Mitandao ya kijamii inavyochangia kuharibu mahusiano ya kimapenzi na kuvunja ndoa….
Bila shaka kila mmoja anahamu ya kujua kwanini nimeamua kuzungumzia mitandao ya kijamii, inawezekana wewe ni miongoni mwa waliyoathiriwa na tatizo hili.
Mitandao inazidi kuongezeka kadri siku zinavyokwenda na kila mmoja anashauku ya kujiunga na mtandao mpya hasa kwa wale wenye simu zenye uwezo wa kufungua mitandao hiyo.
Wakati mwingine tunashauriwa kuwa na kiasi kwa kila jambo, ili tusilemewe, wengi wamelemewa na hata kujisahau kwa kutumia mitandao hiyo, kwa mambo yanayoichefua jamii na hata kuvunja maadili.
Mfano utamkuta mtu anakutumia picha ya mtu akiwa utupu kwenye whatsapp, facebook, Instagram, twitter, tango, viber na mingine bila kujali uhusiano wake kwako au umri wake na wako wakati mwingine sijui ni kukosa adabu.
Lakini unajiuliza lengo la huyo mtu kukutumia picha hiyo ni nini, na wengine wanakesha kwenye mitandao hiyo wakiwa wanachart na watu wasiyowafahamu, na kuwatumia picha za mikao mbalimbali pamoja na ujumbe wa sauti.
Mahusiano mengi sasa yamekuwa katika wakati mgumu baada ya baadhi yao kujiingiza kwenye hiyo mitandao na kujiachia na watu wasiywafahamu vema, na kupokea ujumbe wa aina mbalimbali.
Mwanamke mmoja alinisimulia mkasa uliyokuta baada ya kuwa na maongezi na mchumba wake wakati wakiwa katika maongezi jamaa alikuwa busy akichart na wanawake tofauti.
Mwanamke yule alikereka sana na hali hiyo na kuamua kupokonya simu ile ili kujua kulikono? Baada ya kupokonya alikutana na haya: mpenzi wangu uko wapi?
nipo kitandani nimepumzika nakuwaza wewe malaika wangu?
Lakini unaniita malaika wakati hata hatujaonana? Unavyongea tu mimi hoi, natamani ungekuwepo hapa!!!!!
Usijali we nitumie usafiri nije nikupe mambo?
Utaniua mtoto wa watu…..jamani wewe….. haya nipigie…. Aaa tuendelee kuchati baby.
Mwanamke wa pili sasa kesho jitahidi tuwe wote baby.
Wala usijali niko kwa ajili yako hata leo ungetaka ningekuja,,,, kwani bado uko kazini? Ndiyo lakini bado kidogo nitatoka hapa….. ningekuwa sijachoka ningekupitia tukapumzike wote…
Jamani fanya hivyo basi mbona unanirusha roho sana wakati unajua navyokupenda.
Mme wa mtu akichart na kimada jamani wewe mtoto mzuri uko wapi leo nataka tukapumzike wote…
Leo baba yuko ila kesho kila kitu kitakaa sawa wala usijali..lazima nijali inamaana ujua huyu mwanamke wangu nimeshamchoka sasa wewe, hutaki kuziba pengo hili.
Nakuja ila unakumbuka nilikwambia kodi yangu inaishia mwezi huu, na mtoto wa dada anadaiwa ada, na uliniambia utaninunulia gallax 4 sasa nahamu nayo kweli..
Hayo ni mambo madogo sana ingawa mke wangu anatumia simu ya tochi lazima nikufurahishe ila kodi huyu bibie amechukua ATM yangu sasa kuitoa kazi kwelikweli, ila si unajua mimi ni wako mpenzi….
Haya my honey nakusubiria kwa hamu kwa kweli maana mashoga zangu watanitangaza lazima mwaka huu nimeshawaambia wakanitangaze niko na mtu wa nguvu lakini jamani waume za watu mnajua kuhonga.
Huu ndiyo Ukweli wa mawasiliano yanayofanyika katika mitandao mingi ya kijamii watu wengi akiwemo wewe unayesoma makala hii inawezekana ndiyo tabia yako.
Lakini kumbuka hakuna kilichokuwa na mwanzo kikakosa kuwa na mwisho hizi ni nyakati za mwisho wewe uko upande gani?
Unadhani michepuko kwenye mitandao ni dili au upumbavu? Neno la Mungu linasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
Baki njia kuu kwa kumpenda, kumweshimu, mkumjali huyo uliye naye katika mahusiano ya kimapenzi, kumbuka maamuzi yako ya leo ndiyo matokeo yako ya kesho.