Sunday, 2 November 2014

SERIKALI YAGOMA KUSITISHA MAFUNZO YA JKT KWA WALIMU

TARIME:
SERIKALI IMESEMA KUWA HAITASITISHA MAFUNZO YA JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) KWA WALIMU KWAKUWA MAFUNZO HAYO YANAWAJENGEA WALIMU UKAKAMAVU, NIDHAMU NA KUJUA SHUGHULI MBALIMBALI ZA UZALISHAJI ZIKIWAMO ZA KILIMO.

AKIJIBU SWALI LA JOVENAL THOMAS AIRO MMOJA KATI YA WANAFUNZI WA CHUO CHA UALIMU TARIME NDANI YA UKUMBI WA CHUONI LILILOHOJI KUNA MANUFAA GANI MWALIMU KWENDA JKT ? KWA MADAI KUWA MPANGO HUO HAUNA MANUFAA ZAIDI YA WALIMU KUFARIKI WAKIWA JKT KUTOKANA NA MATATIZO YA KIAFYA,



WAZIRI WA ELIMU NA UFUNDI SHUKURU KAWAMBWA AMESEMA KUWA MPANGO HUO NI MZURI KWA MADAI KUWA HATA MIKA YA NYUMA WALIMU WALIKWENDA JKT BAADA YA KUHITIMU MAFUNZO YA CHUO CHA UALIMU.

KAWAMBWA AMESEMA KUWA MAFUNZO NI MIEZI 3 TOFAUTI NA MIAKA YA NYUMA AMBAYO YALITOLEWA KWA MUDA WA MWAKA MMOJA HIVYO ANASHANGAA KUONA BAADHI YA WANAFUNZI WAKIOGOMA NA KUHOFIA MAZOEZI YA JKT.

WAZIRI HUYO AMEONGEZA KUSEMA KUWA ZOEZI HIILO NI JAMBO ZURI KUWEPO NAKWAMBA ILIKUWA NI MAKOSA KUSITISHWA MIAKA YA NYUMA KUTOKANA NA UKOSEFU WA FEDHA ZA UENDESHAJI NAKWAMBA KWA SASA SERIKALI ILILITAZAMA HILO NA KUONA NUMUHIMU KUREJESHA MAZOEZI HAYO.

Na Asha Juma, eddy blog Tarime

Related Posts:

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA