RAIS PUTIN AKAMILISHA MADAI YA TALAKA YA MKEWE
RAIS wa Urusi amekamilisha madai ya talaka kutoka kwa mkewe waliyeishi naye kwa miaka 30, Lyudmila Aleksandrovna Putina baada ya kutengana kwao, majira ya joto mwaka jana.
Wasifu wa Putin uliotolewa hivi karibuni unaonesha ana watoto wawili bila kutajwa kwa jina la mke wa rais (fisrt lady).
Msemaji wa Rais huyo, Dmitry Peskov amethibitisha kukamilika kwa talaka hiyo katika chombo cha habari kinachomilikiwa na serikali hiyo cha Itar-TASS.
Katika hali iliyowashtua wengi, Juni mwaka jana, Putin alitangaza kuachana na mkewe huyo baada ya kudumu katika ndoa yao kwa miaka 30.
Baada ya hapo Lyudmila Putina hakuonekana tena kwenye hadhara za kiserikali, huku watoto wake wawili nao wakiwa hawaonekani hadharani.
Maisha binafsi ya Putin (61) yamezua uvumi nchini humo, huku akihusishwa kuwa na mahusiano na mwanamichezo Alina Kabayeva.
Hata hivyo uvumi huo ulikanushwa na chombo cha habari kilichotoa taarifa hiyo kilifungiwa mwaka 2008.
na matukio blg
0 comments:
Post a Comment