Friday 24 October 2014

MAREHEMU SHERY MAGARI AZIKWA :MZEE MAGARI AINGIA MITINI: CHEKI PICHA HAPA

Marehemu Sherry enzi za Uhai wake.

Umati wawatu uliofulika kanisani hapo


Na Dustan Shekidele,Morogoro.
MSIBA wa msanii Sherry Choka,maarufu Sherry Magali umetawaliwa na vituko kibao,baba mzazi mzee Salim Choka na baba wa hiyari mzee Charles Magali waingia mitini mziba wa mtoto wao Mama mzazi Afande Flora Msiba awatosa wazazi hao na kuamuakuandika jina la baba yake Mzee Msiba Edward kwenye Msalaba wa mpendwa mtoto wake. 
Mama wa marehemu, Afande Flora akisaidiwa kutoka kanisani 

Kama kawa baada ya vituko hivyo Mwandishi wa mtandao huu alimtafuta msemaji wa familia hiyo Kulwa Choka ambapo alikiri kuwepo kwa vituko hivyo.
 Msanii Tausi akimuaga msanii mwenzake  kwa uchungu

” Nikweli baba yetu mzee Choka yuko Tunduma hakuweza kufika kwenye msiba wa mwanae na kwamba amepiga simu nakumpa madalaka yote babu yetu mzee Msafiri Ngedele ndio maana unaona msiba uko hapa  Mji Mpya nyumbani kwa mzee huyo, pia huyo mzee Magali ambaye watu wanadai ni baba yake Sherry pia hakufika msibani"alisema Kulwa kwa Jazba na kuongeza kusema
 Mwili wa marehemu Sherry ukitolewa kanisani baada ya lbada kumuombea kukamilika
"kuhusu jina la kwenye msalaba tumekuwa na mvutano wa takribani masaa 4 kwenye kikao mama wa marehemu alitushangaza kuacha jina la baba wa marehemu mzee Choka na kung’ang’ania kuandika msalaba jina la baba yake mzee Msiba  Edward ambaye ni babu wa dada yangu sherry kwa upande wa mama yake,tumeona tusiwape watu faida tumekubali lakini undani zaidi wa matukio hayo tutakujuza baada ya kumaliza msiba huu”alisema Kubwa Choka ambaye amechangia baba na marehemu Sherry. 

Juhudi za Mtandao huu za kutaka kuzungumza na Mama mzazi wa Sherry Afande Flora Msiba zilikwama baada ya mama huyo muda wote kuangulia kilio kwa kuondokewa na mpendwa mtoto wake juhuzi hizo zinaendele leo na kesho,Pia juhuzi za Mwandishi wetu kumhoji mzee Choka kwa njia ya simu zinaendele, 

Pekuapekua ya Mtandao huu imefanikiwakumbana mmoja wa wasanii nyota wa bongo Movie kutoka Dar ambapo alipoulizwa kwa nini mzee Mgali hakufika kwenye msiba wa Sherry alisema” Nikweli mzee magari hakufika kwenye msiba wa Sherry yuko Mwanza kwenye shughuli za kisanii”alisema msanii huyo  aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Picha na habair kwa hisani ya Shekidele Blog

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA