Saturday 1 November 2014

WANAFUNZI ARUSHA WAKUTANA NA KUONESHA VIPAJI VYAO ILIKUWA POUWA SANA:CHEKI PICHA

wanafunzi wakishandana kucheza muziki
Story na KD MULA.
Leo wanafunzi kutoka shule na Vyuo mbalimbali jijini Arusha wamekutana katika Tamasha la ARUSHA STUDENTS DAY CONCERT katika uwanja wa Kumbu kumbu ya Sheihk Amri Abeid Arusha na kunesha vipaji vyao pamoja na kuburudika.
baadhi ya wanafunzi waliohudhuria tamasha hilo




Akizungumza na muandishi wetu Mkurugenzi wa kampuni ya OSG Entertainment iliyoandaa Tamasha hilo Ndugu Isack Challo amesema waliamua kuja na wazo hili ikiwa na lengo la kuwaleta pamoja wanafunzi ndani na nje ya jiji ili kuleta umoja.


"Lengo letu hasa ilikuwa ni kuwaleta wanafunzi pamoja waweze kuonesha vipaji vyao pia kupata burudani kwa kuwa wanatakiwa kufamiana na kupanua uwezo wao wa kufikiri kwani mashindano ya vipaji yatawapa changamoto" alisema bwana Challo.
Mambo Jambo Acrobats wakifanya yao

Katika tamasha hilo lilioanza saa nne asubuhi na kuisha saa kumi na mbili jioni wanafunzi walipata nafasi ya kushindana kwa kucheza muziki,kuimba na kukimbia ambapo washindi katika michezo hii waliweza kujipatia zawadi zao.
Young Omega akitoa burudani
Miongoni mwa shule zilizoshiriki nakuweza kupewa vyeti vya ushiriki ni Olasiti sekondari,Olorieni sekondari,Enaboishu sekondari,Royal Green Valley sekondari,Felix Mrema,Moshono sekondari,Momesco collage na nyingine nyingi.
Chidi-bero kijana aliyevutia wengi kutokana na kipaji chake

Wakilizungumzia tamasha hili baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika tamasha hilo walionesha kufurahishwa na burudani zilizokuwa zikitolewa uwanjani hapo.
Dogo wa mambo jambo acrobats wakifanya yake

Sambamba na hilo vikundi mbali mbali vya sanaa vilitoa burudani ikiwemo Mambo Jambo Acrobatics,KGT Dancers,Agesta pamoja na wasanii kama Young Omega,Kitila Boy,Jos D,Dipper,Abamto,Alvin,John Rogers pamoja na wengine wengi lakini hata hivyo kwa upande wa wasanii ni Young Omega pekee ndiye aliyefanikiwa kupanda stejini huku wengine wakiutupia lawama uongozi wa OSG Entertainment kwa kutopangilia vyema ratiba.
Tutakujuza ni kipi hasa kiini cha kwanini mastaa hawa hawakupanda stejini.
Dipper muda mfupi mara baada ya kuwasili uwanjani

Tamasha hili lilikuwa chini ya udhamini wa SBC CoLTD,Radio 5 Sambamba na Milan Cable Television waliokuwa wakichukua matukio mbali mbali yaliyojiri.
Jos D na crew yake  tayari kwa show 


Hili ni miongoni mwa matasha  tamasha machache kujumuisha wanafunzi toka shule mbali yaliyowahi kufanyika jijini Arusha.



OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA