazo pia hutumika kuvunja miamba na majengo watuhumiwa walikuwa wamezihifadhi katika mabegi ndipo jeshi la Polisi walipowakamata na kuwatia mbaroni kwa ajili ya upelelezi zaidi huku jitihada za kumtafuta mwenyeji wao Frank zikiendelea.
 
Katika tukio lingine kamanda Kashai amesema mtu mmoja Michael Charle amekamatwa akiwa na risasi 39 za silaha za kivita ambazo anadai kuwa anafanya biashara ya kuuza risasi kinyume cha taratibu ambazo amedai kuwa ametoka nazo Monduli mkoani Arusha kwenda mkoani Morogoro.
 
CHANZO:ITV

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA